DEAR SON#

Aldonia

Member
Sep 13, 2016
20
14
DEAR SON#

Nilipanga uje mapema iLa mipango ya Mungu na..
Ni kweli nilitafuta kwa jasho na ulikuja kwa uchungu na..
Muda ni asset ila haidumu na inakuja kimafungu..
kama kuna kosa kubwa nilifanya ni kujaribu kubadili kila kitu kutafuta suluhu na watu ambao mikononi walishika virungu..

Ukaitwa Zak ni jina nililipenda sana.. ungeitwa Wallace means stranger ila niliona ni refu sana..nilitaka niongeze X uitwe Zak X ila X ingeleta mtafaruku sana..nilipenda uwe daktari na public speaker uitwe Dr Zak ni kitu mimi sikuweza fanya.

Nilietamani awe mamako kuna mahali tulishindwana tukagawana njia.. yule mwingine angenifaa kama mke asingekufaa kama mama nakwambia..Mwingine akasema kwao ni wa kwanza inabidi atafute pesa asaidie familia..Wengine zilikuwa ni infatuations..Mwingine pesa zikatuharibia..Muda huu ungekuwa na miaka kadhaa kama mipango na mawazo yangu yangetimia.. zile sauti za kuitwa baba Mkubwa na Baba Mdogo kabla yako kuna muda zilinichanganya pia.. nilikaza fuvu kama sijui kitu Tuli nikitafuta njia..

katika Tafuta Mashamba Nikapata Shamba Pia... Nikaanza Ulizia...ili nipate jua kama liko sawa au kuna migogoro ya kifamilia... nikaja jiridhisha kuwa lipo clear...kucheki niko na visenti kadhaa nilivyojisevia..Nikalilipia...Nikaanza Palilia na kutoa kila kitu nilichohisi kisingenivutia... Kwa ruhusa yake jaalia...Muda wa kupanda mbegu ukawadia na Mambo yakawa sawa sawia na... basi ni zile siku mia mbili sabini plus upo ndani umetulia...Hujui hili wala lile kila kitu anakufanyia...Nikitoa company kwa pembeni kama nahodha kwenye meli ya familia.. Na muda ukawadia sauti za kilio zikasikika wengine kwa uchungu wakifurahia...Wodi namba sikumbuki muulize mamako atakusimulia...nnachokumbuka ilikuwa ni siku ya furaha , uchungu na tumaini kwangu katika uso wa dunia..
kuna vitu nlikuwa sivielewi unajua... ni vile ndo mara ya kwanza kumuona mtoto akikua na mi nikiwa ndo muangalizi na msimamizi katika baridi joto mvua na jua... wakasema tumefanana sana nilitegemea... hizo stori za kuwa niko na common face nilisha zizoea na..
kuna kile chumba cha chini hukijui na hukuwahi kuingia..used to be my library en stress free zone...Funguo anazo mamako muombe atakupatia... kuwa makini kuna mechanical stuffs nyingi nili fix in... unajua nilikuwa mtundu nilipenda hesabu na fizikia.. so kila kitu nilikiset nilivyotaka na bila kujua hutopata unachotaka yan hutaweza hata kukifikia.. mamako ni smart sana kuwa nae atakusaidia...
kwenye Meza kubwa kuna autobiographies mbili... Moja ni ya Prophet na iLe yenye cover mtu kavaa miwani kama niliyokuachia ni ya Malcolm I mean Malcolm X zitakupa namna nyingine ya kufikiri..mimi sio mtabiri sio mbashiri iLa nilipenda kufikiri na niliamini katika ukweli yan moja na moja unapata mbili son..
Mpende Mamako na... Thamini sana mawazo yake hiyo ndo nguzo imara kwako..mimi ni heshima tu ndo nahitaji toka kwako.. Mwanaume hapendwi anaheshimiwa Zak.. Tunza imani unapoaminiwa .. Weka heshima unapoHeshimiwa .. Ficha Machozi yako unadhani nani atajali hisia na mateso yako..
utasema ni mama yako fine.. lkn huyo ni sehemu yako yan yeye na wewe ndo huyo mtu mmoja ambaye yupo upande wako Zak...
Binadamu hawana Wema .. kila ufanyalo liwe baya Jema..wakusema Watasema.. sasa Chaguo ni lako uwaskilize wao au uombe mungu upate baraka na siku njema..

Ukiwa na Heshima hutachukiwa na watu...Ukiwa na pesa utapendwa na watu.. Ukiwa na Pesa bila heshima utachukiwa na wenye hekima na maarifa ila bado utafatwa na watu...Ukiwa Mpole utadharauliwa na Watu..Ukiwa mpole bila pesa utanyanyaswa na watu..Ukiwa na Upole na Pesa Utatapeliwa na watu..Ukiwa na Nguvu Utaogopwa na Watu Ukiwa na Nguvu bila pesa Utatumiwa na watu...iLa Ukiwa na Nguvu , Heshima,Upole na Pesa utakuwa Mtu wa Watu Zak..
kati ya njia ya Utajiri na Hekima unapita njia gani ..? jibu utampa mamako kisha Utafata mawazo na busara zake kichwani..
Thamani ya mtu ni maamuzi yake..Thamani ya kitu ni mmiliki wake... Thamani ya pilipili ni muwasho wake..Kama ilivyo thamani ya nyota na mbalamwezi ni kwenye giza Lake.. Swali Unahisi Thamani ya maisha ya dunia yapo kwenye nini son..?

Nimezipata taarifa toka shuleni kwako..wasimamizi wanaridhishwa na tabia na juhudi zako...wengine wanafaidika na uwepo wako... wanakupa mapambio mengine sio ya size yako .. kuwa makini Zak ... wanaokupa sifa ndo hao wanaotamani waje walione anguko lako... usiamini sana sifa unazopewa na unaowaita rafiki zako..kuna muda wAna list ya marafiki zao ambao ni maadui zako..
hivi ulishasoma ile hadithi niloiandika kwa peni Nyekundu..? ndani niliweka kisa cha chanda chema na Pete Nyekundu vile ilivikwa bila tamaa na hiyana ikaziba matundu.

Ukubwa unakuja wenyewe na Matatizo hayapigi hodi.. utapoweza pambana mwenyewe maana misaada watakukata kodi..Ukivikosa ndani kavitafute nje huenda utavipata road.. kukata tamaa MWIKO,haipo kwenye MFUMO na mawazo over your dead body..
Ukishindwa kutafuta akutafutie nani...?Ukishindwa kujua akujulishe nani..? Ukishindwa kujipiga kifua,kuinua kichwa na kunyoosha mgongo unataka akufanyie nani..? Msaada wa kwanza unatoka kwako , ndani yako..hao wengine watafatia kulingana na mshale wako.. ukinyooka ni kheri na ukipinda ndo tatizo kwako..Sababu kanuni ya kwanza ya ubinadamu ni kuwajibika kwa maamuzi na makosa yako...
Zichunge hisia ukiwa peke yako...Ukiwa na Kundi chunga Ulimi wako... Ukiwa na Hasira ama Furaha yachunge maamuzi na ahadi zako...Ukiwa na haraka chunga hatua zako,Wakati wa njaa Chunga Sana akili yako , Ukiiruhusu ifike Tumboni hiyo ni hasara kwako na watu wa karibu yako son#

Nipate nafasi nije niwaone huko mlipo... naamini bado mpo wote Tangu siku sipo..mambo ni mengi na magumu sana huku nilipo.. ILa dua na mawazo yangu yapo kwenu kuliko kwangu sababu moja ya somo nililofundishwa na dunia ni kujua namna ya kupigana vita yangu peke yangu son#
Tutaonana Kwa Mapenzi yake Rahmani..Nawaombea kheri nyingi Amani..Tabasamu Lako mbele ya mama yako ni zawadi isiyo kifani.

DEAR SON#

Ukiisoma Usisahau Kutoa Maoni Yako.... Tutaendelea Na Andiko Jingine
Screenshot_20230601-032029_Chrome.jpg
 
View attachment 2658737

Duuh Hiii Nimeipenda Sana!Na Ni Elimu Kubwa Sana, Hongera Sana mkuu! Tunapenda Kuona JF wanatoa Uzi Kama Hizi Aisee!

Nasubiri Inayofwata
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom