Askari Kanzu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 4,598
- 1,233
Bab al-Aziziya kwishnehi
Lililokuwa hekalu/Ikulu ya Kanali Gaddafi, Bab al Aziziya, limebomolewa rasmi leo Jumapili 16 Oktoba kwa kutumia mabuldoza, nyundo na sepetu. Kwa mujibu wa kongozi mmoja wapo wa serikali ya mpito TNC, "wakati muafaka umefika wa kuanza kubomoa ishara zote za udikteta wa utawala wa Gaddafi". Mtandao wa BBC umemnukuu Afisa Mwandamizi wa jeshi la serikali ya mpito Ahmad Ghargory akisema kuwa eneo la Bab al-Aziziya litageuzwa kuwa hifadhi ya umma
Hadi sasa sehemu ya uwani ya hekalu hilo imekwisha badilishwa kuwa soko la kila wiki ambapo raia kutoka Tripoli na vitongoji vyake huuza bidhaa zao. Sehemu hiyo hapo awali, wakati wa utawala wa Gaddafi, ilitumika kama uwanja wa kuwapokea wageni wa heshima na ndipo mahala Gaddafi alikita hema lake.
Bab al-Aziziya ni jengo mojawapo ambalo lililengwa na mabomu ya NATO karibuni kila siku wakati NATO waliposhambulia Tripoli kwa nia ya kumng'oa Gaddafi toka madarakani.
Zifuatazo ni baadhi ya picha zilizopigwa wakati zoezi hilo la kubomoa Bab al-Aziziya likiendelea. (Hisani ya Getty Images)

Last edited by a moderator: