Hili nimeliona sana tu kwa Walinzi wa Majumbani sehemu mbalimbali je, ni sahihi Kiulinzi au wanahitaji Msasa zaidi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,134
110,490
Haiingii Akilini Mlinzi unaagana nae Usiku Saa 4 unamuacha kakaa Lindoni huku Taa inammulika, ukiamka Usiku Kimachale ili nawe pia kufanya Lindo lako la Kisirisiri kwani Siku hizi hakuna Kuaminiana bado unamkuta kakaa pale pale Taa inammulika halafu Asubuhi ukiamka na Kukutana nae anakuambia Mazingira yako Salama wakati Wewe muda wote umemkuta akiwa pale pale ulipoagana nae jana Usiku wa Saa 4.

Halafu sasa kwa kuomba Nyongeza ya Mishahara wako vizuri kweli kweli. Mlinzi analinda Usiku huku Kafungulia Redio za Kisasa za Kichina kwanini Mwizi au Jambazi asijue uliko kisha akulie Timing aje Kukupiga Kitofa ( Jiwe la Utosini ) Ufe halafu aanze Kuiba?

Na wenye Walinzi punguzeni Mazoea nao sana kwani Wakishakuzoea tu hata ule Ufanisi wa Kazi hapo Kwako unapungua na sasa badala ya kukuona Wewe Mshikaji anaanza Kukuzoea kiasi kwamba hata Ratiba za Chakula chako na Familia anazijua au anataka Kuzijua na ukifanya mzaha hata Kukubandulia na Wanafamilia wako atakubandulia tu.

Shikamooni Walinzi.....!!
 
Kule kwetu nilikatiza usiku saa saba hivi kwenye hoteli fulani nikakuta walinzi wa sehemu zingine karbu wapo wote na redio na jiko la mkaa wanachoma mahindi cha ajabu walinikalibisha pia yaani hawaulizi unafanya nn usiku wao wanaangalia sura tu
 
Yaani kuna Comments nikisoma hapa huwa Nafurahi sana kwa Kucheka na hivi napenda Kucheka na Utani basi ni Raha.
 
Haiingii Akilini Mlinzi unaagana nae Usiku Saa 4 unamuacha kakaa Lindoni huku Taa inammulika, ukiamka Usiku Kimachale ili nawe pia kufanya Lindo lako la Kisirisiri kwani Siku hizi hakuna Kuaminiana bado unamkuta kakaa pale pale Taa inammulika halafu Asubuhi ukiamka na Kukutana nae anakuambia Mazingira yako Salama wakati Wewe muda wote umemkuta akiwa pale pale ulipoagana nae jana Usiku wa Saa 4.

Halafu sasa kwa kuomba Nyongeza ya Mishahara wako vizuri kweli kweli. Mlinzi analinda Usiku huku Kafungulia Redio za Kisasa za Kichina kwanini Mwizi au Jambazi asijue uliko kisha akulie Timing aje Kukupiga Kitofa ( Jiwe la Utosini ) Ufe halafu aanze Kuiba?

Na wenye Walinzi punguzeni Mazoea nao sana kwani Wakishakuzoea tu hata ule Ufanisi wa Kazi hapo Kwako unapungua na sasa badala ya kukuona Wewe Mshikaji anaanza Kukuzoea kiasi kwamba hata Ratiba za Chakula chako na Familia anazijua au anataka Kuzijua na ukifanya mzaha hata Kukubandulia na Wanafamilia wako atakubandulia tu.

Shikamooni Walinzi.....!!
Mkuu umenikumbusha tulikuwa na mlinzi wetu wa kimakonde anapiga rimba usiku kucha na kusuka ukili nilipoona hii mada nimecheka sana hapo kwenye majambazi kumlia timmingi!
 
Mlinzi halindi chochote anakuwepo tu kukupa imani na kufanya vibaka wajue kuna mtu. Watu wa kazi wakiamua kuja kwako huyo mlinzi hakuna kitu anaweza kufanya kuwazuia.
Aaah tusitishane!
 
Ili ulinzi uweze kuwa na maana kidogo inabidi kuwepo na kupokezana,haiwezekani mtu mmoja afanye kazi hiyohiyo kuanzia sa kumi na mbili jioni mpaka asubuhi sana sana itakuwa ni kulala
Kitaalamu kuchange order ni after two hours,sasa imagine mtu asugue 12 hrs
 
Unakuta mlinzi kibabu cha miaka 60. Kimekondeana kwa lishe duni. Silaha pekee anayomiliki ni rungu na firimbi. Halafu jitu linakoroma ndani akiamini analindwa.

Likitokea la kutokea mlinzi anaomba msaada kwako anaepaswa kukulinda.

Wabongo huwa tunashindwa kutofautisha shamba/boy/mfungua gate na mlinzi. Tunachukulia ulinzi kiwepesi kabisa.

Dunia ya leo mambo ya kuweka wamasai mlangoni yamepitwa na wakati. Ni mwendo wa electric fence, motion detectors, CCTV na kuwa na cha moto ndani. Ukisikia purukushani nje unamfyatua mtu za matako.

Baada ya yote mlinzi ni Mungu tu, mengine mbwembwe.
 
Back
Top Bottom