Hii hali nitaiepuka vipi?

Niko social vya kutosha kabisa mkuu, sometimes hata mtu akiniona siku ya kwanza hapo hapo ananihisi

Ndugu wewe umesema (na unadhani) uko social vya kutosha. Lakini inawezekana unaji-assess vibaya. Huko social vya kutosha au u-social wako ni wa kidadisi dadisi. Watu wengi wanaohisiwa ni polisi au wapeleleze huwa wanakuwa hawako social na hawachanganyiki sana na watu wa kawaida kwenye shughuli za kawaida. Na ndio maana mtu akikuona tu mara ya kwanza anakudhania vingine, kwani kwa dakika za kwanza tu anakusoma unavyo-behave.
 
Mimi sidhani kama unaonana na mtu dk ya kwanza tu atakuhisi wewe ni usalama wa taifa. Mimi nadhani ni kutokana na maisha yako ya kila siku na jamii inayokuzunguka iwe kazini au nyumbani. Pia upo uwezekano kabisa wa kuhisiwa hivyo inatokana na aina ya watu unaishi nao( nyumbani) na unavyoshirikiana nao, pia hulka yako kwenye maisha yako ya kila siku inawafanya watu wahisi hivyo. Inawezekana kabisa mfumo, hulka na tabia zako ktk maisha yako ya kila siku yanafanana na USALAMA WA TAIFA.

Mimi nahisi kuna muonekano, tabia fulani zako wewe ambazo huwa zinajitokeza kwenye jamii inayokuzunguka mpaka inakuhisi kuwa wewe ni usalama wa taifa.

Hali hii kwako ina faida na hasara zake. Kwa mtazamo wangu hasara ni kubwa zaidi. Una wajibu wa kujua kwanza kwa nini watu wanakuchukulia hivyo, mimi nina uhakika kuna kitu au tabia unayoifahamu ambacho unahisi watu wanaokuzunguka huanzia hapo kukufikiria hasi na jinsi ulivyo, JITAMBUE na BADILIKA basi utaona utofauti.
 
Nikiona ID yake tu huwa nakuwa attention kuisoma kuliko nyingine,sijawahi jutia kusoma comments zake japo ID yake pia ni burdan

Mbona unanifanya nisiweze kutoka nyumbani? Maana sasa kichwa kimekuwa kikubwa hata milango haitoshi.

Asante mkuu.
 
usalama wa taifa wakoje kwani?

mtoa mada anajihisi mwenyewe ndio maana anahisiwa!!!

Hata mimi sijui wako vp, uposema ajihisi mwenyewe una maana gani?
kwamba watu wanaonihisi wanaweza ku access hisia zangu na kujua kilicho ndani? elezea kidogo tafadhali
 
Ndugu wewe umesema (na unadhani) uko social vya kutosha. Lakini inawezekana unaji-assess vibaya. Huko social vya kutosha au u-social wako ni wa kidadisi dadisi. Watu wengi wanaohisiwa ni polisi au wapeleleze huwa wanakuwa hawako social na hawachanganyiki sana na watu wa kawaida kwenye shughuli za kawaida. Na ndio maana mtu akikuona tu mara ya kwanza anakudhania vingine, kwani kwa dakika za kwanza tu anakusoma unavyo-behave.
Asante kwa ushauri wako mzuri,

nitaufanyia kazi, lakini kuhusu udadisi mimi nadhani siyo kitu kibaya kama mtu una nia njema tu ya kutaka kujifunza na kuongeza maarifa katika mambo mbalimbali
 
Ni kawaida mitaani, watu wakiwa hawafahamu shughuli anayofanya mtu huku akiwa na maisha fulani yanayoeleweka na utaratibu fulanivwa maisha ya kujiheshimu, huwa wanaconclude kuwa ni mtu wa usalama. Wengine ni wale wenye tendencies za kihalifu ambao huwa wanamshuku mtu yeyote.
 
Mimi kila nikipita mahali wanadhani ni kada wa CCM aliyehamia CDM. Hivo kila nikiwa sehemu yoyote napata big up na polisi wananiogopa sana maana wanahisi kwenye serikali ijayo nitakua waziri anaepambana na rushwa ndogo ndogo.
 
Unagombea jimbo gani mkuu, au utakua mbunge wa kuteuliwa/viti maalum?
 
Back
Top Bottom