Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;

  • Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
  • Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu "3" kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
  • Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
  • Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
  • Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa –Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
  • Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
  • Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe.
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika "thesis" iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)

=====

UPDATE: Jan 6, 2016

Historia ma Elimu

1594971240946.png

Nape Nnauye ni waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano, ameteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi.
Hivi sasa Nape ana miaka 39, alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu.

Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.
Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara. Mzee Nnauye ni mmoja kati ya wanasiasa mashuhuri wa kizazi kinachoondoka, kazi yake ya kwanza ilikuwa ni “ukuli” wa bandari ya Lindi na Mtwara. Baadaye alisoma kidogo na kushiriki kwenye harakati za kudai uhuru akiwa kijana mdogo na baada ya Uhuru alikuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Tanu.

Ukiachilia mbali kulitumikia jeshi kuanzia “ukuruta” hadi kuwa Brigedia Jenerali, kuongoza vita ya Uganda kama mwanajeshi , lakini pia kama waziri mdogo wa Ulinzi, pia Nauye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, mkuu wa mkoa wa Singida, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Naibu Waziri wa Ulinzi na Mshauri wa Rais Mkapa.

Ndani ya CCM kwenyewe baba yake Nape amewahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya kwanza, Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya Taifa na Naibu Katibu Mkuu wa Tanzania bara.

Nape alianza elimu ya msingi huko mkoani Singida mwaka 1987-1989 katika shule ya Mwanga iliyopo wilaya ya Iramba (darasa la kwanza hadi la tatu). Alihamia mkoani Mwanza na kuendelea na elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Bukumbi iliyoko wilaya ya Misungwi kati ya mwaka 1989 hadi 1993 alipohitimu darasa la saba. Nape ni kati ya wanafunzi watatu waliofanya vizuri kwenye shule hii, alichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari.

Kati ya mwaka 1994 hadi 1997 Nape alisoma na kuhitimu kidato cha nne katika shule mbili za sekondari. Alisoma kidato cha kwanza na cha pili mwaka 1994 - 1995 katika shule ya Sekondari ya kutwa ya Ngudu iliyoko wilayani Kwimba na baadaye akamalizia kidato cha pili na kuendelea na kidato cha tatu na nne kati ya mwaka 1995 hadi 1997 katika shule ya Bweni ya Sekondari ya Nsumba iliyoko Mwanza ambako alihitimu elimu ya Sekondari.

Nape aliendelea na elimu ya juu ya sekondari kwa kujiunga na mchepuo wa EGM (Uchumi, Jiografia na Hesabu) katika Chuo cha Ualimu Butimba, alisoma kuanzia mwaka 1998 na kuhitimu mwaka 2000.

Kati ya mwaka 2000 hadi 2002 alianza elimu ya juu kwa kusoma Stashahada ya Sayansi ya Jamii katika Chuo cha Sayansi ya Jamii Kivukoni, alihitimu na kutunukiwa stashahada hiyo mwaka 2002 akibobea katika masuala ya Sosholojia, Fiziolojia na Siasa.

Nape alijipanga na kusoma stashahada ya pili mwaka 2002, hii ni ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa kutoka Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam ambayo aliihitimu na kutunukiwa stashahada mwaka 2003. Baadaye mwaka 2005 alikwenda nchini India kujiendeleza zaidi kimasomo, akafanikiwa kusoma na Shahada ya Saikolojia, Lugha na Habari – alihitimu na kutunukiwa shahada hii mwaka 2008 na Chuo Kikuu cha Bangalore.

Safari yake katika elimu haikukoma hapo, mwaka 2009 alianza kupanda ngazi za ubobezi wa juu zaidi. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam na kuanza masomo ya Shahada ya Umahiri ya Usimamizi wa Umma (Public Administration), mwaka 2010 alitunukiwa shahada hiyo. Nape amemuoa Rhobi, ana watoto wawili, Jaydan na Jayson.

Uzoefu
Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.

Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.

Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.

Nape akapambana na kushinda kura ya maoni ndani ya chama chake kwa kupata kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Mathew (mchezaji wa zamani wa Yanga) aliyepata kura 4,766 (baada ya kushindwa Selemani alihamia Chadema na kugombea kwa tiketi ya chama hicho). Kura za jumla zilizopigwa Oktoba 25 zilimtangazia Nape ushindi wa jumla wa kura 28,110, Mathew wa Chadema akatokea wa pili kwa kupata kura 13,918 huku mgombea wa CUF akishikilia nafasi ya tatu. Safari yake imekwenda mbele zaidi baada ya Rais JPM kumteua na kumkabidhi Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.

Nguvu
Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.

Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.

Udhaifu
Nape amekaa na kuongoza kitengo cha Habari na Uenezi cha CCM ngazi ya taifa kwa miaka kadhaa katika kipindi ambacho CCM imepita kwenye wakati mgumu kisiasa. Kitengo alichokiongoza kitaalamu na ndani ya vyama hujulikana kama “kitengo cha propaganda” hata kama wahusika hawawezi kupenda jina hili. Kuongoza kwake kitengo hiki kumemfanya awe mtu wa ‘Propaganda’ ki-kweli kweli na watu wengi niloongea nao wanadhani na kuamini kuwa amewekwa katika wizara hii ili aendeleze propaganda. Lakini wengi wetu wanafahamu kuwa wizara ya habari katika nchi kazi yake siyo propaganda tena, ni kushughulika na kero za wasanii, wanamichezo, wanahabari na hata ustawi wa jamii kimichezo na kiutamaduni. Lakini ikiwa wasiwasi wa wadau uko sahihi na kwamba Nape atajaribu kutumia wizara hii kama sehemu ya kuiimarisha CCM ki-propaganda, naamini jambo hilo litamuangusha.

Matarajio
Matarajio ya Nape ni kuweka matamanio yake katika vitendo. Miaka kadhaa iliyopita yeye amekuwa mmoja wa watu walioamini kwamba Serikali ya CCM imekuwa ikiyumba kwa sababu ya kuwa na “mawaziri mizigo” wanaoshindwa kusimamia mambo muhimu mengi ambayo kimamlaka yako chini yao. Leo naye amekuwa waziri, anatambua kwamba watu wanasubiri kuona tofauti yake na hao aliowaita mawaziri mizigo.

Wadau wa sanaa, habari na michezo ambao nimewafikia wana matarajio kwamba Nape anao uwezo wa kufanya vizuri ikiwa ataamua hivyo. Wengi pia wanaamini kuwa masuala ya propaganda siyo sasa tena na wanadhani kuwa kwa wadhifa wa uwaziri na ili ajijenge kisiasa anapaswa kusimamia “masuala ya kitaifa” kwa umadhubuti wake. Wengi walitarajia kwamba ni lazima angekuwamo kwenye baraza la mawaziri kama mtu anayeifahamu vizuri CCM, bado watu hao wanatarajia kwamba umuhimu wake ndani ya chama chake na Serikali atavitumia vizuri zaidi ili mwisho wa siku watu waone mabadiliko wanayoyataka katika wizara yake na zingine anazoweza kuweka ushawishi wa kitaifa.

Changamoto
Changamoto ya kwanza ambayo Nape anakwenda kupambana nayo ni kudorora kwa michezo hapa Tanzania. Hii ni nchi ambayo imewahi kuwika sana miongo kadhaa iliyopita hasa katika riadha na ndondi. Leo hii hakuna mahali unakoweza kupita ukawakuta Watanzania wanajivunia michezo, ni kama vile kila kitu kimekufa. Hatuna timu za vijana za michezo yote, muda wa michezo katika shule zetu umepunguzwa mno na hakuna walimu wa michezo. Vijana ambao wana vipaji hulelewa tokea wakiwa wadogo, kwa Tanzania hatufanyi hivyo. Siyo ajabu hata kidogo kila siku tunavyoshuhudia namna timu zetu zinavyobugia makapu ya “mayai’ na kutuletea tuyaatamie. Nape anahitaji mipango ya muda mrefu ili aweke historia ya kipekee.

Migogoro kwenye vyama vya michezo na timu mbalimbali ni changamoto nyingine. Jambo hili linaziathiri timu zote moja kwa moja lakini athari hizi huangukia kwenye timu za taifa pia. Kumekuwa na kasumba ya muda mrefu kwamba timu za taifa lazima zitoe wachezaji wengi kwenye timu kubwa, Simba, Yanga, Azam na nyinginezo, baadhi ya timu hizi zimekuwa mabingwa wa kupokezana migogoro na kinachofuatia ni kuambukiza migogoro hiyo hata kwenye timu za kitaifa na ndiyo tunaambulia kusaka visingizio kila siku timu zinapofungwa. Nape ana wajibu wa kutegeneza mfumo wa muda mrefu wa kuhakikisha kwamba migogoro inakuwa mwiko na vilabu vyetu vinakuwa na wadhamini wenye uwezo ili kuondoa kuyumba kusikoisha.

Katika eneo la habari kuna mambo kama manne ambayo ni changamoto kubwa. Kwanza kuna Muswada wa Vyombo vya Habari ambao hadi leo unapigwa dana dana. Muswada huu umekuwa ukipiganiwa na wadau kwa muda mrefu lakini kila mara Serikali inapojaribu kuupeleka Bungeni inakuwa imeshauharibu kimaudhui, unakuwa umejengwa katika misingi ya kukandamiza vyombo vya habari. Katika kikao cha mwisho cha Bunge la 10 almanusura muswada huo uwasilishwe na kupitishwa kuwa sheria, wadau wakaingilia kati, Serikali ikaona aibu na kuuondoa bungeni. Nape ana kibarua cha maana, kuwaonyesha Watanzania kuwa yeye binafsi na wizara yake na hata chama chake wanaheshimu Uhuru wa Habari, kila mtu anasubiri kuona namna atakavyoivuka kadhia hii na kuhakikisha kwamba kunakuwa na sheria imara itakayotenda haki sawa kwa wadau wote.

Jambo la pili ni sheria kandamizi zinazopokonya uhuru wa watu kupashana habari au kutoa habari, sheria hizi ziko nyingi na zimetengenezwa kwa namna ambayo inaiweka Serikali juu ya uhuru huo. Sheria zingine zimekuwapo kwa muda mrefu lakini ya hivi karibuni, (Sheria ya Uhalifu wa Mitandao) ndiyo inatumiwa kama rejea halisi kuthibitisha kuwa Tanzania inaingia kwenye mtego wa kuweka haki za kupashana habari hatarini. Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Milenia (MCC) imesitisha msaada wa zaidi ya shilingi trilioni moja za Tanzania sababu mojawapo ikiwa Tanzania kupitisha na kutumia sheria hiyo. Nape na wenzake wana jukumu la kukaa chini, kubaini sheria hizi, kushirikisha wadau na kuzifanyia marekebisho ya haraka.

Jambo la tatu ambalo linabaki kuwa changamoto ya kudumu ni “kutumika vibaya kwa televisheni ya taifa”, televisheni hiyo ambayo inajiendesha kwa kodi za wananchi imeacha kuwa ya taifa na kufanya kazi kama chombo cha propaganda za chama kinachoongoza dola, jambo hilo linamuumiza kila mwananchi anayetambua wajibu wa vyombo vya habari vya taifa kwa wananchi wake. Shirika la Utangazaji la Taifa halijaishia hapo tu, limekwenda mbali zaidi na hivi sasa linaweza kuthubutu kuahirisha vipindi muhimu kama taarifa ya habari ili kurusha moja kwa moja matangazo ya harusi za watu binafsi. Watanzania wanataka kuona shirika hili linahudumia taifa, vyama vyote vya siasa na wadau wote kwa usawa kabisa na mwenye jukumu la kurejesha nidhamu hiyo ni Nape mwenyewe.

Changamoto ya tatu kwenye habari ni maslahi ya waandishi wa habari. Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa waandishi wengi wa habari kwamba baadhi ya vyombo vilivyowaajiri haviwapi mikataba wala malipo mazuri, havizingatii sheria za ajira kwa kuwapa wataalam hawa malipo ya kazi za ziada, likizo na motisha. Waandishi wa habari wanaofanya kazi kwenye vyombo vya namna hii wamegeuka kuwa watumwa, ombaomba na watu wanaotegemea kulipwa Sh10,000 au Sh20,000 na wadau wakubwa wanaotaka habari zao zitangazwe. Matokeo ya jambo hili ni kuwapo kwa upendeleo wa habari kati ya wale wanaotoa “posho” na wale wasio na uwezo wa kutoa posho. Mwisho wa siku tasnia ya habari inadharaulika na kuonekana kama imejaa “makanjanja” wakati ina watu imara na waliobobea kwenye fani zao, lakini wasiolipwa na kupewa stahiki sahihi ili wafanye kazi kitaalamu. Nape anahitaji mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu kupambana na hali hii.

Hitimisho
Watu wengi wanamchukulia Nape kama mtu anayekurupuka, asiye na busara wala hekima. Mimi namchukulia kama mwanasiasa mwenye mipango mingi madhubuti na anayeweza kusimamia mambo anayoyapanga, naiona nyota yake kisiasa ikikua zaidi na akifika mbali zaidi siku za usoni. Jambo la msingi na ambalo ni kitisho kwake ni kujivua siasa za unazi na “utetezi wa CCM” na kujivika siasa za uhalisia na za kutafuta majibu ya matatizo ya wananchi. Kwa umaarufu mkubwa alionao bila shaka wananchi wengi watapenda kuifuatilia wizara yake na utendaji wake, wananchi wanajua changamoto anazopaswa kuzishughulikia. Tofauti na mawaziri wasio maarufu sana, watu kama Nape wanaweza kuwa kwenye wakati mgumu zaidi kisiasa ikiwa hatatekeleza matarajio ya wananchi. Namtakia kila la heri.

KUHUSU MCHAMBUZI
Julius Mtatiro ni Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa na Kijamii. Ana Cheti cha Juu cha Sarufi (“Adv Cert of Ling”), Shahada ya Sanaa “B.A” katika Elimu (Lugha, Siasa na Utawala), Shahada ya Umahiri (M.A) ya Usimamizi wa Umma na Shahada ya Sheria (L LB); +255787536759, juliusmtatiro@yahoo.com, Jos haluat nähdä sisällön, kirjaudu sisään tai rekisteröidy, - Uchambuzi huu unatokana na utafiti na maoni binafsi ya mwandishi).
1594971714950.png
 
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;

  • Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
  • Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu "3" kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
  • Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
  • Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
  • Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa –Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
  • Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
  • Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika "thesis" iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)
Butimba Alevel?
 
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika "thesis" iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)
TandaleOne Master of Business Administration na sababu zinazochangia ushiriki wa wapiga kura zina uhusiano gani? Angefanya "Reasons lead to poor performance of public corporations" hii kidogo ingelandana na hiyo master yake @Nnauye Jr
 
tunataka aweke alama alizozipata A'level na O'level, hakuna aliyeomba CV hapa! aonyeshe masomo yake alifaulu vipi!
By the way nape yupo mbona mnaleta ukada hapa si aje mwenyewe? hata sisi ambao hatuna vyama tupo interested na kujua perfomance yake equally alivyokuwa anamponda mnyika!
 
Back
Top Bottom