Hili lililomkuta Bashe liwe fundisho kwa Mawaziri

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Leo Waziri wa Kilimo ametamka hadharani kuurejesha Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea BPS ambao ulifutwa Juni 2021 na kusababisha mfumko mkubwa wa bei za Mbolea nchini kwani wafanyabiashara waliuza mbolea kwa bei wanayoitaka wao bila kuwepo usimamizi wa Serikali.

Jambo hili lililalamikiwa sana na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina bungeni lakini Waziri Bashe alitangaza bungeni kumshutumu Mpina kwamba nI Mbunge wa muda mrefu ni hatari kupotosha Bunge na kwamba kwenye suala mbolea yuko tayari kwa lolote juu ya anachokiamini kuhusu mbolea na alitumia neno Im ready to bare any cost for what is what i believe. sasa kwa hili ni vizuri Bashe akachukua hatua kwa kujiuzulu kama alivyolitangazia Bunge

 
Nadhani ni jambo Jema kama yeye na wataalam wale wamegundua kwamba kulikua na kasoro kwenye maamuzi ya awali
 
Namkubali Sana Bashe , sometimes mda huwa unatuelewesha , hii pia inatosha kuonyesha kuwa mwamba huwa anafuatilia na kukubali alipoanguka
 
Back
Top Bottom