Hifadhi ya Serengeti yatwaa tuzo ya Ubora Afrika

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019

Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora kwa Bara la Afrika kwa mwaka 2019, tuzo iliyotolewa jana na Taasisi ya World Travel huko nchini Mariutius.

Hii ni ya pili kwa Hifadhi hiyo ya Serengeti kutangazwa kuwa hifadhi bora Afrika baada ya mwaka jana 2018 kushinda tuzo hizo kupitia mtandao maarufu wa safari za utalii dunia wa safaribooking.com.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, washindi katika tuzo hizo za WTA hupigiwa kura na wabobezi katika masuala ya safari na utalii duniani kote.

Wengine walioingia katika kuwania tuzo hizo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Central Kalahari ya nchini Botswana, Hifadhi ya Taifa ya Etosha ya nchini Namibia, Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Kidepo Uganda, Hifadhi ya Taifa ya Kruger nchini Afrika kusini na Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara ya Kenya.
 
Vipi kuhusu Wakazi wa hiyo Hifadhi na Wao wametajwa kuwa katika Maisha bora ya Kiwango gani duniani yaliyotokana na kuwa karibu nayo?
 
Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora kwa Bara la Afrika kwa mwaka 2019, tuzo iliyotolewa jana na Taasisi ya World Travel huko nchini Mariutius.

Hii ni ya pili kwa Hifadhi hiyo ya Serengeti kutangazwa kuwa hifadhi bora Afrika baada ya mwaka jana 2018 kushinda tuzo hizo kupitia mtandao maarufu wa safari za utalii dunia wa safaribooking.com.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, washindi katika tuzo hizo za WTA hupigiwa kura na wabobezi katika masuala ya safari na utalii duniani kote.

Wengine walioingia katika kuwania tuzo hizo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Central Kalahari ya nchini Botswana, Hifadhi ya Taifa ya Etosha ya nchini Namibia, Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Kidepo Uganda, Hifadhi ya Taifa ya Kruger nchini Afrika kusini na Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara ya Kenya.

1115915
 
Kwa hiyo tumsifie jiwe? Maana yule jamaa kwa kupenda sifa za kijinga hajambo
Nafikiri Nyinyi ndio mna mambo ya KIJINGA coz mko kwa ajili ya KUPINGA na kukejeli tu. Hata hapa umeonesha hii Tabia. Ungechangia bila kejeli za jiwe na kwingine nini kingepungua?
 
Poa sana aisee wachunge tu mbuga isije ikajaa mifuko ya plastiki.
 
Hii imependeza kwa masilahi mapana ya Taifa letu Tanzania.
Tuzidi kuhamasisha watalii ili kuukuza uchumi wa taifa letu.
 
Halafu inakuaje wilaya ya serengeti ni miongoni mwa wilaya maskini hapa Tanzania.

Kwanini mapato yoteyapelekwe mkoa wa Arusha na si Mara?
 
Back
Top Bottom