Hiki ndicho chanzo cha ugonjwa wa mabusha

CTX

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
1,273
984

Ngiri nyingine ni ya Mshipa wa Kushuka ni hii hapa Mabusha kwa lugha ya kiswahilBusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu.

Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani. Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili.

Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili.

Kwa kawaida busha halina maumivu na wala kuleta madhara, isipokuwa kama litapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya wengi wa waathirika, kuwa wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba.

Hata hivyo, ni vyema kama mtu ana uvimbe wowote kwenye pumbu zake, kutafuta msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa mengine ya sehemu za siri kama vile saratani ya korodani (testicular cancer) n.k.

Busha husababishwa na nini? Sababu za kutokea kwa busha hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.

Kwa watoto wa kiume Kwa watoto wa kiume, busha huweza kuanza kutokea kipindi cha ujauzito.

Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye mapumbu.

Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalis hushuka sambamba na kurodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.

Kwa kawaida, ndani ya muda wa mwaka mmoja, kifuko hiki hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto.

Iwapo baada ya kifuko kufunga na maji yaliyomo kushindwa kufyonzwa kurudishwa kwenye tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo na mawasiliano (non-communicating hydrocele).

Hali kadhalika, wakati mwingine inawezekana kifuko kikashindwa kufunga na hivyo maji yakaendelea kujaa ndani ya kifuko kuzunguka korodani.

Aina hii ya busha kwa watoto ujulikana kama busha lenye mawasiliano (communicating hydrocele). Kwa wanaume watu wazima Kwa wanaume watu wazima.

Busha husababishwa na mambo makuu mawili:

1. kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida.

2. Kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system)

Ongezeko la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na

  • Maambukizi au/na majeraha katika korodani (testicular inflammation auorchitis)
  • Maambukizi katika mshipa ujulikanao kama epididymis yanayoweza kusababishwa na kifua kikuu (tuberculosis) cha makende,
  • Maambukizi yanayo sababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanao sababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.
  • Kujinyonga kwa korodani (testicular torsion) kunakoweza kuzifanya korodani kutenda kazi zaidi ya kiwango chake (hyperactive testis).
  • Uvimbe katika korodani (testicular tumors) ambao husababisha uzalishaji wa maji kupita kiasi.
  • Kupungua kwa ufyonzaji wa maji hutokana na Kufanyiwa upasuaji kipindi cha siku za nyuma katika eneo la kinena, au operesheni ya upandikizaji figo ambazo zinaweza kuathiri mfumo wa lymph na vena na hivyo kupunguza ufyonzaji wa maji kutoka kwenye mapumbu.
  • Kuwahi kufanyiwa tiba ya mionzi kipindi cha nyuma nayo uhusishwa na kutokea kwa busha.
  • Kwa hapa kwetu Tanzania, kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha na matende hususani maeneo ya Pwani na mwambao.

Dalili za busha Katika hatua za awali,

busha huwa halina dalili zozote (asymptomatic).

Hata hivyo, baada ya muda fulani, mapumbu hujaa na uvimbe huweza kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri uvimbe unavyozidi kuongezeka, ndivyo dalili zingine uzidi kuonekana.
 
uzi mzuri, elimu nzuri.. kwaku ongezea na fikiri kwa aslimia kubwa ya mabusha Tz ni hayo yanayo sababishwa na filarias worm. Na mahali watakapo shambulia ndipo ugonjwa utakapo tokea mfano wanaweza sababisha mabusha.. matende na aina na uvimbe kwa wanawake... pia NOTE: ngiri maji yaweza tokea sehemu nyingine za mwili siyo kwenye korodani tu.
prevention ya hao filarias worms kama wucherreria ni kumeza dawa za chanjo ambazo hutolewa kila mwaka kwani wadudu hawa huwa asymtomatic wana dwell ndani ya nyama mwaka mzima bila kuonekana mwisho wa siku una shangaa una matendee au mabusha au calabor swellng kwa wanawake( sina uwakika na uandshi vzr wa ilo jina) . Nakumbuka test yake ina fanyikaga saa 8 za usiku kukiwa na giza ww na mgonjwa..test pendwa hosptaln
 
Ahsante kwa somo zuri sana.

Je kuna uhusiano gani kati ya busha na miluzi au honi!?

Mara nyingi naona wenye ugonjwa huu wanafanyiwa dhihaka na wenyewe huwa wanakuwa km wanasikia maumivu.
 
Wengine wakijambishwa wanaruka kweli kweli
 
Maanangu ana seven yrs ila alikuwa nalo toka kuzaliwa korodani moja ikajirudi nyingine ikabakia....

Nilimpeleka Hindu mandal mwanza nikashauriwa kusubiri hadi afike 5 yrs lisiporudi sasa halikarudi na ana miaka 7 yani kila nikimwazia operation nachanganyikiwa.
 
Asante sana kwa somo zuri. Mwanangu pia ametoka shule na mke wangu kagundua kama ana uvimbe huo. ana miaka 15 sasa. Amepelekwa Hospitali, tumeambiwa kuna weza kufanyika upasuaji ndani ya wiki hii. nauliza tu. Je upasuaji wake hauna complication sana na hakuna dawa zaidi ya upasuaji?
 
Maanangu ana seven yrs ila alikuwa nalo toka kuzaliwa korodani moja ikajirudi nyingine ikabakia....

Nilimpeleka Hindu mandal mwanza nikashauriwa kusubiri hadi afike 5 yrs lisiporudi sasa halikarudi na ana miaka 7 yani kila nikimwazia operation nachanganyikiwa.
Pole kiongozi. Wataalam watusaidie kutoa elimu hii. Wazazi wengi hatuna elimu ya kutosha.
 
Habari mkuu.. Mwanangu amepasuliwa ni op. Ndogo sana.. Leo amarejea nyumbani...!! SIFA NA UTUKUFU NI KWA MUNGU ALIYE JUU
 
Back
Top Bottom