Heko CCM: Wao wakifarakana, wewe kandamiza hapo hapo!

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,899
Hasira za nini ndugu zangu? Badala ya kupambana nao tumegeukiana sisi kwa sisi.

Majibu ya awali:

1. Mikataba 3 na wale ndugu, kwishney.
2. Konda boy ndani ya nyumba.

Na Bado!

Ama kweli tunapoendelea kujitafuta, mwana mikakati wao apewe sifa.

Hizo ndiyo siasa za kiutu uzima. Wao ni kutu zoom na kufanya kazi.

Ngoma ya watoto haikeshi!
 
Hii ngoma ya bandari haijaisha, wote wanaojielewa wanaendelea kupinga ule mkataba wa maigizo walioingia ili kutufunga midomo, haiwezekani kujenga nyumba nzuri juu ya msingi mbovu, huo ni utapeli wa mchana kweupe.

Mkataba hawajatuonesha, wanasema tu una hiki na kile kama vile sisi ni watoto wadogo tusiojua kusoma na kuandika, wamefeli, hawaaminiki tena, wale wote walioingia ule mkataba mpya wana mikono michafu, hivyo hawawezi kutudanganya wametuletea chakula kisafi.
 
Hii ngoma ya bandari haijaisha, wote wanaojielewa wanaendelea kupinga ule mkataba wa maigizo walioingia ili kutufunga midomo, haiwezekani kujenga nyumba nzuri juu ya msingi mbovu, huo ni utapeli wa mchana kweupe.

Mkataba hawajatuonesha, wanasema tu una hiki na kile kama vile sisi ni watoto wadogo tusiojua kusoma na kuandika, wamefeli, hawaaminiki tena, wale wote walioingia ule mkataba mpya wana mikono michafu.

Ngoja tupopoane mawe hadi tutoane macho kabisa kwanza tukigombea ustaa kwenye mapambano dhidi ya ma CCM. Haya ya bandari tutayarudia baadaye.
 
Back
Top Bottom