Hii ni watoa lifti wote

MDANGANYIKAJI

Member
Jan 27, 2011
77
59
Jamani kwa wenzangu na mimi wenye magari please be alerted that kuna utapeli mpya umeibuka jijini. Ni kisa cha kweli kwamba kuna jamaa alitoa lifti kwa askari wakapiga stori fresh na jamaa akafunguka anapoelekea, then akaomba kushuka mita chache mbele, suprisingly enough baada ya yule askari kushuka jamaa akaendelea kuendesha na baada kama ya mita chache akasimamishwa na askari mwingine wakiomba kukagua gari. being confident na kutokujua whats going on hakuofu akamruhusu ila cha ajabu yule askari akaibuka na mfuko wenye unga mweupe na akamtuhumu kwamba ile ni unga na walikuwa wanamsuspect mda so its either atoe one million or waende kituoni; so kwa kiwewe alikubali kutoa hiyo hela though hakukujua yale madawa yametokea wapi.

the only thing he suspect ni kwamba yule askari wa mwanzo alimwekea; kwa hiyo wanandugu tuweni makini mimi tangia nipewe hiyo story sijawahi tena kutoa lifti esp kwa hawa wanafunzi na maaskari wanaoomba lifti.
 
Hao uliowapa lifti hawakuwa askari ni matapeli kama walivyo wengine, askari wanaoheshimu kazi zao wapo. Cha kufanya askari akikuomba lifti kariri '"orce number yake" utaujua ukweli.
 
Uhuni huu Askari Polisi walikuwa wanafanya miaka ya 80's.

Askari anakukamata kisha anakusachi mfukoni kumbe katika kucha zake ameweka Bangi hivyo anaiweka mfukoni mwako kisha anaitoa na kusema amekukuta na Bangi.

Wahuni sana hawa siyo wa kuwaamini 100%.

Hata Lift wasipewe kwani wanaharibu uaminifu kabida. Watimulie vumbi na matope tu.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Khaa, mboana mie natoaga sana lifti kwa askari na wanafunzi. Coz ndo nawaona kidogo ni ngumu kunitapeli. Juzi kati nilitoa lift kwa askari magereza kumbe mmoja wa wale askari nilisoma nae msingi enzi hizo za miaka ya tisini. Nilifurahi sana, nikamtembelea kwake akaja kwangu. Nawaaminia hawa watu. Sasa kama nao wanakua hivyo baasi tinted ndo suluhishi. Tena ile ambayo huoni nnje na wewe hakuoni.

Leo mapema asubuhi kuna mkaka nilimnyima lift kwa kuogopa mambo kama hayo. Ilikua saa tisa alfajiri. Jamaa kavalia tu poa. Lakini alfajiri ile nkasema chochote chaweza tokea. I felt guilty kumpita jamaa lakini hamna jisni
 
Hao uliowapa lifti hawakuwa askari ni matapeli kama walivyo wengine, askari wanaoheshimu kazi zao wapo. Cha kufanya askari akikuomba lifti kariri '"orce number yake" utaujua ukweli.
Nakubaliana na wewe mkuu
 
Na wewe 999 ulitoka wapi alfajiri yote hiyo?
Khaa, mboana mie natoaga sana lifti kwa askari na wanafunzi. Coz ndo nawaona kidogo ni ngumu kunitapeli. Juzi kati nilitoa lift kwa askari magereza kumbe mmoja wa wale askari nilisoma nae msingi enzi hizo za miaka ya tisini. Nilifurahi sana, nikamtembelea kwake akaja kwangu. Nawaaminia hawa watu. Sasa kama nao wanakua hivyo baasi tinted ndo suluhishi. Tena ile ambayo huoni nnje na wewe hakuoni.

Leo mapema asubuhi kuna mkaka nilimnyima lift kwa kuogopa mambo kama hayo. Ilikua saa tisa alfajiri. Jamaa kavalia tu poa. Lakini alfajiri ile nkasema chochote chaweza tokea. I felt guilty kumpita jamaa lakini hamna jisni
 
Kuna hawa walioko hapa Mbezi kwa Yusuph hawa sio maaskari bali ni vibaka ....................... wizi na mitungo ya kila aina hapo ndo kwao jamani kuweni makini naooo!!!!!!!!!
 
kweli siku izi hali si nzuri kabisa,utoe lifti kwa watu unaowafahamu tu jirani nk
kuna wengine wadokozi km umeweka vitu vyako basi ujue vinaenda usipocheki
 
Mimi yalinikuta, kuna watu wa mtaani kwetu ambao sikuwa nawafahamu sana zaidi ya ukazi wa mtaa mmoja tu waliniomba lift. Kwa kuwa huwa niko peke yangu au na wife tu nilizoea kuweka simu sehemu yoyote ndani ya gari hata siti ya nyuma. Siku nimewachukua nikajisahu kuiondoa,baada ya kushuka nilipotaka kupiga simu ndipo nilipogundua simu yangu haikuwepo sehemu yake.

Siku ya pili nilipowauliza waliapa kwa miungu yote kwamba hawajui chochote, nikamwachia Mungu.
 
Ndo maana sitoi wala kupokea lifti kwa mtu yoyote, jirani nitamsaidia hata
kumoeleka hospitali pale atakapokuwa hajiwezi, lakini mambi ya kuoakiana asubuhi au jioni daily siyataki, binadamu hawaaminiki siku hizi, unamsaidia mtu kwa roho njema kumbe anachonga mchezo akuumize.....

Back
Top Bottom