Hivi hili ' jarida ' la Forbes ni mbadala wa ' Kakakuona? '

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,353
108,385
Kuna kajitabia ambako binafsi nakaita ka ' kipuuzi ' kama siyo ka ' hovyo hovyo ' na ambako naona kanazidi tu kuota mizizi hasa kwa Watanzania wengi tena hasa wale so called ' intellectuals '. Miaka ya huko nyuma taarifa zozote ambazo zilikuwa zikitolewa katika hili ' jarida ' ambalo limeanza kujizolea ' umaarufu ' wa ghafla kwa sasa Watu walikuwa hawaziamini au hawazifuatilii.

Kwa siku za karibuni nimeshuhudia ' jarida ' hili hili la ' Forbes ' likija na taarifa ' fulani fulani ' ambazo kuna zingine kiukweli ukizifuatilia kwa jicho lako la tatu utakuja kukuta si za kweli lakini cha kushangaza siku hizi hili jarida limeonekana kuaminika mithili ya yule mnyama wa ' nadra ' na ambaye anaaminika mno na Watu pale anapoonekana sehemu yoyote aitwae Kakakuona.

Jana nilishikwa na ' butwaa ' kubwa sana baada ya kuona baadhi ya Magazeti na hadi Vyombo vya Habari Waandishi na Watangazaji wao wakiwa busy kwa ' kutiririka ' kuwaaminisha Watanzania juu ya taarifa ' fulani fulani ' hivi kitu ambacho kiuhalisia kama umebahatika kulisoma hilo jarida hicho kitu ' tunachoaminishwa ' hakipo na wala hakijazungumzwa hivyo tunavyoambiwa.

Namalizia kwa Swali kwenu je hili jarida la Forbes sasa limekuwa kama Kakakuona? Hivi Watanzania leo tumefikia hatua hadi ' akili ' zetu sasa zinaongozwa na jarida la Forbes? Hofu yangu kuna siku hawa hawa Forbes wanaweza wakaja na taarifa kuwa ukitaka uishi maisha marefu na ya ' kitajiri ' basi hakikisha unaenda Mbuga yoyote ya Wanyama na ukiwaona Simba wengi wamejikusanya mahala Wewe jipitishe tu pale tena ukiwa ' unacheka ' na ukifanikiwa kuwavuka basi unakuwa ' umeukata / umeula '.

Good morning!
 
Kwa hiyo tukuamini wewe mpangusa viatu Vya wanene wa ufipa?

Au lile tambala lenu la kufungia maandazi linaloitwa Tanzania daima?
 
Tafadhali hebu wapishe Great Thinkers wachangie with a Critical mind juu ya hiki nilichokiweka na Wewe nenda kacheze na Marafiki zako wale ' Mende ' wa Chooni ambao kimsingi ndiyo unaendana kama siyo kufanana nao hasa ' kiakili '.
 
Mkuu wala usingepoteza mda kuandika,kwanza hile habari ni ya mwaka 2014.
Pili hile habari ni swali ambalo linasubiria majibu.
Hawa wandishi wa habari makanjanja wa Habari Leo na Uhuru wakaibeba hiyo habari hivyo hivyo.
 
Kwani hiyo habari inasemaje mkuu?
 
Hawa waandishi wa habari wa UHURU na HABARI LEO ni makanjanja wa kiwango cha Phd. Na ndiyo maana tuliuza mtambo wa kuchapia magzet, wacha waendelee kubeba Flash Disk na kupeleka kwa wahindi JAMANA.
 
Kwa hiyo tukuamini wewe mpangusa viatu Vya wanene wa ufipa?

Au lile tambala lenu la kufungia maandazi linaloitwa Tanzania daima?
Mbona mganga njaa unakuwa mkali hivyo? kha! unakuwa mkali kuliko hata maboss wako wanaokulipa book 7!
 
Back
Top Bottom