Heshima siyo kitu cha bure, usijidanganye

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,243
12,767
Nadhani umewahi kukutana na watu wakilalamika, "Mke wangu haniheshimu. Wadogo zangu wananidharau." Wengi hawa wanaamini kuwa maneno ya wahenga kuwa heshima ni kitu cha bure ni ya kweli.

Ukweli ni tofauti kabisa. Binadamu siku zote wanamheshimu mtu mwenye uwezo, yaani mtu capable. Social animals wote tupo hivyo, hata simba na mbwa mwitu hulifuata na kuliheshimu dume lenye uwezo. Kama upo upo na huwezi kutimiza yale unayotarajiwa kutimiza hakuna mtu atakuheshimu. Mtu hujiletea heshima na dharau yeye mwenyewe.

Siku moja waalimu walimwita mzazi wa mtoto mmoja mtukutu. Wakamwambia, "Mwanao jeuri na hana heshima. Hata tukimchapa anacheka tu." Yule mzazi akawajibu, "Hilo ni kosa lenu. Mbona mi nikimchapa huwa hacheki!"

Ipo hivyo, ukiona mke wako, mtoto wako au watu ofisini kwako hawakuheshimu. Jitathmini. Ukiona dharau zao zina sababu za msingi jirekebishe. Ukiona hazina msingi wapuuze. Lakini hata siku moja usilaumu watu kwa kutokukuheshimu. Heshima siyo kitu cha bure.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom