Hii interview ya Rightway Primary school inatesa watoto

😃😃😃 Yaan katoto ka 1-3 kana pigwa interview jaman haya ni maajabu binafsi nayaona embu naomba nijuze interview ya watoto wa umri huo una husisha nini hasa ?
general knowledge, ewe kama mtoto wako unamuwekea WASAFI TV siku nzima anajifunza kumenua kiuno kama maua sama ndio itafahamika, ataulizwa unapenda mziki gani, unajua kuucheza, etc atajibu na takjata mauno, hiyo ndiyo general knowledge
 
Okay !
 
Leo ni siku ya interview hapa Rightway Nursery and Primary school, Mbezi .
Haiwezekani mtoto wa lower primary school(std 1-3) afanye mtihani kuanzia saa 2 Asbh mpk saa 7 mchana . Mtoto anatahiniwa masomo 4 .Wakati zamani kwenda form one unatahiniwa masomo 2 tu, Hesabu na Kiingereza.
Naomba wizara ya Elimu ifatilie hili Jambo. Yaonekana hIzi english medium schools haziratibiwi ipasavyo.
Inaonesha ukilaza wa wenye shule na waalimu wao. Hawaoni hata mfano mtihani wa taifa inachukua muda gani?
Ujiulize je waalimu walisomea saikoloji ya upevu wa akili ya mtoto? Usanii kila pahala na majanga juu.
 
Shule nzuri inapika wanafunzi yenyewe sio kudandia tu watoto vichwa alafu wajewajichukulie sifa na utukufu wao
Kwa Tanzania yetu wazazi wanaangalia matokeo ya necta haijalishi shule imewapika au imechukua vichwa
 
Unajuaje kama mtoto mdogo ni kilaza au sio kilaza.. Mtu ubongo unakamilika kujua akifikisha miaka 10..
Kumbuka matokeo mazuri ndio sale point ya shule za Kitanzania, hivyo wenye shule lazima wapige mchujo mkali ili wapate wanafunzi bora, wafaulu necta, shule ipate sifa, wanafunzi wengi wajiunge, shule wapige pesa.
Tukitaka kubadilisha hili labda serikali ianzishe mfumo wa kurank shule kwa sifa kadha wa kadha sio kwa kigezo cha matokeo ya necta tuu.
 
😃😃😃 Yaan katoto ka 1-3 kana pigwa interview jaman haya ni maajabu binafsi nayaona embu naomba nijuze interview ya watoto wa umri huo una husisha nini hasa ?
Unawaacha wacheze wakishikwa na haja kubwa unaangalia kanavyo omba msaada. Vile visivyo na tabia nzuri Vita poo kwenye nguo.
 
Elimu ya kifala sana hii, wazazi wanajali sana ufaulu wa mtoto kuliko maarifa anayopata. Mzazi haulizii shule ina facilities gani (computer, viwanja vya michezo, usalama wa watoto, lishe, nk), wao wanauliza tu inafaulisha? Shule ilikuwa ya ngapi kwenye mtihani wa NECTA? Upuuzi mtupu.
 
Elimu imekuwa biashara na middle class ndo wamechangia kurasimisha hili, kiss eti kiingereza. Shule za public hazina wa kuzipigania. Hii ndo nchi pekee ambapo private schools zimeshika hatamu. Ukienda nchi za wenzetu kama Kenya, au Uganda, Mwanafunzi aliyesoma public yupo vizuri zaidi ya wa private bongo. Kuna katabia kameanzishwq na baadhi ya shule kununua mitihani halafu watoto wanakaririshwa na baadaye shule kuonekana inafaulisha sana. Lakini wengine wanapofika ELIMU ya juu wanaonyesha uwezo duni wa kuhimili taaluma. Tunahitaji mjadala wa kitaifa. Kwanini tumekubali public schools zife?
 
Leo ni siku ya interview hapa Rightway Nursery and Primary school, Mbezi .
Haiwezekani mtoto wa lower primary school(std 1-3) afanye mtihani kuanzia saa 2 Asbh mpk saa 7 mchana . Mtoto anatahiniwa masomo 4 .Wakati zamani kwenda form one unatahiniwa masomo 2 tu, Hesabu na Kiingereza.
Naomba wizara ya Elimu ifatilie hili Jambo. Yaonekana hIzi english medium schools haziratibiwi ipasavyo.
Kwani lengo la mimi kuwapelekea mtoto ni nini!?
 
Tunahukumu vibaya kwa kukosa taarifa sahihi toka upande wa shule.

Kuna mdau kafafanua hiyo shule wanapima watoto na tabia zao, hivyo katika hayo masaa mengi wanakuwa wanacheza tu huku wanamsoma character zake, kama mbaya wanamkataa hata kama mitihani ya taaluma kapa 100% yote.
Mimi personally watoto wangu wawili nawasomesha hapo na siwezi kuwahamisha, it is one of the best schools. Angalia matokeo yake kimkoa na hata kiwilaya imafanya vizuri sana.

Alieanzisha mada hii hata hana alijualo kuhusu shule hii.
 
Wawapunguzie ada watoto wanaofaulu sababu wazazi wao tayari wameshafanya kazi kubwa. Siyo kuwaadhibau wazazi kwa ada kubwa.
Hao wanachukua Top layers ili ziwasaidie ku brand biashara yao
If you think education is expensive try ignorance. kama unauelewa msemo huu basi utatulia
 
Mimi personally watoto wangu wawili nawasomesha hapo na siwezi kuwahamisha, it is one of the best schools. Angalia matokeo yake kimkoa na hata kiwilaya imafanya vizuri sana.

Alieanzisha mada hii hata hana alijualo kuhusu shule hii.
Nyie ndio wale mnapima ubora kwa matokeo ya mkoa!? Does your kids learn and adopt the knowledge!? Au mnataka ushindani tu ..tumekuwa wa kwanza ...kimkoa!?

Watoto wanapimwa kwa kukariri taarifa .. jana kuna mtoto wa kitanzania ametoka shule namuuliza kesho kwanini hamuendi shule akaniomba kwanza "Niongee kingereza" !? Nikasema sawa..

Akajibu Because tomorrow we are celebrating Tanganyika Independence day! Nikamuuliza na kwa kiswahili!? Hajui... Huyu mtoto kakariri.. wazazi wake Wanakenua tu utadhani kuongea kingereza ndio mtoto ameelewa... na shule inakuwa ya kwanza kimkoa huku kwetu mpaka ya nne kitaifa....

Elimu lazima ije na Maarifa. Kama mtoto hawezi kuitafsiri Elimu its useless... Hata angekariri dictionary na kupass mitihani yote..
 
We kwanza hata sidhani kama unasomesha au unawatoto. Kama unaufahamu kwa mimi tuu kukuambia watoto wangu nawasomesha hapo na sina mpango kuwatoa basi itoshe kukaa akilini kwako kua shule ni nzuri.

Nimeuwona uwezo wa watoto wangu tokea wanaanza na wanavyo kua kiakili, kielimu na uwezo wao wakuchanganua mambo.

Sasa tunaweza tofautiana kama ungeniambia nawe unamwanao hapo anasoma au kashawaji kusoma, ila kwa mimi mpaka sasa katika shule zote nilizotembelea in mbezi so far its the best school.
 
Back
Top Bottom