Hii mboga inaliwa? Msaada wenu!

Mtatuongezea idadi ya watu wanaohitaji kusafishwa damu. Kitu haujawahi kula unamchuuza mwenzako.
hiyo mboga inaitwa mchicha mshenzi ukichanganya na nyingine inaitwa mgagani, ambayo yenyewe ni chungu, mboga hiyo inakua tamu zaidi na ni tiba pia 🐒

kama hujaishi kijijini na wanainchi huwez elewa hiyo kitu, utakua na fikra kama hizo tu ambazo ni upotoshaji 🐒
 
Kula majani hayo ni mboga safi sana na salama. Kuuogopa ni sawa na kuogopa mtama mwekundu kwa rangi yake hali mababu zetu huko Kishapu, Bariai, Maswa, Igunga n.k wamekula na walikuwa imara zaidi ya wala mahindi ya panna, zam seed n.k

Waabeja sana Mwandende, kwa kiangazi unakubali?
 
ni miongoni mwa mboga mujarabu sana huku kwetu,
yote nyekundu na isiyo nyekundu tunaitumia barabara🐒
asubuhi ni mboga ya faster fasta sana, chapchap na kiporo cha kuchoma au kupasha, na mchana na ugali mujarabu wa dona na maziwa mtindi 🐒

wewe acha kabisaa mimi na wanainchi wangu ni bam bam kwenye misosi....

Thanks mkuu, nitaanza kuula
 
huo mchicha una afya sana, mwanaume hapo kula na dona maziwa mgando msuli unasimama mpaka kende zinatoa jasho
 
Siku si nyingi tumtasikia kamanda wa polisi wa mkoa fulani akitoa taarifa ya watu kadhaa wa familia moja wamefariki kwa kula mchicha pori
 
Mchicha pori mwekundu je! Unaliwa ama sumu?

Na upandaji wake ni kama mchicha tuliouzoea?

Hivyo nikisema nijaribu kuupanda unakubali kwa all season kwa maana kiangazi na masika?

Mchicha pori nimetokea kuupenda sana sana, ila huu mwekundu unanipa mashaka kama unaliwa.
View attachment 2934369View attachment 2934370

Msaada wenu wanajamvi.

Herbalist Dr MziziMkavu n.k
Mtamu sana huo na unaongeza nguvu za kiume.
(wanaume wa Dar siyo kila kitu cha kujaribu plz....najua mpo na hili ombwe........)
 
hiyo mboga inaitwa mchicha mshenzi ukichanganya na nyingine inaitwa mgagani, ambayo yenyewe ni chungu, mboga hiyo inakua tamu zaidi na ni tiba pia 🐒

kama hujaishi kijijini na wanainchi huwez elewa hiyo kitu, utakua na fikra kama hizo tu ambazo ni upotoshaji 🐒
Mgagani niujuao mimi unamajani madogo na hutumiwa na wasukuma, wanyamwezi, wagogo na wanyiramba na majirani zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom