Hilo sio shamba lako

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,232
754
1.Ewe malenga mahiri,mie mgeni wako,
Lillilo kwako shuburi,sio tamu kwa mwenzako,
Leo naomba hubiri,utambue vya wenzako,
Wapandaje mbegu zako,hilo sio shamba lako

2.Hilo sio shamba lako,wapandaje mbegu zako,
Cha mwenzio sio chako,hiyo sio mali yako,
Wahangaika wenzako,wajilia kama vyako,
Wapandaje mbegu zako,hilo sio shamba lako

3.Kwanini wajivunia,kwa kupanda ya wenzako,
Ipo siku tajutia,upate adhabu yako,
Iwe mwiko yako nia,kupenda visivyo vyako,
Wapandaje mbegu zako,hilo sio shamba lako

4.Lipi unalo ogopa, kutayarisha la kwako,
Umekuwa kama papa,unatishia wenzako,
Utakuja toka kapa, ndio uwe mwisho wako,
Wapandaje mbegu zako,hilo sio shamba lako

5.Fahamu ya hili jiji,yalowafika wenzako,
Hatupendi wa rufiji,kwahiyo tabia yako,
Utakuja hama mji, ukimbie nyumba yako,
Wapandaje mbegu zako,hilo sio shamba lako

6.Nimefika kituoni,kwa tuhuma dhidi yako,
Yamenifika pomoni,kwahiyo tabia yako,
Malenga leta maoni,nipate mchango wako,
Wapandaje mbegu zako,hilo sio shamba lako

jidu!
 
Shairi limetulia vina vimekaa sawa haya wajuzi wa lugha tusaidieni

MS, Asprin tusaidieni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom