GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,747
- 109,200
Kuna kajitabia ambako binafsi nakaita ka ' kipuuzi ' kama siyo ka ' hovyo hovyo ' na ambako naona kanazidi tu kuota mizizi hasa kwa Watanzania wengi tena hasa wale so called ' intellectuals '. Miaka ya huko nyuma taarifa zozote ambazo zilikuwa zikitolewa katika hili ' jarida ' ambalo limeanza kujizolea ' umaarufu ' wa ghafla kwa sasa Watu walikuwa hawaziamini au hawazifuatilii.
Kwa siku za karibuni nimeshuhudia ' jarida ' hili hili la ' Forbes ' likija na taarifa ' fulani fulani ' ambazo kuna zingine kiukweli ukizifuatilia kwa jicho lako la tatu utakuja kukuta si za kweli lakini cha kushangaza siku hizi hili jarida limeonekana kuaminika mithili ya yule mnyama wa ' nadra ' na ambaye anaaminika mno na Watu pale anapoonekana sehemu yoyote aitwae Kakakuona.
Jana nilishikwa na ' butwaa ' kubwa sana baada ya kuona baadhi ya Magazeti na hadi Vyombo vya Habari Waandishi na Watangazaji wao wakiwa busy kwa ' kutiririka ' kuwaaminisha Watanzania juu ya taarifa ' fulani fulani ' hivi kitu ambacho kiuhalisia kama umebahatika kulisoma hilo jarida hicho kitu ' tunachoaminishwa ' hakipo na wala hakijazungumzwa hivyo tunavyoambiwa.
Namalizia kwa Swali kwenu je hili jarida la Forbes sasa limekuwa kama Kakakuona? Hivi Watanzania leo tumefikia hatua hadi ' akili ' zetu sasa zinaongozwa na jarida la Forbes? Hofu yangu kuna siku hawa hawa Forbes wanaweza wakaja na taarifa kuwa ukitaka uishi maisha marefu na ya ' kitajiri ' basi hakikisha unaenda Mbuga yoyote ya Wanyama na ukiwaona Simba wengi wamejikusanya mahala Wewe jipitishe tu pale tena ukiwa ' unacheka ' na ukifanikiwa kuwavuka basi unakuwa ' umeukata / umeula '.
Good morning!