Hii hapa ni tathmini fupi baada ya mikutano michache ya hadhara ya Chadema

Kwa ujumla ni kwamba sasa ni dhahiri kwamba Watanzania wote wanataka waongozwe na Chadema, ukiachilia mbali watoto wa viongozi wa CCM na binamu zao na familia zao na hao wanaojiita Chawa. Kimsingi, hao wanaojiita Chawa ni koo za viongozi wa CCM, tena wale viongozi wa juu. Mimi natokea Kyela, kule hakuna Chawa wa CCM. Hii ni kwa sababu hakujawahi kuwepo viongozi wowote wa juu wa CCM. Hata watoto wa Elias Mwanjala au Harrisson Mwakyembe si Chawa wa CCM.

Wananchi wa Tanzania wamechoshwa na dhiki isiyoisha. Kote ilikopita, Chadema wananchi wanaililia. Wanataka leo kesho utawala wa kitapeli, mabavu na dhuluma uondoke haraka. Wananchi wanataka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ili warudi tena kupiga kura ili kuhalalisha uchaguzi. Hebu fikiria, mnaandikisha watu mil 29 lakini wanaojitokeza kupiga kura ni mil 9 tu. Lakini kwa vile mnategemea wizi wala hamjali kitu, mpinzani anapata kura mil 7.6, wa kwenu anapata chini ya kura mil 1.5 lakini anatangazwa kapata kura mil 12. Kazitoa wapi ikiwa waliojitokeza hawakuzidi 10mil?

Mpaka leo, Tume ya Uchaguzi ya Tanzania haikuweka kwenye tovuti yake matokeo ya Urais 2020. Unadhani ni kwanini?

Kwa kadiri ya macho yangu kwenye mikutano ya hadhara iliyopigwa na Chadema kanda ya Nyasa na kwingineko, yafuatayo yafanyike:

Chadema Digital iongezewe nguvu kila jimbo. Mahitaji ya watu kujiunga na Chadema ni makubwa mara 10 zaidi kuliko wakati wowote. Wengi wanaiita kadi ya Chadema kama Kadi ya Uhuru na kujitambua, kwamba ukiwa na kadi ya Chadema unaonekana unajitambua na pia unaonekana ni mpigania haki. Heshima yako kwenye jamii inaongezeka.

Yaanzishwe maduka ya Sare na Magwanda ya Chadema kila Jimbo. Mahitaji ya mavazi haya sasa yanatakiwa kwa zaidi ya mara 10 kuliko awali. Binafsi, nimelazimika kugawa zaidi ya sare zangu 7 za Chadema, yakiwemo magwanda yangu makali mawili kwa wenye uhitaji.

Mambo haya ni muhimu sana yakafanywa haraka.
Laana ya Mwenyezi Mungu IPO juu ya CHADEMA, imetawala katika vinywa na midomo ya viongozi wa chadema,Ni laana kutoka ofisi za chadema Hadi katika vichwa vya viongozi wake. Ni laana katika hotuba zao Hadi katika mipango na mikakati yake.

Ni chama ambacho kimepigwa na upofu na mkono wa Mwenyezi mungu, Ndio sababu ya kuona hotuba za viongozi wao wakubwa Kama akina Lema mjumbe wa kamati kuu wakiwatukana Watanzania, wakiwadhalilisha vijana,wakitukana mama zetu, dada zetu na wazee wetu, kwa Sasa Chadema haipo Tena na wananchi na haiongei Tena habari za nguvu ya umma maana kwa Sasa Chadema wanaongea kutokana na nguvu za matumbo Yao na midomo Yao, Sasa viongozi wa chadema wameshiba na kuvimbiwa viinua mgongo vyao, Sasa wanatapika na kuwatapikia watanzania matusi.
 
JamiiForums442997317_236x211.jpg
 
Back
Top Bottom