Hili la rais Kagame mnalionaje?

smart people huwa wana vision nyerere asingewasomesha hawa viongozi wetu hadi chuo kikuu bure hali ingekuwaje leo ,naunga mkono hoja uwekezaji kwenye elimu kagame yuko sahihi.
 
rais kagame amechukua vijana bright wanaotakiwa kuendelea na elimu ya juu na kuwaombea scholarship na wengine kuwalipia elimu ya juu kwenye vyuo maarufu marekani ili baadae waje kuitumikia nchi yao.
Kitendo alichofanya rais kagame pamoja na udikteta wake lakini kitaifanya rwanda kuwa nchi yenye maendeleo makubwa baada ya miaka 5 kuanzia sasa kwani watakuwa na wataalamu wa kila fani.
Wakati rwanda wanafanya hayo sisi tumeendelea kusaini mikataba ya madini na gesi wakati hatujajiandaa kwa kusomesha wataalamu wetu na pia tunasaini mikataba bila kuwa na sera yoyote ya uchimbaji madini na gesi.
Pia tumeshindwa kusomesha wataalamu wetu na badala yake viongozi wa serikali wametumia nafasi walizonazo kusomesha watoto wao na kuwapa nafasi kwenye nyazifa nzito kama bot,kwenye ubalozi na sehemu nyingine wameshindwa kuimarisha elimu na kugawa keki ya taifa kwa watanzania wote

maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana, chukua hatua
 
;

Mimi nionavyo kwanza nikupongeze kwa kufuatilia kinachojiri kwa nchi zinazotuzunguka (JIRANI) huo ndio ujirani mwema siku zote..., naomba tu kutofautiana na wewe eneo moja tu kwamba Kagame ni dikiteta, hayo ni mambo ya magazeti hajawahi kuwa dikiteta hata siku moja. Ni mtu anayependa vitu viende kwa kufuata cheria, kanuni na taratibu, amechaguliwa kidemocrasia wakati wote, kuna mahakama na kila akoseaye sheria inachukua mkondo wake, ameweza kufuta adhabu ya kifo, ni nchi peke yake Duniani yenye asilimia kubwa ya wabunge wanawake wengi . hapo udikiteta uko waapi.

Maendeleo Rwanda juwezi kulinganisha na nchi yoyote Africa hii.....!! ukiondoa South africa na Mauritius nafikiri, usafi, ruhwa zero torelance ngoja niache hapo kwa leo, na sisi tunahitaji kubadilika na kufuata nyayo.

Hapo umesema vitu ambavyo serikali na CCM hawapendi kusikia. Siku zote kama unataka kwenda hatua moja mbele you don't do it blindly. You benchmark youself with the best out there. Na ndicho kitu ambacho Ulimwengu kwenye makala zake amekuwa anatukumbusha ya kuwa viongozi wetu wanatembea sana sasa sijui maendeleo yaliyopigwa na nchi za wenzetu tena zisizokuwa ana raslimali kama zetu hawayaoni? Ametolea mfano wa Ethiopia. Na sasa kuna jirani zetu Kenya na Rwanda wanafanya vitu vinaonekana. Lakini viongozi wetu wa ajabu sana ukiwaambia tufanye as Ethiopia and Rwanda have dine wanakwambia kuwa yetu ni nchi ya demokrasia na Ethiopia ana Rwanda hawafati demokrasia. Nimesikia haya toka kwa Prof.Tibaijuka na Director General wa PCCB -Hosea. Sielewi hiyo demokrasia inayotudumaza tumeiga toka wapi? Tunaambiwa kuwa hatuwezi kufanya as Kagame does because of democracy. if that be the case kwanini hatukufata demokrasia hiyo wakati tunasainisha mikataba ya madini na gesi tukaitisha kura ya maoni na baadae tuka award contracts and kuzianika hadharani ili Mtazania ajue kinachoendelea? Why this fishy defence mechanism?
 
sasa kama kuna kitu hakitazamwi kabla ya mambo yote na sisi waafrika kwa ujumla ni kwamba nini cha kujifunza nini cha kuacha nini kitunzwe nini kidumishwe viongozi wengi tunaowaweka madarakani ni watu wa copy and paste na kuuwa ethics na utaifa wao kwa ujumla pia huwa hawana hata primary plans ndio maana wazungu huwa wanawafurahia kwa sababu kazi yao kubwa ni kuimport technology from abroad kitu ambacho huwa ni kuipika jamii ya nchi husika kuwa watu wa second au third priority technical and workers hii huwa ni sherehe kwa wazungu anachofanya kagame ni vitu special sana ambavyo havipendwi na marais mapandikizi kama watanzania na wazungu kwa ujumla kwa ujumla wakati sisi tunahubiri udini hatuoni hata aibu rwanda sasa inatuzidi kila kitu
 
katika leadership style a leader must contain all the model dictatorship,democratize, and leisure fair style na kila 1 inafanya kazi inapohitajika sasa wewe ukisema mwizi ameiba unamwambia kidemokrasia si atapanga majibu ya kuhalalisha wizi wake
 
smart people huwa wana vision nyerere asingewasomesha hawa viongozi wetu hadi chuo kikuu bure hali ingekuwaje leo ,naunga mkono hoja uwekezaji kwenye elimu kagame yuko sahihi.

Hawataki kufanya kama alivyofanya Nyerere na huku akiwa hachimbi madini, gesi wala hauzi mbuga za wanyama. Deni la Taifa halikuwa kubwa maana aliamini katika kujitegemea na elimu yetu ilikuwa of quality and standards. Lakini wenzetu wanachokifanya ni kupandisha hadhi taasisi za elimu alizoanzisha Nyerere kama incubators for professionals into University status bila maandalizi ya kutosha. Tusubiri bomu litakalokuja maana with a competitive EAC we will see how far will be lagging behind maana tutakuwa na so called wasomi with excellent certification but short of reason, critical and critique mind. "Education begins when you graduate" by Mwl Nyerere in one of the graduaations at Makerere University. It's applicability that will tell and not a good certificate. Sisi Tanzania tunajiaandaaje wakati tunajenga shule za kata ambazo hakuna hata mtoto mmoja wa kiongozi yuko mle? Tunapandisha taasisi kuwa universities amidst maandalizi duni. Viongozi wetu mnaotembelea JF tunayasema haya kwa uzalendo tuliokuwa nao kwa nchi. You brand us to be opposition fans au tusiokuwa na shukrani lakini ukweli unabaki palepale. Boresha elimu iwe bora na sio bora elimu kwa Watanzania wote kama alivyofanya Nyerere. Lete wanenu na wajukuu wenu kwenye shule za kata na mtaona kama hazitaboreka. Achana na mbio za zima moto za walimu wanaitwa voda fasta
 
sio tu wamepata rais mwenye kufikiria bali pia wananchi wanajua nini wanachokitaka katika nchi yao,hapa kwetu kama mazuzu tu ilimradi siku iende:photo::photo::photo::photo::photo:
Ni kwa sababu wamepata rais mwenye akili ya kufikiria. Ama sisi tumepata..
 
Rais kagame amechukua vijana bright wanaotakiwa kuendelea na elimu ya juu na kuwaombea scholarship na wengine kuwalipia elimu ya juu kwenye vyuo maarufu marekani ili baadae waje kuitumikia nchi yao.
Kitendo alichofanya rais kagame pamoja na udikteta wake lakini kitaifanya rwanda kuwa nchi yenye maendeleo makubwa baada ya miaka 5 kuanzia sasa kwani watakuwa na wataalamu wa kila fani.
Wakati rwanda wanafanya hayo sisi tumeendelea kusaini mikataba ya madini na gesi wakati hatujajiandaa kwa kusomesha wataalamu wetu na pia tunasaini mikataba bila kuwa na sera yoyote ya uchimbaji madini na gesi.
Pia tumeshindwa kusomesha wataalamu wetu na badala yake viongozi wa serikali wametumia nafasi walizonazo kusomesha watoto wao na kuwapa nafasi kwenye nyazifa nzito kama bot,kwenye ubalozi na sehemu nyingine wameshindwa kuimarisha elimu na kugawa keki ya taifa kwa watanzania wote

Wanafunzi wakitanzania wanaosoma na kufanya kazi nje ya nchi wapo wengi sana, kuna wataalamu wengi wa ki TZ wamezagaa nchi mbalimbali.Serikali ya CCM haijawahi na wala haina sera ya kutumia hivi vichwa vyenye exposure, utaalamu wa kutisha, kuna maacademicians, technicians na watu wenye proffessional za kutisha wa kitanzania wamesambaa humuhumu duniani.Lakini hakuna mipango yoyote ya kuwatumia watu kama hawa.Sijui hizo schoolership zilikuwa na malengo gani!wanatumikia tuu mataifa ya nje(brain drain).Kama suala la kuwalipa maslahi mazuri ni suala la mipango tuu kwakuwa outcome zao zitakuwa very productive ktk manufaa ya taifa.
Tatizo lingine la serikali ya ccm ipo bize sana kuitumikia SIASA (wanatumia resource nyingi ktk kuwekeza kwenye siasa za kutawala milele na kuwa bize kudhibiti upinzani) badala watumie muda mwingi na resources zaidi kwenye maendeleo ya kukuza uchumi na ustawi wa watu wake.Hata ukisoma dira zake za maendeleo ni porojo tuu na siasa siasa tuu.Hakunaga nia ya dhati tena ya kuondoa umasikini na kukuza uchumi.Mambo yote ya kitaalamu yameshafanywa ya kisiasa.Wimbo wa uzalendo na Maslahi ya kitaifa hakunaga tena.
 
Hii ndo njia wanayoitumia wachina kupeleka brilliant students kusoma ulaya na marekani kuchukua maarifa halafu kurudi nyumbani kusambazia ujuzi raia wote vyuoni. Hongera Kageme. Tanzania tutapeleka Wafanyasiasa ili waje na mbinu mpya za kuwadanganya Watanzania, kwani Tanzania kilakitu ni SIASA. Vijana wanamaliza vyuo vikuu na kutaka political positions tu.
 
;

Mimi nionavyo kwanza nikupongeze kwa kufuatilia kinachojiri kwa nchi zinazotuzunguka (JIRANI) huo ndio ujirani mwema siku zote..., naomba tu kutofautiana na wewe eneo moja tu kwamba Kagame ni dikiteta, hayo ni mambo ya magazeti hajawahi kuwa dikiteta hata siku moja. Ni mtu anayependa vitu viende kwa kufuata cheria, kanuni na taratibu, amechaguliwa kidemocrasia wakati wote, kuna mahakama na kila akoseaye sheria inachukua mkondo wake, ameweza kufuta adhabu ya kifo, ni nchi peke yake Duniani yenye asilimia kubwa ya wabunge wanawake wengi . hapo udikiteta uko waapi.

Maendeleo Rwanda juwezi kulinganisha na nchi yoyote Africa hii.....!! ukiondoa South africa na Mauritius nafikiri, usafi, ruhwa zero torelance ngoja niache hapo kwa leo, na sisi tunahitaji kubadilika na kufuata nyayo.
hapo natofautiana na wewe,..anna malecela,anna abdallah,yule mbunge wa nkenge,manyanya etc wote ni wanawake lakini majuha
 
Rais kagame amechukua vijana bright wanaotakiwa kuendelea na elimu ya juu na kuwaombea scholarship na wengine kuwalipia elimu ya juu kwenye vyuo maarufu marekani ili baadae waje kuitumikia nchi yao.
Kitendo alichofanya rais kagame pamoja na udikteta wake lakini kitaifanya rwanda kuwa nchi yenye maendeleo makubwa baada ya miaka 5 kuanzia sasa kwani watakuwa na wataalamu wa kila fani.
Wakati rwanda wanafanya hayo sisi tumeendelea kusaini mikataba ya madini na gesi wakati hatujajiandaa kwa kusomesha wataalamu wetu na pia tunasaini mikataba bila kuwa na sera yoyote ya uchimbaji madini na gesi.
Pia tumeshindwa kusomesha wataalamu wetu na badala yake viongozi wa serikali wametumia nafasi walizonazo kusomesha watoto wao na kuwapa nafasi kwenye nyazifa nzito kama bot,kwenye ubalozi na sehemu nyingine wameshindwa kuimarisha elimu na kugawa keki ya taifa kwa watanzania wote

Watu kama Kagame ndiyo wanaotakiwa Afrika, huu wimbo wa DEMOKRASIA na KUONGOZA KWA AWAMU ndiyo unaosababisha nchi nyingi Afrika Tanzania ikiwa mojawapo; kuwa na viongozi wasio waadilifu, waliojaa ubinafsi na uchu wa madaraka na ambao hawajali maendeleo ya nchi na wananchi wake kwa ujumla.

Kuwa DIKTETA haimaanishi kuwa unakandamiza haki bali unatoa mwongozo/maelekezo yanayofaa kwa mustakabali wa wananchi na taifa kwa ujumla. AKIWA NA DIKTETA ANAYEJALI HALI NA MAISHA YA WANANCHI WAKE NI BORA AACHWE ATAWALE KWA KIPINDI CHOTE CHA MAISHA YAKE AMBACHO ATAKIWA NA NGUVU YA KUSIMAMIA YALE MAMBO ANAYO 'DICTATE' KULIKO KUWA NA RAIS WA TERM MBILI ZA MIAKA MITANO MITANO AMBAYE MUDA WAKE WOTE ANAWAZA KUSAFIRI NA KWENDA KUJIRUSHA/KUFANYA SHOPPING ULAYA NA AMERICA
 
sina tatizo na maelezo yako lakini ningependa nikutaarifu miongoni mwa nchi zenye sera nzuri za afya kwa Afrika Mashariki na kati ni Tanzania, bahati mbaya sera hizi hazijafanyiwa kazi ipasavyo. Mfano wetu bora kabisa ni Community Health Fund (CHF) ambao ni mfuko wa afya ya jamii hasa hasa wilayani na vijijini ambapo sehemu nyingi wanatoza sh 5,000 na zingine sh 10,000 kwa mwaka kwa kaya ya watu 6 ambayo ni very cheap ukilinganisha na hizo dola 16 za kagame na rwanda yake. nina ushahidi wa kina kabisa kwamba zile halmashauri ambako mfuko huu umesimamiwa ipasavyo, wananchi wameweza kupata huduma bora za afya , mfano nenda wilaya za mkoa wa dodoma, nenda igunga, mwanga, handeni etc huku kote CHF imefanya vitu vizuri sana kwenye afya, ila tatizo ni usimamizi mbovu katika utoaji wa huduma za afya kwa ujumla wake nchini.

pia ukumbuke universal health insurance ni jambo gumu sana, kwani hata marekani ni mwaka juzi tu ndio obama ameleta ile bill ya kusaidia masikini kupata unafu wa huduma za afya, so kwa tanzania yetu yenye watu millioni 45 kulinganisha na rwanda yenye watu milioni 9.5 bado si sahihi sana

Mkuu inaonesha ulivyo analytical wa sera ya afya. Nimesikia misemo kama hii kutoka kwa wasomi na wasio wasomi: CCM kama chama siyo kibaya ila baadhi ya viongozi wake; sera za ccm ni nzuri ila utekelezaji wake; ...huku nikujifariji tu. Watunga sera watanzania ndo hao watekeleza sera, kama hawawezi kutekeleza walichotunga then something is wrong na hapotusitegemee maendeleo coyote.
 
Rais kagame amechukua vijana bright wanaotakiwa kuendelea na elimu ya juu na kuwaombea scholarship na wengine kuwalipia elimu ya juu kwenye vyuo maarufu marekani ili baadae waje kuitumikia nchi yao.
Kitendo alichofanya rais kagame pamoja na udikteta wake lakini kitaifanya rwanda kuwa nchi yenye maendeleo makubwa baada ya miaka 5 kuanzia sasa kwani watakuwa na wataalamu wa kila fani.
Wakati rwanda wanafanya hayo sisi tumeendelea kusaini mikataba ya madini na gesi wakati hatujajiandaa kwa kusomesha wataalamu wetu na pia tunasaini mikataba bila kuwa na sera yoyote ya uchimbaji madini na gesi.
Pia tumeshindwa kusomesha wataalamu wetu na badala yake viongozi wa serikali wametumia nafasi walizonazo kusomesha watoto wao na kuwapa nafasi kwenye nyazifa nzito kama bot,kwenye ubalozi na sehemu nyingine wameshindwa kuimarisha elimu na kugawa keki ya taifa kwa watanzania wote

Kinachotokea Rwanda ni matokeo ya mipango na sera bora ambazo hata hapa Tanzania imekuwa ni ndoto toka aondoke Mwalimu Nyerere. Zaidi tunachotofautiana na Rwanda ni Uongozi bora, wenye commitment, muono wa mbali, adilifu na ulio tayari kusimama kidete kutetea maslahi ya nchi na watu wake.

Tunaizungumzia Rwanda ambayo kwanza imeanza kujijenga mwaka 1994 tu, ni ndogo kwa eneo, haina ardhi ya kutosha wala rasilimali nyingi ikilinganishwa na nchi yetu.Rwanda imeweza kupaa katika elimu ime enroll almost watoto wote, ime install ICTs katika shule,rushwa na ufisadi ni mwiko, umaskini wa kipato umepungua sana, nyumba za nyasi kwa sasa ni historia, sekta ya usafiri wa anga na ardhi iko juu, utalii inakaribia kulifunika eneo la Afrika Mashariki, Usambazaji wa umeme umefikia asilimia karibu 70 sasa, sekta ya Afya wameshavuka kiwango cha malengo ya millenia (8-MDGs) nk.nk.

Sasa huwezi kamwe kuilinganisha Rwanda na Tanzania iliyojaa UFISADI WA KAGODA, MEREMETA, RADA,PANAFRICAN ENERGY, NDEGE YA RAIS, RICHMOND, Mikataba ya Kimangungo kwenye madini na sasa mafuta na gas na ubakaji mwingine mwingi wa Rasilimali watu na fedha. Sasa ufisadi huo ukichanganywa na Sera mbovu za CCM ndiyo jehanamu yetu tunayoishudia. Hakika maendeleo tutaendelea kuyasikia kwa wengine si kwa sababu hatuna uwezo kama ambavyo Makada wa CCM wamekuwa wakituaminisha lahasha bali kwa kuwa UFISADI UMEKUWA NDIYO MAISHA YETU NA HATUNA VIONGOZI WAADILIFU,WENYE VISHENI NA WALIO TAYARI KUPIGANIA MASLAHI YA NCHI NA WANANCHI WOTE.
 
Waheshimiwa sio kwamba amewapeleka ulaya tuu.... hapa UDSM amemwaga vijana kama 150 hvii kuanzia BA., M.A mapaka PhD courses aina mbali mbali. Pia naona Mozambique na Angola nao wameamua kumwaga vijana wao kibao. Nadhani na sisi ingebidi tuchukue mkondo huo kwa kuwapeleka huko china na US kama china wanavyowapeleka vijana wao US na UK. Imani yao no moja tuu: Acha waksome na kupata ujuzi kwani nyumbani ni nyumbani tuu..ipo siku watarudi home...
 
;

Mimi nionavyo kwanza nikupongeze kwa kufuatilia kinachojiri kwa nchi zinazotuzunguka (JIRANI) huo ndio ujirani mwema siku zote..., naomba tu kutofautiana na wewe eneo moja tu kwamba Kagame ni dikiteta, hayo ni mambo ya magazeti hajawahi kuwa dikiteta hata siku moja. Ni mtu anayependa vitu viende kwa kufuata cheria, kanuni na taratibu, amechaguliwa kidemocrasia wakati wote, kuna mahakama na kila akoseaye sheria inachukua mkondo wake, ameweza kufuta adhabu ya kifo, ni nchi peke yake Duniani yenye asilimia kubwa ya wabunge wanawake wengi . hapo udikiteta uko waapi.

Maendeleo Rwanda juwezi kulinganisha na nchi yoyote Africa hii.....!! ukiondoa South africa na Mauritius nafikiri, usafi, ruhwa zero torelance ngoja niache hapo kwa leo, na sisi tunahitaji kubadilika na kufuata nyayo.

global economic forum ktk report yao ya mwezi uliopita kama sijakosea walisema Rwanda ni mojawapo ya nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi sana hasa sekta ya fedha.
 
Naionea huruma Tanzania imepitia kwenye mikono ya majambazi ,walafi, mabinafsi sijui itakuaje
 
Viongozi wetu wamekuwa wakilizungumzia shirikisho la Afrika Mashariki kisiasa zaidi bila kujiandaa.Mara nyingi tumesikia kauli za viongozi wetu waskisema watanzania wajiandae kwa ajili ya soko la ajira la East Afrika lakini hawajafanya chochote kuandaa wananchi wao kulikabili hilo soko(hakuna mkakati wowote) tusishangae tukigeuka vibarua(hapa nazungumzia kama Taifa siyo mtu mmoja mmoja) kwani tutakaporuhusu soko la ajira(ingawa limesharuhusiwa) kisiri siri sidhani kama watanzania watapata nafasi kwenye nchi nyingine wenzetu kwa sababu wanaona mbali wanaweza kuwa wanasomesha wataalamu wa mambo ya gesi ingawa hawana gesi kwa kujua maadamu tanzania kuna gesi watu wetu watapata ajira nafikiri ni wakati muafaka tuwaelimishe watu wasichague viongozi wenye ubinafsi ingawa kiutekelezaji ni ngumu kufanyika.
 
Always, Kagame IS THE MAN to reckon with in Africa. Ma-Rais wote wezi wa mali za umma yapaswa tukawapeleka tuisheni kwa Mzee Kagame wakafundishwe visionary leadership clear of corruption at all levels of governance, no bla bla bla, no majungu, no fitina, no safari kibao ...

Nani kama Kagame...?????????????
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom