Hili limekaaje wadau? Huyu manzi atakuwa anamaanisha nini?

Melancholic

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,831
3,063
Kuna binti mmoja ni mama lishe. Ni mdada mzuri sana, kama mnavyojua wadada wanaofanya hizi shughuli za umama lishe, tena ukiwa mzuri kuna kuwa na mtiririko wa wanaume kuomba namba kila mara.

Na mimi mara nyingi huwa napoenda kwenye shughuli zangu, ni lazima nipitie hapo kwenye mgahawa wao kupata chakula, lakini yule mdada akaanza kuniletea mazoea. Ila mimi nilisita kumtongoza kutokana na jinsi navyomuona mara nyingi yupo bize na simu. Nkaona nisionekani kati ya watu wanaomshobokea, lakini mara nyingine huwa naenda pale na mpenzi wangu, lakini yule mdada anakuwa ananiangalia sana na mimi nakuwa kama simjali. Na mara nyingine ananiomba hela ndogo ndogo, na huwa nampa, halafu namkaushia.

Lakini juzi nimeenda kula akaniuliza, "Leo mpenzi wako yupo wapi?" Nkamwambia, "Yule sio mpenzi wangu." Akakataa kwamba namdanganya. Nkamwambia, "Po, halafu nkamuomba namba." Akawa kama kahamaki, nkamuuliza kuna shida, akasema hapana. Baadae akanipa namba, ila kwenye akili yake nkaona kabisa kajua nataka kumtongoza, kumbe mimi nilichukua namba kwa ajili ya kunifanyia delivery ya msosi. Maana sikai mbali na ulipo mgahawa wao. Siku hiyo ilikuwa Jumamosi, sikumtafuta, tukaja kuonana jana nilipoenda kula. Ila yule binti naona kama kangiwa na unyonge sana, halafu naona anichangamkii pia ananiangalia kama ananitafakari sana.

Sasa leo ndio nimempigia simu, nkamwambia niletee msosi mitaa flani. Bac akuja yeye akaleta binti mwingine, ila wakati wa kuja kuchukua ela, kaja mwenyewe, na akujua kama ni mimi ndio nlimuagiza msosi, bac akanicheka kwa hewa. Nikamuelekeza akaja, nikatoka getini alivyoniona ni mimi, akashangaa, halafu akaniambia, "Kumbe ni wewe?" Nkamwambia, "Ndio." Akasema, "Ningejua ni wewe hata nisingekuja." Nkamuuliza kwanini, akasema, "Bac tu." Akachukua pesa akasepa.

Hivi, hili limekaaje wadau? Huyu manzi atakuwa anamaanisha nini?
 
b8022b17-edd5-40d8-9417-d90715e97894.jpg
 
mkuu hapo huyo mtoto ushamaliza,actions speaks louder than words.

1.hujataka kabisa kumshobokea

2.umeshow up na manzi yako.

3.unampa mpa vichenji chenji.

4.ukaomba namba then unamtafta kwa kazi maalumu.

Aseee umecheza kama pele mkuu,sasa swali lange je,unataka umle kimasikhara au unamzingua tu,coz huyo mtoto hachomoki hapo.

Mi nna kisa kama chako,ntaleta one day.
 
Back
Top Bottom