Hivi karibuni Julius Malema, kiongozi muasi na mbaguzi wa Umoja wa Vijana wa ANC, ambaye hata hivyo amefukuzwa uongozi na kuvuliwa uanachama amenukuliwa akisema kwamba amepokea salaam za pongezi toka kwa wenyeviti wa Youth Leagues za ZANU PF na CCM. Taarifa hiyo imekariri na kunukuu salaam zilizotumwa na Benno Malisa (Benno Malema) akimuita Malema kama shujaa. Kitendo hiki kimeuudhi uongozi wa ANC.
Bila kujali kwamba CCM itachukua hatua gani dhidi yake, swali la kujiuliza ni kwamba je, Malisa amepongeza uasi huo wa Malema au alichopongeza na kukiona cha maana ni ubaguzi uliojikita katika hulka ya Malema? Je, mapenzi yake kwa Malema yanaweza kutafsiriwa kuwa chanzo cha uasi wake kwa Chama chake, Kama tulivyoushuhudia hivi karibuni?