Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

RIWAYA: Historia Batili (Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba( Jk)
+255718274130
+255719274130

EPISODE 21
2⃣1⃣
ILIPOISHIA...
Hisham amempigia simu Khatib kumueleza juu ya majibu ya HIV yalivyokuwa kwa Regina, Khatib anamshauri Hisham atekeleze mauaji halafu watatengeneza ushahidi.
Je, Hisham atafanikisha mauaji??
Hii hapa Historia Batili na Mtunzi wako Jk..

SONGA NAYO.....
Baada ya kukata simu ya Hisham, Khatib aliona ampigie mamaake tena kwa mara nyingine..
“Unajua nilisema sitaki kuonana na Mzee J4 kabisa leo, lakini nafikiria kwanini nisionane nae tu ili nikiondoka huku niwe nimemaliza kazi? Maana mambo mengi sana sidhani kama nitaweza kurudi tena huku, na nisipokuja kuonana nae si ataona nimemdharau?” Alijaribu kushauriana na mamaake.
“Kama ni hivyo sawa, ila usiende mpaka nimpigie Sheikh Lesangwa simu kwanza.. Akituruhusu utaenda” Mama Mdharuba alishauri.
“Mama, nimekwambia jambo la Mzee J4 liacheni, acha kabisa kumpigia simu Lesangwa..acheni tu mimi niende nikaonane nae, naamini hawezi kuniita kwa ubaya” Khatib alionyesha msimamo wake kuhusu Mzee J4, yeye aliamini Mzee J4 ni mtu mstaarabu sana, na hawezi kuwa na nia mbaya na yeye..
“Naona siku hizi umekua, haya fanya unavyotaka” Mama Mdharuba alikasirika na kukata simu. Khatib akawasha gari yake mpaka nyumbani kwa Marehemu mkewe. Bahati nzuri na Mzee J4 naye alimkuta, wakasalimiana na kuongea mambo mengi na wanafamilia..lakini cha ajabu ambacho kilimpa maswali mengi sana Khatib ni kuwa hakuna aliyemuongelesha wala kumuuliza kuhusu kutofika kwake katika arubain ya marehemu mkewe.. Kichwa chake kilijawa na mawazo mengi..alijifikiri sana, na kuhisi amewakosea sana hawa wazee... Ila aliamua na yeye kupotezea..
“Nadhani muda wowote ambao mtakua tayari mniambie ili nitafute usafiri wa kuvihamisha vile vitu vya marehemu vije huku” Jambo la mwisho aliloamua kuliongelea Khatib kuhusu mirathi ya Sauda.
“Siku yoyote wewe panga tu sisi tutamuagiza mtu” Mama Sauda aliamua kujibu ili kuondoa utata na kufupisha habari ili jambo lisiwe refu.
“Sawa basi, nitaweka mambo sawa halafu tutawasiliana” Khatib alikubaliana na rai ya mama mzazi wa marehemu mke wake, kisha akamuangalia Mzee J4, “Safari hii pia imeitika wito wako Mzee J4, vipi tunaongea hapa au unataka faragha kidogo?”
“Maongezi yangu mimi na wewe ni maongezi ya kiume bana, hakuna haja ya kusikilizwa na wanawake” Mzee J4 alitania na kuwafanya wote waliopo pale wacheke..
“Sawa basi, mimi jamani naomba niwaage, jamani tutaonana tena, siku mbili hizihizi” Khatib aliwaaga wanafamilia huku akiwapa mikono kila mmoja.. Baada ya hapo akageuka kuelekea nje ambapo Mzee J4 alimfuata. Wakaingia kwenye gari na Khatib akawasha gari wakaelekea moja kwa moja maeneo ya Mkonge hotel ambapo Khatib alihisi kutokana na utulivu uliopo hotelini pale, pangekua ni sehemu sahihi zaidi kwenda kufanya mazungumzo na Mzee J4. Mzee J4 hakupinga wazo hili, wakaongozana. Wakafika na kukaa katika viti vilivyoizunguka meza moja iliyojitenga katika mti mmoja ulio katika bustani ya Hotel ile iliyokuwa na mandhari ya kuvutia, muhudumu ambaye alikua makini tangu wanaingia, alikuja haraka na kuwauliza watatumia nini..
“Nipe maji, yasiwe baridi” Mzee J4 ndiye alikua wa kwanza kuagiza.
“Kuna uhai, Dasani, Kilimanjaro, Mt Uluguru, Usambara na Udzungwa, nikupe yapi?” Aliuliza Muhudumu ambaye alimtaka Mzee J4 awe 'specific' bila kujua kuwa ataitibua akili ya huyu Mzee hivi karibuni.
“Wewe lete hata ya bombani hata yawe kwenye kibakuli, mradi tu yasiwe ya baridi” Ndivyo alivyojibu.
“Mimi niletee Mountain Dew.. ya baridi” Khatib aliongea baada tu ya mhudumu kumuangalia..
Baada ya kuletewa, maongezi yao yakaanza..
“Kiukweli unajitahidi sana katika kazi zako, unafanya vizuri mno, na kwa vijana wenzio wenye umri kama wako nadhani wana vingi sana vya kujifunza kutoka kwako, ilaaaa..nimeanza kuwa na mashaka na utajiri wako, kwa kiasi kikubwa upo vizuri sana, lakini unaonekana ni mtu mwenye tamaa sana..” Mzee J4 hakuona sababu ya kupindisha maneno, akaona agonge msumari moja kwa moja.
“Mimi usinione hivi hapa leo, nimepitia mambo mengi saana..yaani nimepitia mengi mazito, na kuna muda niliishi maisha ya shida sana..ilishafika kipindi nikawa 'Pastor' tena ilikua Afrika Kusini.. Nikikuangalia wewe nakuona ndani kabisa katika mambo ambayo watu wengine hawawezi kuyaona.. Mimi nataka nikushauri kitu kimoja, ambacho kitakuweka salama zaidi kuliko unavyofanya sasa.. Dhambi ya kuua huwa inazunguka, ogopa sana damu za watu..ni kitu kibaya sana kuua..kibaya sana..sana tena sana..” Mzee J4 ambaye alikua akiongea bila kumpa Khatib nafasi ya kutia neno, aliendelea kusisitiza kuwa mauaji sio mazuri.. Na kumfanya aanze kukumbuka maneno ya Hisham ambayo alimwambia wakati akimueleza kuhusu Mzee J4, akakubali kuwa ni kweli huyu Mzee alimwambia Hisham kuhusu kuua..Hapa alijifunza pia kuwa Mzee J4 anafahamu sana kuhusu kifo cha Sauda..wazo la kumkimbia kwa hoja au kumkatalia kama alivyotaka kufanya, akalifuta. Safari hii alikua akimsikiliza kww makini sana ili akimaliza akiri makosa yake halafu ampe wazo Mzee J4 kama atakubali kuwa mmoja kati ya 'Surbodinates' wake.
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Hisham, pamoja na kuwa unanifariji sana, lakini najua kuwa huwezi kuendelea kuishi na mimi tena, huwezi Hisham, nakufahamu vizuri na naijua hatma yangu endapo nitaendelea kukaa na wewe hapa Hisham..” Baada ya machozi kukauka, Regina aliamua kutoa ya moyoni. Alishaishi na Hisham kwa miaka saba sasa, sio mtu wa aina hiyo eti aweze kuvumilia usaliti ambao umemfanya akwae na ukimwi, alijua kuwa hii kwa Hisham ni 'geresha -----' tu, na kama angejipendekeza kulala hata usiku mmoja tu 'ingekula kwake'..
“Unataka kunambia kuwa huniamini? Hisham wa kipindi kile sio Hisham wa sasa..mimi nakupenda sana mke wangu, ni kazi ngumu sana kwa sasa kwenda kuanzisha uhusiano na mtu mpya nisiyemjua vizuri..nitapata tabu, naomba usiondoke, baki hapa kwa ajili yangu mke wangu, au unataka kuniwekea picha mbaya kwa watu kuwa nimekufukuza sababu umeathirika? Tafadhali usifanye hivyo” Hisham alimbembeleza Regina mpaka akafikia kutokwa na machozi, kitendo kilichomfanya Regina alainike.. Akaamua kubaki nyumbani, licha ya kuwa na wasiwasi mkubwa..
Akaanza kukumbuka alipokutana na Hisham kwa mara ya kwanza, usiku wakati Hisham akiwa amelewa sana na kumkuta amelala katika mtaro uliokuwa pembeni ya nyumba ambayo Regina alikuwa akiitumia kama danguro..
Alishangazwa na muonekano wa mlevi yule ambaye alikuwa mtanashati, akaamua kumsaidia.. Ndio kutokea hapo wakazoeana mpka wakafikia hatua ya kuwa wapenzi na mwisho kabisa wakaamua kuoana..na ni kwa ushauri wa Hisham ndo Regina akaacha biashara ile haramu..akamiliki baadhi ya maduka ya vtu mbalimbali pale mjini, Hisham akiwa bado anasafiri sana nje kwenda kuchukua 'unga' kama alivyoagizwa na mabosi wake, mpaka alipokutana na Khatib Canada na kumfanya rafiki, ambaye leo hii ndiye amemfikisha hapa.. Regina alikua na majuto makubwa sana, ila hakuwa na cha kufanya.
Hisham nae alikua na mawazo mengi sana juu ya Regina, hasira alizokuwa nazo ni zaidi ya simba jike aliyefiwa na mwanawe.. Kazi ya kubembeleza ilishaisha na kwa sasa alikua bize sana na simu yake kuangalia 'contact' ambayo huenda angeipunguzia mzigo ule wa mawazo, walau kwa kumpa taarifa tu, habari ile ya Regina ilimuelemea sana, ingawa alijikaza kiume mbele ya Regina kwani hakutaka afahamu mpango wake..
Akiwa ametulia bado 'akisearch contacts' zake, simu yake iliita, alikuwa ni Dr Mwinyi.
“Vipi umemaliza hiyo kazi?” Aliuliza Dr Mwinyi mara tu baada ya simu yake kupokelewa..
“Kazi gani tena Dokta?” Hisham anaonekana hakuwa 'aware' kabisa na anachokiulizia Dr Mwinyi.
"Khatib amenitaka nitengeneze ushahidi na kunambia muda si mrefu unakuja na mwili..sasa nimeona kimya ndo maana nikakupigia kukuuliza..”
Hisham aliduwaa, akamuangalia mkewe ambaye alikua amelala chali pale kitandani macho yake yakiwa yanaangalia 'gypsum' ya chumbani mle.. Hisham akakosa jibu la kutoa.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Je, Mpango wa mauaji utakamilika??
Je, unajua Mzee J4 atampa ushauri gani Khatib??
Huu ni mwanzo tu..kuna zaidi ya episode 300 zinakuja..

Usiache pia kufollow: jk.stories huko instagram..utapitwaa..

Tukutane Episode ya 22..
 
Wadau mnivumilie kidooogoo mambo ya shule yamenibana sana, ila ntajitahidi niwe naleta episode mbili kila weekend,, mpaka mwezi wa 6 utakapoisha, baada ya hapo kila siku nitakua naleta episode moja..
Ila leo nitaweka episode moja, baaadaee..
Nawapenda wote, story itaendelea wala msijali.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Wadau mnivumilie kidooogoo mambo ya shule yamenibana sana, ila ntajitahidi niwe naleta episode mbili kila weekend,, mpaka mwezi wa 6 utakapoisha, baada ya hapo kila siku nitakua naleta episode moja..
Ila leo nitaweka episode moja, baaadaee..
Nawapenda wote, story itaendelea wala msijali.

Ok masomo mema mydia, God b with u
 
Pole, najua vyuo vingi tarehe 15 wanaanza mitihani, komaa mwaya......

Wadau mnivumilie kidooogoo mambo ya shule yamenibana sana, ila ntajitahidi niwe naleta episode mbili kila weekend,, mpaka mwezi wa 6 utakapoisha, baada ya hapo kila siku nitakua naleta episode moja..
Ila leo nitaweka episode moja, baaadaee..
Nawapenda wote, story itaendelea wala msijali.
 
RIWAYA: Historia Batili (Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba (Jk)
+255718274130

EPISODE O22
★★★★★★★★★★★★★★★★
ILIPOISHIA..
Mzee J4 anataka kumpa ushauri Khatib apate cha kufanya na kujiepusha na mauaji anayoendelea nayo.
Huku nako Dr Mwinyi anampigia simu Hisham kutaka kujua kama tayari amekamilisha mauaji ili watengeneze ushahidi haraka, hii ni baada ya Dr Mwinyi kupigiwa simu na Khatib na kupewa maelekezo.

SASA ENDELEAA..
Baada ya kukosa cha kumjibu Dr Mwinyi,Hisham alikata simu. Regina, pamoja na mawazo tele aliyokuwa nayo kichwani kwake, aliigundua ile simu aliyoipokea mumewe kuwa ilimuhusu kwa namna moja au nyingine. Pamoja na kufarijiwa sana na Hisham mpaka akaamua kubaki pale, lakini wasiwasi juu ya hatma ya maisha yake ulikua mkubwa.. Alimfuatilia vizuri Hisham tangu anapokea simu, na jinsi alivyogeuka kumuangalia kabla ya kukata simu. Akahisi kuna jambo. Bahati nzuri Regina alipata kufahamu vitu vingi kuhusu Khatib kupitia mumewe-Hisham. Hivyo alifahamu kuwa kama jambo lake la kukutwa na HIV atashirikishwa Khatib, kulikua hakuna namna nyingine zaidi ya yeye kuuwawa..na kwa jinsi pia anavyofahamu uhusiano wa Hisham na Khatib ulivyo, aliamini kuwa mpaka sasa Khatib ana taarifa zake. Hata hapa aliposikia mumewe akitaja neno Dokta, alijua kuwa tayari 'kimenuka'. Hapa akili yake iliwaza kitu kimoja tu-Kutoroka.. Alishapanga kutolala nyumba hii leo, ingawa kichwa chake kiliuma kwani hakujua angetoka vipi pale.
“Nini tatizo mume wangu? Mbona unaonekana umeduwaa halafu umekata simu?” Regina aliamua kusikiliza jibu la Hisham kwa swali hili.
“Huyu Dokta nilikua na ahadi, nilipanga tukapime kwake, lakini sikwenda huko..ndo ananiuliza hivi maana nilimuahidi nitaenda nimkute, sasa kaona kimya” Hisham alidanganya, na kumfanya Regina awe na maswali mengi zaidi..
“Sasa kwanini umemkatia simu? Si ungemwambia ukweli tu kuwa tumeshapima hospitali nyingine?” Alichokuwa akikifanya Regina hapa ni kuendelea kupata ukweli tu kuwa kuna mpango maalum, na kwakuwa alimfahamu vizuri Hisham kuwa mara nyingi ni mwepesi wa kupanic akiambiwa ukweli, aliamua kukazia msumari.
“Nimekata ndio, kwani we huoni kuwa nimechanganyikiwa? Sasa nitamueleza nini yeye? Hebu achana na hizi habari za Dokta, kwanza simu si nimepigiwa mimi? Wewe mbona maswali mengi?” Hisham alipandisha sauti na kumfanya Regina ajue nini kinaendelea hapa.
“Basi mume wangu, samahani sana” Regina aliamua kuwa mpole.
Alilala pale kitandani na mawazo meengi sanaa.. Alijua kuwa Hisham leo hatatoka kwenda kazini kama kawaida yake, hilo alilifahamu kwani ni lazima Hisham atakua na mpango wa kumuua tu.
Hisham yeye alikuwa akiusubiri kwa hamu usiku wa leo, ili Regina atakapolala tu, ampake ile sumu ya unga maeneo ya puani ili ndani ya dakika 10 asiwe miongoni mwa watu hai wanaoishi duniani.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Labda niwaulize swali moja muhimu, hivi mnafikiri nyinyi ni nani katika nchi hii?” Ally Ngoswe alikuwa amewatolea macho Detective Rukia na Ahmed Khamis baada ya kuwaita ofisini kwake. Licha ya kuwa alishirikiana kwa karibu sana na Noor, ila Ally Ngoswe alipinga wazo la Noor na Khatib kutaka kumuua Ahmed. Aliamini kwa kumuua Ahmed mambo yangevurugika zaidi katika idara hiyo, na huenda Ngoswe angebeba mzigo mkubwa wa lawama ambao ungeambatana na uchunguzi mzito. Na kwakuwa alishamuonyesha Detective Rukia wazi kuwa alipinga jambo la Ahmed kwenda Canada wakati ni jambo liliokuwa likifanywa ndani ya misingi ya kiusalama, hivyo kuruhusu kufikia huko kwenye uchunguzi kungefanya yakaibuka mengi zaidi..
“Naomba tusamehe mkuu, hili kosa ni kubwa tumelifanya, tulidhani tukishakamilisha itakua bora zaidi kukufahamisha. Ila sisi tunakiri tumekosea, na tunakuahidi kosa halitojirudia mkuu” Rukia alijitetea kwa niaba yao wawili.
“Sitaruhusu ujinga huu ujitokeze tena, na kuanzia sasa hiyo kesi ya Khatib naitoa mikononi mwenu, na nitaikabidhi kwa wengine.. Na Ahmed urudi kule shule ukawaage, tutatengeneza uhamisho ndani ya wiki moja urudi hapa nijue nitakupanga wapi, Detective nitakupangia kazi nyingine mbali na hii. Halafu naomba ripoti ya Nuro nijue nae namkabidhi jukumu lipi, ingawa yeye ataendelea kubaki kulekule.. Sihitaji maelezo mengine ya ziada..hii ni Command!” Ally Ngoswe ndivyo alivyomaliza na kuwaonyesha ishara wawili wale watoke nje.
Ahmed na Rukia walitoka nje ya ofisi ile huku wameinamisha vichwa vyao, hawakujua sababu haswa ya 'boss' wao kuamua vile. Wakaanza kuhisi kuna mchezo mchafu nyuma yao. Rukia akatoa simu yake katika pochi yake ndogo ya rangi ya pink aliyokuwa ameshikilia mkononi, akaamua kumpigia Nuro huku akitembea kurudi ofisini kwake.
“Mwenzangu, leo wenzako tumebadilishwa vitengo na boss..tumetolewa kwenye hiyo 'case' ya Khatib” Rukia aliongea baada ya salamu.
“Yaah, nililitegemea hilo tangu ile siku ulivyonambia 'boss' alikuita ofisini na kukuuliza kuhusu Ahmed..” Nuro hakuonekana kushtushwa na hii habari, ila akaamua kumpa Rukia habari zingine ambazo hakuzifahamu kabisa..
“Unajua mimi nafahamiana sana na Noor, yaani ni mtu wangu wa karibu haswa, yeye ndiye aliyenitafuta na kuniambia nimtafutie Khatib mke, yaani nina maelewano naye mazuri sana tangu zamani, nikipata siku ntakueleza nilifahamiana nae vipi, ila mpaka leo yeye hajui kuwa mimi ni Usalama” Maelezo haya yalimfumbua macho Rukia, ila alikua hajapata mwanga haswa Noor anahusika vipi katika 'issue' ya boss Ally, akaamua kuendelea kusikiliza bila kutia neno zaidi ya kusema "Heeh" na kumfanya Nuro aendelee na maongezi.
“Sasa hivi karibuni ndio nimekuja kugundua kuwa 'boss' na Noor wana urafiki mkubwa, tena kuna biashara wanashirikiana..”
“Duuh.. Makubwa haya!” Rukia alijikuta akihamaki.
“Ndo hivyo mama, madogo yana nafuu..” Nuro aliongea kirafiki zaidi wakati huu, sio kama mtu anayeongea na boss wake.
“Sasa kama boss anashirikiana na Noor sisi tutakua na la maana kweli? Maana yule Noor ndiye ambaye muda wote anafikiria kumlinda Khatib tu” Rukia alionyesha kuchoshwa na maelezo haya.
“Ndo hivyo, Noor ndiye chanzo kikubwa cha Ahmed kumuua Alice, nadhani unakumbuka, yule baba ni hatari kuliko hata huyo Khatib mwenyewe”
“Nakumbuka, uliniambia, kwahiyo hata hizo damu za watu wasio na hatia kina Alice na Sauda tutaziacha ziteketee hivyo” Rukia alionyeshwa kukerwa sana na Ally Ngoswe..
“Ndo hivyo, fuata 'order' Detective, tusije na sisi tukapotea buree”
“Hilo nalo nenoo..” Alimalizia hvyo Rukia kisha wakaagana na kukata simu.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Kuwa mtu wa busara, toa sana sadaka, onyesha kila unachomiliki ili watu wakujue vizuri..kwakweli utaishi kwa amani sana” Mzee J4 aliamua kutoa ushauri wake. Khatib alikuwa bado yupo kimya akimsikiliza.
“Kwakweli ukiwa muwazi hakuna mtu atayekufikiria vibaya, kwani wangapi wamerithi mali za baba zao hapa nchini kwetu na bado wanaonekana watu wazuri tu kwenye jamii? Sasa wewe pia si inasemekana umerithi? Kwanini machoni pa watu usiwe mzuri? Acha mambo ya ajabu kuanzia sasa, jiweke juu kama mfano, watu watakuheshimu, hebu watoe wasiwasi watu ndugu yangu, watu wamekuwa na wasiwasi na wewe..waonyeshe kuwa wewe ni mtu mzuri, kwanini unaendelea kujizolea sifa mbovu wakati nafasi ya kusawazisha unayo?” Mzee J4 aliongea maneno toka moyoni.. Na alifanikiwa kuyapenyeza maneno yale moja kwa moja kwenye moyo wa Khatib. Ila katika kichwa cha Khatib kulikuwa na maswali mengi sanaa, kwanini huyu Mzee anamtaka afanye hivi? Yeye anafaidika nini? Na kwanini amshauri mambo hayo wakati anafahamu ukweli kabisa kuwa alimuua Sauda? Kwanini bado yuko upande wake na kumsihi abadilike? Au Mzee J4 alikuwa anahitaji kitu kutoka kwake? Maswali yote hayo hayakujibika katika kichwa chake.
“Mzee mimi nimekuelewa sana, na nakuahidi nitalifanyia kazi hilo ndani ya muda mfupi” Khatib alimuahidi Mzee J4, ila alikuwa na swali ambalo alipanga lazima amuulize leo.
“Ila natamani kujua hizi habari zote wewe unazijuaje, mpaka kufikia kunambia kwa kujiamini kuwa nimemuua mke wangu?”
“Mimi najua kila kitu unachofanya, na kila hatua unayopitia, najua kuwa wewe jina lako Mwatete Mwinjuma, najua pia kuwa ulitokea katika familia ya kimasikini tu na ukaja kusaidiwa kimaisha na mzungu mmoja mwenye asili ya Canada na baadae kumfanya mwanamke wako licha ya kuwa amekuzidi miaka 24, na najua pia kuwa unamiliki Euler Hotel na Mambo Pub pale Morogoro pamoja na ile Hotel ya Dar anayosimamia mamaako, nafahamu vizuri pia ushauri wako uliompa Hisham muda mfupi uliopita ukitaka amuue mkewe, na hata kabla hujakuja nyumbani leo nafahamu ulikuwa Hotel na mama wa mtoto wako Abdul ambaye umemwachia milioni 1.3 wakati mnaagana.. Kiufupi nakujua sana ndani nje, mimi naijua HISTORIA BATILI yako, na nina nafasi kubwa sana ya kukufanyia vyovyote utakaponikera..” Mzee J4 alifunguka kuhusu HISTORIA BATILI ya Khatib ambayo ilikua ikijulikana kuwa alikulia katika maisha ya kitajiri na kumbe si hivyo.. Hapa Khatib aliduwaa.
“Kunikera kwangu ni kutofuata ninachokushauri, nimekusamehe moja kwa moja kwa kumuua kipenzi cha mdogo wangu nimpendaye.. Lakini siku zijazo sitakusamehe kwa lolote, hivyo naomba twende sawa kutokea sasa” Mzee J4 alionekana kubadilika ghafla, Khatib alikua kwenye wakati mgumu sana ambao hakuwahi kuutegemea.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Haya sasaa.. Fumbo la muda mrefu linafumbuliwa na Mzee J4, tunaanza kuijua HISTORIA BATILI ya Khatib. Hapa ndipo story yetu inapoanzia..
Utamu unaanza hapaa...

Ila kwa leo, tukomee hapa..
Tukutane Episode ya 023.

Usiache kufollow IG:mad: jk.stories kwa story tam zaid, updates na mambo mengine kibaaaaoooo..
Kaa tayari pia kusoma kitabu cha HISTORIA BATILI kinakuja hivi karibuni.
Una maswali? Maoni? Usiache kuandika kupitia mdharuba@gmail.com
Au
Call/sms @ +255718274130/+255654727266
 
Hatimaye nimefanikiwa kuileta episode, niombeeni Mungu shule iishe vizuri..tuko pamoja!!
 
  • Thanks
Reactions: ram
ekhee! kwelin hii riwaya kali. Huyo mzee J4 anatumia sayansi gani kuyajua yote hayo?
 
Back
Top Bottom