Heshima sio kitu cha Bure

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Kwema Wakuu!

Ukiona unataka kuheshimiwa na kila mtu basi jua hujiamini.

Mara nyingi mtu akikosa pesa tena Kwa bahati mbaya akakosa na elimu basi hufikiri kila mtu anamdharau.

Heshima sio kitu cha Bure.

Huwezi heshimika Kama hujagharamia heshima husika.

Maisha ni bure lakini kuishi ni gharama.

Wanaopenda mambo ya bure hukosa heshima.

Moja ya sababu inayopelekea wanawake kudharaulika ni pamoja na kupenda vitu vya bure.

Hakuna aliyependa vya Bure akaheshimika.

Wanaume wengi WA siku hizi hawaheshimiki Kwa sababu nao wamejiingiza katika mkumbo wa bure.
Yaani uchukue mtoto wa watu bure, hakuna mahari wala Harusi, umzalishe Bure utegemee mwanamke atakuheshimu.

Wazazi hasa Wababa wapendao vya Bure nao huonja joto la jiwe.
Ulitekeleza mtoto, akalelewa na Mama yake, iwe Kwa Raha au Kwa shida. Alafu utegemee mtoto atakuheshimu. Thubutu! Hakunaga heshima ya bure.

Huna pesa, huna elimu, huna Mungu, huna lolote alafu unataka heshima.
Si utakuwa umechanganyikiwa wewe!!

Mungu anasema; ukiniheshimu nutakuheshimu.

Sasa huna lolote hata Kumheshimu Mungu umeshindwa huenda hiyo ndio ponapona yako.

Heshima inagharama.
Alafu kuna watu wanapenda kulazimisha usawa hapa Duniani Jambo ambalo kamwe halitatokea.

Utabaki kusema, kwani hatutakufa, ndio maneno ya watu waliodharauliwa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
 
Hapo kwenye kutokutoa mahari sijapenda, unamaanisha ningemtolea mahari huyu pasua kichwa ninayeishi nae ndo angeniheshimu?
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokupata mungu atakupa wepesi
 
Back
Top Bottom