Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
HAMTAKI KUJIINGIZA KWENYE SIASA BASI ACHENI WALIOJIINGIZA WALE WAO NA WATOTO WAO
Na, Robert Heriel
Waacheni warithishane madaraka, waacheni wapeane vyeo. Mlitaka wafanyaje? Wao ni wanasiasa na watawala mlitaka wawape watoto wao nini kama sio mambo hayo.
Haiwezekani watu wahangaike na siasa kutwa kuchwa, miaka nenda Rudi ninyi mnawatazama tuu. Wengine Baba zao wamekufa, wengine wamefanywa vilema, wengine walionja joto la jiwe, alafu wakifanikiwa na kuanza Kula matunda Yao mnaanza kupiga makelele, come on motherfantashiru. Tuweni serious kidogo.
Hivi Kwa mfano mtu Kama Tundu Lisu, au kina mbowe, au kina Mdude Chadema na kambi Yao. Wachukue nchi alafu wakianza Kula matunda ya jasho lao na kuwarithisha watoto wao Madaraka au vyeo watokee watu wanapiga kelele kuwa wanajipendelea. Mlitaka wafanyaje?
Wakati wakipigana mliwaachia au mlikuwa nyumanyuma Kwa Hofu au wengine hamkuwa upande wao. Leo wamepata mnajifaraguza Kama ajuza asiye na tumaini. Pumbavu!
Kama unataka Madaraka au utawala ingia kwenye Siasa. Utakula vya Siasani, utawapa watoto matunda ya Siasa.
Lakini kama utajiingiza kwenye biashara utakula vya kwenye biashara na kuwarithisha watoto wako mambo ya biashara.
Kuna watu wanapenda vitu vya burebure.
Wengine watoe jasho alafu Yao Yale tuu. Upuuzi tuu!
Wana-CCM wataendelea kurithishana matunda ya Siasa Kwa sababu ndio haki Yao. Hakuna haja ya kulaumiana hapa.
Wakati unawaza Kwa nini viongozi wa nchi wanarithishana Madaraka na utawala jiulize Baba yako alikuwa anafanya nini hapo Kabla, isijekuwa Baba au Babu yako ndio Wale wenzao walipokuwa wakiitisha maandamano kupigania maslahi ya nchi au chama cha Siasa wao walikuwa nyumanyuma kama Mfuko wa suruali ya kabwela.
Jiulize hao Watoto wa viongozi wanaopewa vyeo na kurithishwa Madaraka Baba au Babu zao walifanya nini.
Hata hao CHADEMA au ACT au chama chochote kitakachoanzishwa watakaopigania Dola wakafanikiwa kupata hiyo Dola elewa watakaokula Mema ya nchi ni Wale wa Kule juu tuu.
Alafu mwisho ujiulize wewe unayohaki hiyo Kwa misingi ipi?
Umefanya nini upewe Cheo au Madaraka.
Sio utake kuvuna mahali usipopanda.
Kwenye Siasa kuna mambo hatari mno.
Kuna kupoteza maisha,
Kuna kujeruhiwa na kufanywa kilema,
Kuna kuwekwa Jela,
Kuna kufilisiwa,
Kuna kuvurugiwa familia,
Kuna kubakwa
Kuna kuharibiwa jina,
Sasa wewe upewe Cheo au Madaraka bila kutoa kafara fulani, uliona wapi mambo Kama hayo ndugu yangu.
Hata Daudi kabla hajawa Mfalme Ali-risk maisha yake Kwa Goliath, yaani ilikuwa Do or Die. Yaani pata potea.
Daudi alishanusurika mara kadhaa kuuawa na Mfalme Sauli, unafikiri Mpaka Daudi anakuwa Mfalme alipewa burebure kama pesa ahongwavyo Demu.
Hivyo Suleiman kurithishwa ufalme ni kutokana na jasho la Baba yake Daudi,
Ninachotaka kusema ni kuwa, hakuna mambo ya burebure hapa, Kama ulitaka mambo ya burebure muombe Mungu uzaliwe wakati mwingine mwanamke, tena hata ungezaliwa mwanamke lazima kuna mambo ulipie ndipo uyapate.
Wanasiasa, viongozi wa nchi, watawala endeleeni kula nchi kadiri muwezavyo, rithishane peaneni vyeo na Madaraka muwezavyo Hilo ndio Fungu Lenu. Msione haya Kwa kufanya hivyo. Ni Haki yenu. Hiyo ni halali yenu.
Kama kuna mtu anaona sio halali basi aingie kwenye Ligi au ringi na ninyi akishinda Fresh asiposhinda basi aache lawama.
Kila kazi inanamna yake ya kuifanya. Hivyo ndivyo hata kwenye Siasa zina namna yake.
Katika ngazi ya familia, unakuta Kijana wakati ana- hustle kutafuta maisha mazuri ndugu na marafiki wanakuwa mbali naye. Lakini akishapata tuu kelele ndio zinaanza,
Ooh! Anatumia pesa vibaya,
Anavaa nguo za gharama alafu hasaidii ndugu zake,
Ananunua magari na majumba makubwa wakati ndugu zake ni choka mbaya,
Anasomesha watoto wake shule za gharama ilhali watoto wa ndugu zake wanashindwa kulipa Ada za Shule za bei nafuu.
Oooh! Anampendelea mkewe alafu site ndugu zake ametusahau.
Hivi hiyo ni Akili Kweli. Acheni uzombi!
Ukitaka kitu kizuri fanya mwenyewe, kitafute mwenyewe sio usubiri wengine wakutafutie au wakutanyie. Huo ni upuuzi.
Au unakuta mtu kuanzisha Kampuni yake anaajiri ndugu zake au kabila lake alafu unasikia wapuuzi wanapiga kelele oooh! Wanaukabila, oooh! Wanaubaguzi! Oooh! Hivi ninyi Mbuzi meee mtakuwa na akili Lini?
Kwa nini nanyi msianzishe Kampuni au biashara zenu ili mfanye kama mnavyopenda?
Mnachojua ni kupangia watu chakufanya huku mkishindwa kujipangia wenyewe chakufanya. Acheni upuuzi.
Yaani mtu aache kuajiri ndugu yake akuajiri wewe ili asionekane ati ni mkabila au mbaguzi, labda awe hamnazo. Mambo ya hivyo wanafanyaga watu wajinga wasiojielewa, wanaopenda sifa za kijinga.
Ninachotaka kusema ni kuwa; Kula mtu awajibike Kwa kile anachokitaka katika maisha yake. Ukiona changamoto pambana sio uanze kulalamika
Kanuni kuu inasema; Usitamani Mali ya jirani yako.
Kumaanisha usiwe na kijicho, wivu mbaya.
Kama wanarithishana nawe fanya kazi upate cha kurithisha watoto wako. Hakuna atakayekuonea wivu.
Kama unapenda Madaraka au utawala kanuni za kiulimwengu zipo wazi Kabisa. Weka mikakati, pambana kufa na kupona upate hayo Madaraka.
Sio umuombe mwenye Madaraka au utawala akupe Madaraka au utawala wake. Tumia hata akili, Hilo Jambo haliwezekaniki.
Usituletee mambo ya umama hapa.
Na lazima ujue kuwa kwenye mapambano yoyote hasa ya Kisiasa lolote linaweza kutokea. Hivyo ujipange haswa sio ujipange kulialia kama Mbuzi Bali jipange haswa
Taikon nimemaliza mwenye swali anaweza kuuliza.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam