Hiki kitabu cha risiti cha huyu Trafiki, ni cha Serikali au chake binafsi?

MT255

JF-Expert Member
May 3, 2012
3,388
4,662
Natumaini ni wazima kabisa wanajamvi,

Leo katika pitapita yangu nikielekea kwenye mihangaiko yangu ya kujitafutia riziki, nilisimamishwa na Askari wa barabarani maeneo ya Argentina pale Manzese. Lakini baada ya kukagua gari langu aliniambia ananiandikia kwa kuwa sina kifaa cha kuzimia moto ambacho kimesajiliwa na zimamoto, nikamwonyesha kifaa anachosema sina lakini akaniambia kilichokuja na gari hakitakiwi..

Lakini cha kushangaza, Risiti hiyo niliyoandikiwa inasema hiyo risiti ni ya mwaka 2011 na kiasi nilicholipa kwa kosa ni 30,000/=...

Swali la kujiuliza, inawezekana kikosi cha usalama barabarani wakatumia kitabu cha risiti cha zamani ? Au ni zoezi lao la kuwaibia wananchi?

Nawasilisha!
 
Attachments

  • 1426623241594.jpg
    1426623241594.jpg
    94.8 KB · Views: 3,098
  • 1426623260017.jpg
    1426623260017.jpg
    81.4 KB · Views: 2,676
  • 1426623273564.jpg
    1426623273564.jpg
    84.9 KB · Views: 2,453
  • 1426623288569.jpg
    1426623288569.jpg
    66.2 KB · Views: 2,375
  • 1426623400526.jpg
    1426623400526.jpg
    99 KB · Views: 3,642
Sijaona mantiki ya wao kung'ang'ania fire extinguisher wanazozitaka wao. Muhimu ni ufanisi wa hiyo Mitungi (uzima na tarehe ya matumizi)..

Tukija kwenye risiti.. kwa nikivyotazama mimi haraka haraka, kwa kurejelea hiyo lugha ya wazungu... hapo wamenukuu kifungu cha sheria kilichotoka mwaka 2011 tarehe 26 mwezi agosti...

OTHERWISE NAMI NIWE SIJAELEWA
 
Ukilipia unatakiwa upewe ERV sasa sijui kama umepewa. Halafu hoja ya kitabu kuwa cha mwaka 2011 haina mantiki kwani wanaweza kuomba vitabu toka mikoa ambayo ina stock kubwa na haina makosa sana wakapewa na kutumika.
 
hahahah kweli ww ni mburula aiseee wacha upigwe umekubali kabisa kuripa pesa kwa risit ya mwaka 2011!?

hahaha pole sana aiseee
 
Ee ndo muwekege mitungi mikubwa sio hvo vichupa vya dawa ya umbu kheh! mwenzio Nina litengi la zima moto kwenye buti akidai tu namwambia cheki muzigo huo anabloo mapigo utasikia,nenda.
Aftaro hilo litingisha ni kwa faida yako sio ya tulafiki!:(
 
Hili suala la mapolisi kung'ang'ania fire extinguisher ni ujinga wetu wa Kiafrika na ujinga wa wabunge wetu kulikubali. Tunalipia 30,000 mpaka 40,000 kila mwaka, inabidi watembee na fire extinguisher watupe bure kila gari iliyokuwa haina na imelipia motr vehicle licence.

Zile pesa za kila mwaka tunalipia za nini?

Hivi hii mikanjanja inayojiita miandishi ya habari kazi zao ni nini ikiwa wanashindwa kupigia kelele mambo kama haya ambayo yanawagusa wengi?

Wao kazi yao kuandika udaku tu?

CC Makanjanja wote wanaopitia JF including Pasco na Manyerere Jackton
 
Halafu wewe jamaa si ndio nimekukamata pale Argentina Asubuhi? sasa ni hivi fuata risiti yako kesho kuanzia saa 6 pale ofisi ya Mhasibu MAGOMENI hiyo ni hela ya UMMA si ya ASKARI (Utapewa Risiti ya rangi ya NJANO ikiwa imeandikwa jina lako kamili)
 
Sasa mukuu huko kwenye boneti gari ikiwaka ghafla utalipata limutungi on time kweli?
 
Hili suala la mapolisi kung'ang'ania fire extinguisher ni ujinga wetu wa Kiafrika na ujinga wa wabunge wetu kulikubali. Tunalipia 30,000 mpaka 40,000 kila mwaka, inabidi watembee na fire extinguisher watupe bure kila gari iliyokuwa haina na imelipia motr vehicle licence.

Zile pesa za kila mwaka tunalipia za nini?

Hivi hii mikanjanja inayojiita miansihi ya habari kazi zao ni nini ikiwa wanashindwa kupigia kelele mambo kama haya ambayo yanawagusa wengi?

Wao kazi yao kuandika udaku tu?

CC Makanjanja wote wanaopitia JF including Pasco na Manyerere Jackton
Acha kuhohoroja hapa wewe ajuza FaizaFoxy, wewe utakuwa ni 'macho woman' ambapo sometimes ukiwashwa, unataka uridhishwe kwa kufanyiwa 'masochism' ndio maana sometimes unakuja 'as an agent provocateur' ili utukanwe, ndipo upate ... utafute kuridhishwa, ambako ndio 's.. gratification!" yako!, wewe unamjua fika kuwa , Manyerere Jackton, sio tuu ni mwanahabari makini, bali pia ni mzalendo wa kweli na kamanda mpigaji, ambae pia ni mmiliki wa gazeti la Jamhuri, huwezi kutuita "hii mikanjanja inayojiita miansihi ya habari" najua lengo lako ni kutu provoke ili tuu, tukutukane!, kwa mimi nimeligundui hili, hatukutukani na sana sana tunakuongezea heshima,

Shkamu Bibi Faiza!.

Pasco
 
Pasco sasa hivi yuko na Zitto. Ishu hizo zitengee bajeti yake muelewane aje hapa kuvurumisha mauongo yake
 
Last edited by a moderator:
Hili suala la mapolisi kung'ang'ania fire extinguisher ni ujinga wetu wa Kiafrika na ujinga wa wabunge wetu kulikubali. Tunalipia 30,000 mpaka 40,000 kila mwaka, inabidi watembee na fire extinguisher watupe bure kila gari iliyokuwa haina na imelipia motr vehicle licence.

Zile pesa za kila mwaka tunalipia za nini?

Hivi hii mikanjanja inayojiita miansihi ya habari kazi zao ni nini ikiwa wanashindwa kupigia kelele mambo kama haya ambayo yanawagusa wengi?

Wao kazi yao kuandika udaku tu?

CC Makanjanja wote wanaopitia JF including Pasco na Manyerere Jackton

Mbona umeandika kwa hasira sana?
BTW, zoezi la ukaguzi na fine za fire extinguisher ni kazi na zinaingizwa kwenye kasma ya kikosi cha zimamoto. Si kazi ya jeshi la polisi...huu ndiyo uelewa wangu.
 
Last edited by a moderator:
Mbona umeandika kwa hasira sana?
BTW, zoezi la ukaguzi na fine za fire extinguisher ni kazi na zinaingizwa kwenye kasma ya kikosi cha zimamoto. Si kazi ya jeshi la polisi...huu ndiyo uelewa wangu.
Hajaandika kwa hasira bali amejifanya ana hasira ili atukanwe!.

Kuna type fulani ya wanawake wanaitwa 'macho women' hawa ili kupata 's..gratification' wanahitaji kuwa abused, kubakwa, au kutukanwa!, sasa siku wanapohitaji, wanajikuta wanatafuta watu na kuwa provoke ili hao watu wawatukane, wao wawe gratified!.

Dawa yao sio kuwatukana kwa sababu watapata walichotaka bali kuwa mwagia heshima!, mimi pale nimemwaga shikamoo!.

Pasco
 
Acha kuhohoroja hapa wewe ajuza FaizaFoxy, wewe utakuwa ni 'macho woman' ambapo sometimes ukiwashwa, unataka uridhishwe kwa kufanyiwa 'masochism' ndio maana sometimes unakuja 'as an agent provocateur' ili utukanwe, ndipo upate ... utafute kuridhishwa, ambako ndio 's.. gratification!" yako!, wewe unamjua fika kuwa , Manyerere Jackton, sio tuu ni mwanahabari makini, bali pia ni mzalendo wa kweli na kamanda mpigaji, ambae pia ni mmiliki wa gazeti la Jamhuri, huwezi kutuita "hii mikanjanja inayojiita miansihi ya habari" najua lengo lako ni kutu provoke ili tuu, tukutukane!, kwa mimi nimeligundui hili, hatukutukani na sana sana tunakuongezea heshima,

Shkamu Bibi Faiza!.

Pasco

Jibu hoja wewe achana na mimi. Wewe lini uliandika kwa maslahi ya wananchi?

Kuwa na gazeti ndiyo kuwa mwandishi mzuri? hata Rostam ana gazeti ni lini uliona article yake? hata Mengi ana magazeti ni lini uliona article zake zaidi ya anazoandikiwa? Iddi Simba hali kadhalika.
Manyerere Jackton na Pasco ni makanjanja wa karibu ambao nnaweza kuwafikishia ujumbe kwa haraka kupitia JF.

Ikiwa imekuuma ujuwe imekuingia.

Ngoja tuone kanjanja mwenzio Manyerere Jackton na yeye atajibu nini.
 
Last edited by a moderator:
Mbona umeandika kwa hasira sana?
BTW, zoezi la ukaguzi na fine za fire extinguisher ni kazi na zinaingizwa kwenye kasma ya kikosi cha zimamoto. Si kazi ya jeshi la polisi...huu ndiyo uelewa wangu.

Subiri tuone makanjanja yatajibu nini, au na wewe ni mmoja wao?

Umemsoma mleta mada? kama ulichosoma hukukielewa basi hata picha huoni? Kama si kazi yao kwanini wakaguwe na kuwalamba watu faini kwa ajili ya mitungi ya fire extinguisher?

Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
 
Jibu hoja wewe achana na mimi. Wewe lini uliandika kwa maslahi ya wananchi?

Kuwa na gazeti ndiyo kuwa mwandishi mzuri? hata Rostam ana gazeti ni lini uliona article yake? hata Mengi ana magazeti ni lini uliona article zake zaidi ya anazoandikiwa? Iddi Simba hali kadhalika.
Manyerere Jackton na Pasco ni makanjanja wa karibu ambao nnaweza kuwafikishia ujumbe kwa haraka kupitia JF.

Ikiwa imekuuma ujuwe imekuingia.

Ngoja tuone kanjanja mwenzio Manyerere Jackton na yeye atajibu nini.
Shkam Da Faiza, Shkam Mamdogo Faiza, Shkam, Bibi Faiza, heshima mbele sana!.

Mdogo wako, mwanao na mjukuu wako!.

Pasco
 
Back
Top Bottom