Hili la rais Kagame mnalionaje?

RAIS PAUL KAGAME WAKATI UMEFIKA NA KWAA HESHIMA ZOTE NA TAADHIMA TUNAKUOMBA UKACHUKUE FOMU YA KITI CHA URAIS WA AFRIKA MASHARIKI KUOKOA VIZAZI VINGI KATIKA ENEO HILI KUSALIMIKAA NA MADHARA YA UFISADI WA KIMFUMO KATIKA MATAIFA YETU HAYA

Kwa heshima zote na taadhima, namuomba Balozi wa Rwanda hapa nchini kwetu achukue fursa ya kumfikishia UJUMBE WA VIJANA WA KI-TANZANIA tulio wengi kwamba TUNAMUOMBA SANA aje kuchukua uongozi wa Afrika Masharika mara moja.

Ndio, vijana tuliowengi kwa pamoja tunasema kwamba huyu Rais Kgame akimaliza hatamu ya uongozi nchini mwake pamoja na hiyo LEGACY YA USOMI BORA anaoujengea taifa lake hivi sasa, wenzio TUNAMSIHI AKACHUKUE FOMU YA KUGOMBEA KITI CHA URAIS WA AFRIKA MASHARIKI na sisi tupo hapa tutatumia nguvu zetu zote na ushawishi wote kupita kote huko Uganda, Burundi, Kenya, Sudan Kusini pmoja na hapa nchini kuhakikisha kwamba anapata zaidi ya asilimia 85 % ya kura zote zitakazosajiliwa kupiga kura (hata kama mgombea atakua ni yeye peke yake) kushika nafasi hiyo muhimu.

Uwezo Tunao wa kujenga Bara la Afrika kuwa zaidi ya Ulaya au kwingineko ilmradi kuwepo na
POLITICAL WILL AND ZERO TOLERANCE FOR CORRUPTION, safari kibao Ughaibuni, na haka ka-tabia ka-kuibia uchumi wa nyumbani na kwenda kuficha ngambo ili fedha hizo bora kusaidia Ulaya kuliko nyumbani.

Balozi kamwambie Mhe Kagame kwamba hatumpendekezi ili kujipendekeza kwake kwa lolote lile, nasema wala hatumpendekezi kwa kuwa yeye pengine anayo miguu minne zaidi ya ma-rais wengine, ndio hatumpendekezi kwa kuwa pengine yeye alifanikiwa kuumbwa akiwa na pembe kama nyati porini la hasa; tunachovutiwa nacho kwake tena kwa viwango vya kupindukia ni hizo sifa hapo juu penye wino mzito wa blue.

We want Kagame NOW ND NOT TOMORROW kuja kuongoza eneo letu hili la ukanda wa Afrika Mashariki kwa kazi ya kuondoa rushwa na matawi yake yote, kutunyunyizia japo ka-dozi ka U-DICTATOR kidogo kama hiyo ndio siri ya kuendelea kwa taifa lake kwa kasi yote hii ya ajabu basi udikteta wake kumbe ni wa kuleta neema kuliko wengine ambao husifika kwa upole huku tukikombewa kila kitu hadi wanyama hai kwenda kwa wapendwao wao huko.

Baba Paulo Kagame, chonde karibu ukatutawale Afrika Mashariki sasa hivi na wala si kusubiri kesho!!!
 
Kagame na wanyarwanda wanavision, wanajua wanakwenda wapi so mambo kama haya ni ya kawaida kabisa. Sisi hatujui tunakokwenda sanasana tunasikiliza mziki wa wazungu na wanaojiita wawekezaji. Congrats wanyarwanda na rais wenu CEO Kagame
 
maskini nchi yangu ,maskini watanzania wenzangu ,elimu yetu haikidhi haja ,imevamiwa mitaala inabadilishwa kila wakati ,wizara husika hawajui au hawana vipaumbele nini kifanyike kuhusu elimu ,hebu angalia university graduates wa leo compare na enzi za mwalimu nyerere ,hebu tazama pale IFM wanafunzi wa kike wanaongoza kwa kujiuza ,elimu inakwenda wapi ,angalia kigamboni pale kuna chuo kipo pale fika saa za jioni .aibu tupu ,wakati umefika sasa kuangalia mfumo wa elimu tulionao unafaa ,sasa hivi tuko kwenye mfumo wa 7-4-2-3 .std 7 miaka 7 ,sec ,miaka 4 ,form five na six miaka 2 ,university 3
 
Rais Kagame amechukua vijana bright wanaotakiwa kuendelea na elimu ya juu na kuwaombea scholarship na wengine kuwalipia elimu ya juu kwenye vyuo maarufu marekani ili baadae waje kuitumikia nchi yao.

Kitendo alichofanya rais Kagame pamoja na udikteta wake lakini kitaifanya Rwanda kuwa nchi yenye maendeleo makubwa baada ya miaka 5 kuanzia sasa kwani watakuwa na wataalamu wa kila fani.

Wakati Rwanda wanafanya hayo sisi tumeendelea kusaini mikataba ya madini na gesi wakati hatujajiandaa kwa kusomesha wataalamu wetu na pia tunasaini mikataba bila kuwa na sera yoyote ya uchimbaji madini na gesi.

Pia tumeshindwa kusomesha wataalamu wetu na badala yake viongozi wa serikali wametumia nafasi walizonazo kusomesha watoto wao na kuwapa nafasi kwenye nyazifa nzito kama bot,kwenye ubalozi na sehemu nyingine wameshindwa kuimarisha elimu na kugawa keki ya taifa kwa watanzania wote
kama anafanya udikteta kwa maendeleo ya nchi hii ipo poa sisi hatuwezi kufanya hivyo kwa kuwa tunapenda matumbo yetu kuliko nchi yetu watawala wahawataki kuelimisha wananchi kwa kuofia kupokwa machaka yao
 
sina tatizo na maelezo yako lakini ningependa nikutaarifu miongoni mwa nchi zenye sera nzuri za afya kwa Afrika Mashariki na kati ni Tanzania, bahati mbaya sera hizi hazijafanyiwa kazi ipasavyo. Mfano wetu bora kabisa ni Community Health Fund (CHF) ambao ni mfuko wa afya ya jamii hasa hasa wilayani na vijijini ambapo sehemu nyingi wanatoza sh 5,000 na zingine sh 10,000 kwa mwaka kwa kaya ya watu 6 ambayo ni very cheap ukilinganisha na hizo dola 16 za kagame na rwanda yake. nina ushahidi wa kina kabisa kwamba zile halmashauri ambako mfuko huu umesimamiwa ipasavyo, wananchi wameweza kupata huduma bora za afya , mfano nenda wilaya za mkoa wa dodoma, nenda igunga, mwanga, handeni etc huku kote CHF imefanya vitu vizuri sana kwenye afya, ila tatizo ni usimamizi mbovu katika utoaji wa huduma za afya kwa ujumla wake nchini.

pia ukumbuke universal health insurance ni jambo gumu sana, kwani hata marekani ni mwaka juzi tu ndio obama ameleta ile bill ya kusaidia masikini kupata unafu wa huduma za afya, so kwa tanzania yetu yenye watu millioni 45 kulinganisha na rwanda yenye watu milioni 9.5 bado si sahihi sana



kwenye kijani, wewe unaonekana unaumia watu wanapompongeza anayefanya vyema.... umekuwa biased, sifa si nzuri kwenye constructive critisicm......

penye nyekundu, tatizo mara zote si uwepo wa sera, ni utekelezaji..ambao chini ya Mr Dhaifu hauna mbele wala nyuma....

usipokuwa makini utasema wewe BWANA MKUBWA huna matatizo....matatizo ni ya WALIOKUZUNGUKA..... kha walikaribiaje huo mzunguko?
 
watanzania wengi ni wajinga,mijini na vijijin wanaitaj elimu ya kujitambua,wanapata matatizo miaka 10 sababu ya kupewa kanga,kofia na kupakiwa kwenye malori,huu ujinga usipoondolewa kwenye akili zetu wadanganyika tutaumia sisi,wajukuu na vitukuu,tuamke sasa

Mjinga unamjua? We si mTZ? Usilalamike na kuita waTZ wajinga huku huna la kufanya. MJINGA ni watu kama wewe ambao wanlaalamika huku hawajui kuwa wao ni WAJINGA na aina yenu ni watu hatari mnaokatisha watu tamaa ya maendeleo kwa ulopokaji wa kijinga kama huu, na mbaya zaidi unaandika USHINDWE NA UJINGA WAKO
 
Mjinga unamjua? We si mTZ? Usilalamike na kuita waTZ wajinga huku huna la kufanya. MJINGA ni watu kama wewe ambao wanlaalamika huku hawajui kuwa wao ni WAJINGA na aina yenu ni watu hatari mnaokatisha watu tamaa ya maendeleo kwa ulopokaji wa kijinga kama huu, na mbaya zaidi unaandika USHINDWE NA UJINGA WAKO

watanzania awapendi kuambiwa ukweli,mimi nilikuwa mtanzania lakin sasa siyo mtanzania baada ya wazaz kubadili uraia
 
Sisi kaka tunaongoza kwa fani ya ushirikina na uchawi ujasikia kutoka CNN kaka
 
sina tatizo na maelezo yako lakini ningependa nikutaarifu miongoni mwa nchi zenye sera nzuri za afya kwa Afrika Mashariki na kati ni Tanzania, bahati mbaya sera hizi hazijafanyiwa kazi ipasavyo. Mfano wetu bora kabisa ni Community Health Fund (CHF) ambao ni mfuko wa afya ya jamii hasa hasa wilayani na vijijini ambapo sehemu nyingi wanatoza sh 5,000 na zingine sh 10,000 kwa mwaka kwa kaya ya watu 6 ambayo ni very cheap ukilinganisha na hizo dola 16 za kagame na rwanda yake. nina ushahidi wa kina kabisa kwamba zile halmashauri ambako mfuko huu umesimamiwa ipasavyo, wananchi wameweza kupata huduma bora za afya , mfano nenda wilaya za mkoa wa dodoma, nenda igunga, mwanga, handeni etc huku kote CHF imefanya vitu vizuri sana kwenye afya, ila tatizo ni usimamizi mbovu katika utoaji wa huduma za afya kwa ujumla wake nchini.

pia ukumbuke universal health insurance ni jambo gumu sana, kwani hata marekani ni mwaka juzi tu ndio obama ameleta ile bill ya kusaidia masikini kupata unafu wa huduma za afya, so kwa tanzania yetu yenye watu millioni 45 kulinganisha na rwanda yenye watu milioni 9.5 bado si sahihi sana


Mkuu, nimeupenda mchango wako, japo kuna maeneo ambayo nimeyawekea wekundu, nina wasiwasi kidogo.
Yawezekana TZ ikawa na sera nzuri za afya, lakini siku zote uzuri wa kitu hupimwa kwa matokeo yake. Hivyo kama zingetekelezeka kwa ufanisi ungekuwa na kiburi cha kuzisifia. Vinginevyo ni sifuri tu mkuu.

Mwishoni mwa mchango wako umejaribu kugusia kwa mlinganisho wa idadi ya watu katika nchi mbili hizo, Rwanda na TZ, lakini umesahau pia kulinganisha fursa dhahiri ya uchumi hususan katika raslimali za asili kati ya nchi mbili hizo.

Nadhani kwa vyovyote vile Tz imeipita kwa mbali sana Rwanda kwa uwiano wa fursa ya rasilimali za asili na idadi ya watu katika nchi hizo. Kwa mantiki hiyo Tz ilitakiwa kuwa mbali sana kiuchumi na maendeleo kuliko nchi yoyote katika Jumuia ya Afrika Mashariki kutokana na Raslimali lukuki ilizokuwa nazo.
 
Ni kwa sababu wamepata rais mwenye akili ya kufikiria. Ama sisi tumepata..[/QU

Rais Kagame wa Rwanda ni mtu makini kwasababu he spends some of his time reading the development history of other countries and by doing so he learns what they went through and adopts those techniques to his country's needs. Yeye sio kama Vasco Dagama wetu anakwenda kubembea na kupanda mikokoteni badala ya kwenda kutembelea vyuo vikuu kama mwenzie!! Haya anayofanya Kagame sio mageni bali ni hayo hayo aliyoyafanya Lee Kuan Yew kule Singapore na akaiwezesha ile nchi ndogo kuendelea kwa kiwango cha kutisha!! Huyu ****** wetu hata vitabu hanunui huko anakozurula ;yeye kazi yake kubwa kununua suti na kupiga picha na wasanii basi!! Wadanganyika kweli kazi tunayo!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom