Hii ni Neema kwa Wanafunzi wote vyuo vikuu! Msipuuzie!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Sitaki kulisemea hili kisiasa lakini ukweli ndio huu hapa!

Tunatakiwa kuchagua urais atakayefanya Wanafunzi wote wasome vyuo vikuu bila hofu,wasome kama vile Tanzania ni nchi yao, wasisoneneke! Wafurahie fsida ya rasirimali zao,Wasomeshwe kama ni bure basi wapate fursa wote!

Tusifanye makosa tuliyoyajutia huko nyuma, tumepigwa mabomu,watu wamevunjwa miguu,watu wamewekwa ndani bila sababu, Viongozi wa bodi ya mikopo wanaifanya bodi kama Mali yao,hawana majibu mazuri kwa Wanafunzi, TCU hawana lugha nzuri, NACTE hawatoi majibu mtu unapokua na Shida, ukimkuta mtu ofisini anakujibu huvyo utafikiri umeenda nyumbani kwake hata kama ni secretary.

Nina imani ya nyuma yametufanya tujifunze na tujutie, tunasubiria tugome ndipo pesa zitolewe hazina! Hii inaumiza sana! Kama kuna kiongozi anayetaka kutoa elimu ya chuo kikuu bure, kwanini tusimpe kura ili baadaye tumdai?

Kwani pesa za kugharamia masomo ya Wanafunzi wote Tanzania ni kiasi gani,kwani hata pale bandarini zinakusanyawa sh. ngapi japo kwa mwezi tu? Kwani ESCROW zililambwa kiasi gani? Huenda huyu anayetaka kutoa elimu bure kwa Wanafunzi wote anajua pesa atasanya wapi.

Shime Wanafunzi msisubirie mabomu tena fanyeni maamuzi ya kweli, safiri hata hapo ulipo nenda ulikojiandikisha kapige kura yako tarehe 25/10/2015 kura yako moja ni muhimu kwa maisha yako na ya kizazi kijacho.
 
Mkuu umepewa fungu nn...?

Mkuu naapa Mbele ya Mungu wangu! Siwezi pewa kitu na haitatokea, Ila suala la elimu bure ni faraja sana kwetu sisi vijana wa Tanzania!CCM wamegoma kutoa elimu bure bora LOWASSA atufanyie mambo mema.
 
Mkuu naapa Mbele ya Mungu wangu! Siwezi pewa kitu na haitatokea, Ila suala la elimu bure ni faraja sana kwetu sisi vijana wa Tanzania!CCM wamegoma kutoa elimu bure bora LOWASSA atufanyie mambo mema.

Amka kijana. Unapigwa changa la macho. Hakunaga chuo kikuu bure duniani hata kama ingekuwaje. Hiyo hela ya kulipia chuo kikuu atatoa wapi? Usifanye mzaha wewe. Tatizo la vijqna wa Tanzania ni wepesi wa ku twistiwa. Pole sana. Hilo halitakuwepo.
 
kwa wale wasioamini elimu bure embu tuooredheshe pesa ambazo serikali ya ccm imepiga
-escrow
-Richmond
-epa
-kigoda
-green
-meremeta
mwenye kumbukumbu atujazie kiwango hapo,ni pesa iliyopotea nzimaaaaaa
acha sasa mikataba hii ya kichina na migodi

Bro chuo kikuu kuwa bure unataka tuwe km primary utakubali kufagia ww, kudeki darasa, nk

Au serikali unadhani itawalipa makampuni ya kufanya usafi vyuoni

Chukua akili zako changanya n zakuambiwa
 
Amka kijana. Unapigwa changa la macho. Hakunaga chuo kikuu bure duniani hata kama ingekuwaje. Hiyo hela ya kulipia chuo kikuu atatoa wapi? Usifanye mzaha wewe. Tatizo la vijqna wa Tanzania ni wepesi wa ku twistiwa. Pole sana. Hilo halitakuwepo.

Hiyo nikudanganya watanzania unaposema hakunaga chuo kikuu bure ebu fanya utafiti katika hizo nchi mnazoziita za kibepari kama kuna kijana yeyote wenye uwezo wa kuendelea na elimu ya juu ameshindwa kutokana na umasikini wa mzazi wake kama ameachwa mtaani mf. marekani elimu bure kuanzia chekechea mpaka kwa wenye uwezo wa kufika chuo kikuu kwa raia wake.Mzazi kama uwezo wa kuchangia sawa kama una uwezo kijana atasoma.
 
Bro chuo kikuu kuwa bure unataka tuwe km primary utakubali kufagia ww, kudeki darasa, nk

Au serikali unadhani itawalipa makampuni ya kufanya usafi vyuoni

Chukua akili zako changanya n zakuambiwa

Tatizo ni akili yako sio bure! Hao wanaofagia sasa hivi wanalipwa na Nani kama sio hizo hela za bodi kupitia ada? Kwa mwaka piga hesabu wanadahiliwa Wanafunzi kiasi gani? Jumla ya pesa za kulipia Wanafunzi wote kwa mwaka ni kiasi gani? Unafikiri hizo pesa zote serikalini hazipo?Jiulize mwenye kikao cha mwezi mmoja bungeni zinatafunwa sh.ngapi? Funguka akili yako kijana usishikwe.
 
Kwani kufagia au kudeki kunatatizo gani?mbona wewa nyumbani huwa unadeki na kufagia?sasa chagua kulipa ada au kudeki kipi ni chepesi na kinawezekana bila kwaa yeyote yule ambaye ni mtoto wa maskini!
 
Hiyo nikudanganya watanzania unaposema hakunaga chuo kikuu bure ebu fanya utafiti katika hizo nchi mnazoziita za kibepari kama kuna kijana yeyote wenye uwezo wa kuendelea na elimu ya juu ameshindwa kutokana na umasikini wa mzazi wake kama ameachwa mtaani mf. marekani elimu bure kuanzia chekechea mpaka kwa wenye uwezo wa kufika chuo kikuu kwa raia wake.Mzazi kama uwezo wa kuchangia sawa kama una uwezo kijana atasoma.
Nani amekuambia marekani chuo kikuu bure?there is no free lunch,hata watoto wa maskini wanapewa mkopo na wakianza kazi tu wanaanza kukatwa,watoto wa matajiri wao wanajilipia wenyewe
 
Nani amekuambia marekani chuo kikuu bure?there is no free lunch,hata watoto wa maskini wanapewa mkopo na wakianza kazi tu wanaanza kukatwa,watoto wa matajiri wao wanajilipia wenyewe

Soma post yangu uwelewe siyo unakurupuka muhimu ni wanafunzi wapate elimu ya juu iwe kwa mkopo au bure asiwepo mtu anauwezo wakusoma harafu anakaa kijiweni kwa kukosa ada.sasa hivi tunaosoma vyuo vikuu 90%hatuna hata hiyo mnayoita mikopo wapo wengine wamefahuru vizuri form six wazazi wao hawana uwezo wapo nyumbani.
 
Bro chuo kikuu kuwa bure unataka tuwe km primary utakubali kufagia ww, kudeki darasa, nk

Au serikali unadhani itawalipa makampuni ya kufanya usafi vyuoni
Chukua akili zako changanya n zakuambiwa

Ngoja tukusaidie kufikiri maana khali yako haikuruhusu kufikiri.
Ni hivi: unapoambiwa elimu bure ni kwamba hiyo gharama sasa inabebwa na serikali. Ada yako italipwa na serikali na sio wewe ama mzazi wako. Kwa hiyo mambo yote yataendelea kama kawaida isipokuwa serikali itaipa elimu kipaumbele yaani katika matumizi, elimu itapewa fungu kamili la kutosha gharama zote za uendeshaji bila kuhitaji cost sharing kama iliyopo sasa.

Siku zote kumbuka hili; kupanga ni kuchagua! Hakuna tusichoweza, tukiamua.

Unanikumbusha kuku aliefungwa miguu muda mrefu anavyokuwa. Ukimfungua anakuwa akilini hakubali kama anaweza akatembea kwa uhuru wote kwa hiyo anabaki ameduwaa....tafakari, chukua hatua
 
Huu upuuz ulitakiwa uwe jukwaa la siasa na si hapa.

Mpuuzi ni wewe usiyefahamu kinachojadiliwa humu unaugulia mihemko ya kishabiki tu!Hii mada ungeisoma kuanzia mwanzo hadi mwisho usingeleta upuuzi wako humu.
 
Back
Top Bottom