Hii imewezekana vipi? napata taabu kuamini kilichotokea

Jina lake kanitajia mkoa alipo kwa sasa aisee ni girl wangu wa mkoa nikabaki mdomo wazi sikuwa na kufanya nikarukia daladala kuelekea mbezi mwisho appointment yangu na faza ikaharibika
Wakuu hii imewezekana vipi? bado jibu sipati nikijihoji

Ngoja nikushauri faza,
Siku nyingine ukiwa umemzoea tu mshichana na humpendi, ukakuta kuna kidume chenzio kimeinverst Heavily hapo fanya hivi;
Mueleze huyu msichana tumekuwa wote na hili jina la mahaba huwa namtania lakini yeye hataki. Kisha baadae mjulishe huyo msichana kuwa hujamharibia kwa mtu wake, kisha muonye aache mazoea. Don't let the normal flow of life to stop over a girl 'Uliyemzoea tu'
 
Akili yangu inaniambia si kweli.
Umechezewa mchezo
Huyo jamaa bilq shaka alienda kucheki namba inayopigwa mara kwa mara au iliyoandikwa jina la kimahaba..
then akaichukua na kumpigia kumuuliza Abcd akijifanya kuungwana pengine kutaka kumsaidia,au ameshinda biko,au ni jamaa kutoka mtandao flani,ili apate detail za dem wako aje akuzingue ww.
Either aku(wa)kuibie au waondoke na ww wakatimize lengo lao.

Km Dem angekua wake kweli jamaa angeuchuna anze kufuatilia nyendo za dem wake mpk ambambe.

Huwezi ukamvaa mtu from no where na kumwambi ni dem wako kaipataje namba.
Je kama ni Babaake mdogo,Au Binamu au Auncle wake.
Wewe utakuwa ujasiri gani kufanya hivyo tena mtaani,anajiamini nn km sio tapel yupo na kampani yake?
Nina uchambuzi wa kutosha ila acha niachie hapa.
Faza hata mimi naona ni ndoto siamini kabisa naona ni kitu ambacho hakiwezekani lakini sikuwa nimelala faza ningesema naota
 
Hii story mbna kma ina umande si mngempandia hewan bidada mpate muafaka

Au kila mtu hatak kuachwa
 
Sasa mkuu ningekuwa wewe ningembana huyo jamaa anieleze kila kitu.

Cause you never know,usikute jamaa ndo anamfukuzia alafu ukamhisi vibaya girl wako.
 
Maandishi yako yanaakisi uhalisia wako, binafs nakuona huna future na huyo mdada hata yeye nahis analijua hilo, hizo safari za mkoan to dar huenda mlengwa hukua wewe, wewe ulitumika kama sponsor wa safari au wa mambo madogo madogo, najua umekua disappointed kwa kilicho tokea lakini kubali ulipo 'kosea' kuna kitu huyo mdada hajakiona kwako ndio maana akatega sehem ya pili.
 
Kwani hukuwahi onaga uzi kuhusu wanawake wa kilokole aliletaga jamaa mmoja alikula mashambulizi ya kutosha humu kama vipi utafute uzi ule..
 
Yaani unashangaa kupata bahati ya kipekee ya namna hiyo, MOLA amekudhihirishia tabia mbaya ya mwanamke uliyenaye, huyo hana ulokole wala nini anajifanyisha tu ili uje umuoe, huenda amekuona waweza kumfaa kuwa mme.


ANGALIZO: JE mliangalia namba vizuri kama ndiyo yenyewe maana iliwahi kunitokea binamu yangu alichukua simu yangu kumpigia mpenzi wake, ghafla likaja jina la mwanamke badala ya namba tu, akakata simu huku tukabaki tunashangaana na kuulizana imekuaje, tukaamua kuangalia namba vizuri na kubaini kuwa namba zilifanana kasoro moja tu, kwahiyo kumbe mtandao wa simu ndiyo ulikuwa na tatizo la kufananisha namba za watu wawili ilhali zinatofautiana.
 
Yeah hii inawezekana kabisa mzee!!!

Sijajua khasa point yako ni ipi mkuu ila sidhani kama wewe ndiye uliyepaswa kujiuliza coz hiyo scene umeiona wewe uso kwa macho tunaopaswa kujiuliza ni sisi kwamba imewezekanaje na kwanini iwe hivyo?

Miujiza amma!?ndo maana nasemaga hawa wanaojifanya walokole sana ndo wabaya kuliko hata wale wasio-act ulokole, ushauri wangu huyo muache tu na kama ulivyosema hujui kama unampenda au lah naona una nafasi kubwa sana ya kutokuumia.
 
Salamu sio muhimu sana i hope amani imetawala

Niko na girlfriend wangu me naishi Dar na yeye yuko mkoani huyu manzi sijajuana nae jana bali kitambo sana tumesoma wote primary baadae familia yake ikajaga kuhama na kwenda mkoa wa mbali kidogo lakini wakati hayo yote yanatokea hatukuwa wapenzi, tulipotezana kwa takribani muongo na pointi mbili hivi baadae tumekuja kuonana mapenzi yakaja automatically akaniletea shobo nyingi nikamdandia

Ni mwaka wa pili sasa yupo na mimi analeta mapenzi mengi sana na me nimemzoea sana nasema nimemzoea kwasababu me sijui kupenda namzoeaga mtu tu sijui ndo kupenda kwenyewe au la ameshalifungaga safari toka mkoani kuja Dar kwaajili yangu kama mara mbili hivi wasifu mkubwa wa huyu manzi ni mlokole sana mcha mungu mno na ndivyo familia yao ilivyo.

Ishu iko hivi jana wakati natoka kwenye mishe zangu town nikashukia kimara baruti kuonana na mzee fulani hivi maana me nakaa mbezi mwisho wakati namsubiri huyo faza nikawa napata soda kwa duka moja mitaani hiyo, kuna jamaa alikua kakaa pale baada ya stori kadhaa akaniomba nimsaidie simu yangu kama ina salio apige nami bila hiyana nikafanya hivo.

Nakiri kabisa huyu mwamba simjui hanijui na wala hutujawahi kuonana mahali popote haikuchukua mda sana jamaa akaanza kunihoji kwa ukali kwamba namba ya mchumba wake nimeipata wapi? na nina uhusiano gani na yeye?maana namba niliisevu kimahaba akadai kuwa ni mchumba wake mda mrefu toka wako chuo na wana mipango ya ndoa.

Jina lake kanitajia mkoa alipo kwa sasa aisee ni girl wangu wa mkoa nikabaki mdomo wazi sikuwa na kufanya nikarukia daladala kuelekea mbezi mwisho appointment yangu na faza ikaharibika
Wakuu hii imewezekana vipi? bado jibu sipati nikijihoji
Kuna kitu sijakuelewa kwa kuwa hujamalizia mkasa ulivyo, yani mtu umemkuta mahala humjui hakujui na pia ilikuaje akuombe simu wewe na akute namba ya the same girl anaemzungumzia? Hivi mazingaombwe yapo bado? Hebu rudi foa ufafanuzi vizuri
 
Back
Top Bottom