Hii Serikali inayosifiwa kwenye mabango nchi nzima nini hasa dhumuni lake?

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
999
2,056
"Siku mkisikia wazungu wananisifu tambueni nimewasaliti" ni maneno ya Samora Machel kwa wananchi wake. Tuje hapa kwetu sasa. Hii serikali inayosifiwa kwenye mabango nchi nzima Nini hasa dhumuni lake?. Kwanini imekimbilia kwenye mabango kujitangaza na si kuacha kazi ijitangaze yenyewe?

Ukweli ni kwamba wale wanaopiga pesa za umma wamegundua njia nyepesi ya kumteka akili huyu ni kumwagia sifa kama ilivyo hulka ya wanawake wengi kupenda kusifiwa huku wakinaswa kirahisi.

Mabango haya hayawekwi Bure ni pesa. Huku zahanati haina dawa, shule haina madawati na maji hakuna kwenye Kijiji cha Songambele. Hivi inakuwaje kiongozi unakubali upuuzi huu kama wewe si dhaifu kuliko hata udhaifu wenyewe. Tazama, wananchi hatuelewi kama hii Serikali inasimamia Nini hasa. Tumekata tamaa na kuomba 2025 ifike haraka tuchague wengine wenye nia ya dhati ya kujenga nchi.

Ni Rais Gani katika awamu zilizopita aliwahi fanya huu ujinga? Mabango? Mbaya zaidi hata hadhi ya Urais imetekwa nyara sasa imekuwa ni mama anatimiza na si Rais anatimiza! Hivi nchi yetu inaongozwa na mama au na Rais?
Kama unataka kuitwa mama nenda kahudumie familia yako na mme wako nchi mwachie Rais .
Unafanya vitu vyepesi lakini mabango nchi nzima. Vipi Marais walio leta uhuru, waliojenga viwanda,waliojenga SGR na bwawa kubwa la umeme nao wangeweka mabango nchi nzima ingekuwa vipi? Big brain hawezi hangaika na mabango anajua kazi ndiyo itamtambulisha. N sisi tunataka kazi na si mabango .

Hovyo kabisa
 
Nakuunga mkono 💯 Mafisadi yanakwiba yakiungana na mabeberu ya kimataifa kutupiga huku wakinyamazisha bi mkubwa kwa mabango ya sifa! Hivi ni jambo gani lenye mashiko analoweza kujisifia kafanya?
 
Waswahili wana msemo, "Zimwi likujualo, halikuli likakumaliza".
MajiIzi yanauma na kupuliza.
 
"Siku mkisikia wazungu wananisifu tambueni nimewasaliti" ni maneno ya Samora Machel kwa wananchi wake. Tuje hapa kwetu sasa. Hii serikali inayosifiwa kwenye mabango nchi nzima Nini hasa dhumuni lake?. Kwanini imekimbilia kwenye mabango kujitangaza na si kuacha kazi ijitangaze yenyewe?

Ukweli ni kwamba wale wanaopiga pesa za umma wamegundua njia nyepesi ya kumteka akili huyu ni kumwagia sifa kama ilivyo hulka ya wanawake wengi kupenda kusifiwa huku wakinaswa kirahisi.

Mabango haya hayawekwi Bure ni pesa. Huku zahanati haina dawa, shule haina madawati na maji hakuna kwenye Kijiji cha Songambele. Hivi inakuwaje kiongozi unakubali upuuzi huu kama wewe si dhaifu kuliko hata udhaifu wenyewe. Tazama, wananchi hatuelewi kama hii Serikali inasimamia Nini hasa. Tumekata tamaa na kuomba 2025 ifike haraka tuchague wengine wenye nia ya dhati ya kujenga nchi.

Ni Rais Gani katika awamu zilizopita aliwahi fanya huu ujinga? Mabango? Mbaya zaidi hata hadhi ya Urais imetekwa nyara sasa imekuwa ni mama anatimiza na si Rais anatimiza! Hivi nchi yetu inaongozwa na mama au na Rais?

Hovyo kabisa
Ni kwasababu tu ya kuwaeleza, kuwajulisha na kuwafahamisha wananchi wote wanao penda na wasio penda kwa pamoja kwamba,.....

mambo yanafanyika bayana mchana kweupe hadharani ili waTanzania wote kwa pamoja wafahamu na kuelewa matunda ya maendeleo wanayofurahia ni mipango madhubuti sana ya serikali sikivu ya CCM chini ya mwanamana shupavu sana, comrade Dr Samia Suluhu Hassan 🐒
 
Back
Top Bottom