hii imetokea dodoma

kiapo kipo sawa, tuache kuweka fikra za udini mbele, itafikia watu hawataweka status ya Dini kwenye cv zao eti wakihofia watabaguliwa makazini. Swala la msingi ni wahitimu gani tutawajenga udom huku wakiwa wamejengewa hofu kiasi hiki? Naamini kuthubutu na kusimamia haki zako ni part n parcel ya elimu. Nadhani wanafunzi badala ya kudai haki zao hadharani watadai kwa siri kwani mnaweza kuamka chuo kimechomwa moto.
 
ninachokiona hapa ni vitisho/ubabe haya wadogo zangu akufukuzae hakwambii toka, mvumilie tu mmalize chuo hayo mambo mengine ya kudai haki yawekeni pembeni kwa muda uliobaki maana hicho kiapo wakiamua kuwa serious hasara itakuwa kwenu, well sijui kama sasa hivi tz kuna credit transfer
 
Picha ya Mwanafunzi
HATI YA KIAPO YA MWANAFUNZI
Mimi, ……………………………….,Muislamu/Mkristo/Mpagani, nikiwa na akili zangu timamu na bila kushurutishwa, NAAPA NA KUTHIBITISHA kwamba;
1. Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa………………….Chuo Kikuu cha Dodoma.
2. Namba yangu ya usajili ya Chuoni ni………………………………………………
3. Nathibitisha kwamba mimi………………………………………………… nimelipa madeni yote ninayodaiwa na Chuo ikiwa ni pamoja na kulipa gharama ya usajili wa kurudi chuoni baada ya kusimamishwa masomo.
4. Naapa kwamba mimi……………………………………………………………….
nitakapokuwa nimesajiliwa upya nitatii sheria za Chuo na kanuni zake,sheria ndogo za wanafunzi na sheria za nchi kwa ujumla. Na kwamba mimi………………………………………………………………………………..nitatumia muda wangu kusoma badala ya kujihusisha au kuhusika kwenye migogoro na siasa chuoni.
5. Mimi………………………………………………………………………………..nitatumia uongozi wa Chuo kupata msaada pindi ninapojikuta kwenye mgogoro nisiokubaliana nao.
6. Kwa kiapo hiki mimi………………………………….……………………………
naahidi iwapo nitashindwa kuzifuata sheria hizo Chuo kiniondoe masomoni mara moja.
7. Natoa kiapo hiki nikitambua Sheria ya Viapo na matamko Sura ya 34 ya Mwaka 1966 [Sura 34 Marejeo 2002]
UTHIBITISHO Nathibitisha kwamba, yale yote yaliyosemwa katika aya ya 1, 2, 3, 4, 5, 6, na 7 hapo juu ni kweli tupu kwa kadri ya uelewa wangu. Imesainiwa hapa …………………….., hii leo tarehe………………………..., Mwezi wa…………….2011.
Saini ya Muapaji…………………….. Jina la Muapaji………………………
Kiapo kimetolewa hapa ………………. na
…………………., ambaye ametambulishwa
Kwangu na ……………………......................
Ambaye nimemfahamu binafsi hii leo
Tarehe……… Mwezi wa………… , 2011
MBELE YANGU
KAMISHNA WA VIAPO

NAHISI ENZI ZA MANAMBA INA ZINAREJEA NCHINI. Wanasheria mko wapi? Tunaomba mtufafanulie sheria ya kiapo inatumika maeneo yapi? Hii ya chuoni nimeiona UDOM. ikifanikiwa hapa itatumika sekondari, shule za msingi na hata tutakapoingia ofisi za serikali kupata huduma.
 
Kuonyesha imani ya dini kwenye kiapo hicho ni makosa. Affidavit za kuthibitisha uraia au kuzaliwa mbona hazina mambo ya dini na mimi ninazo affidavit zilizosainiwa mahakamani, na hakuna mahali popote suala la dini limeonyeshwa. Nadhani kuna kitu kimekusudiwa.
 
Sasa nyinyi kiapo si lazima ijulikane anaapishwa na kitabu gani au aapishwe na katiba, hata bungeni inatumika, tunapoapisha mawaziri, mahakimu, mahakamani hutumika hivyo hivyo na hata unapokwenda kutoa statement polisi unaulizwa dini gani. Mbona mnaifanya kuwa issue kuuubwa kama ndio kwanza inaanza kutumika? Mnashangaza sana!

FaizaFoxy, hivi ni viapo fake hakuna kitabu chochote cha dini wanchoshikishwa hawa vijana wala sidhani kama kuna hakimu au wakili anayesimamia hivyo viapo labda wanasheria watatujuza zaidi
 
Back
Top Bottom