Heche atangaza maandamano Dar kesho, Polisi yapiga marufuku!

Anapoteza tu muda! akaandamane tu huko vijijini, siyo hapa dar. Huku watu wana ufahamu na wanajitambua. aje kwa staili nyingine!

Mlitabiri kuwa Lema angetoka juzi mahakamni asingepata watu NMC. Matokeo yake pamoja na kunyimwa dhamana uwanja ulifurika watu, na angetoka NMC kusingetosha kabisa.
Inabidi mkubali kuwa watu wamechoka na utawala mbovu wa Kikwete na chama chake cha majambazi. siyo vijijini wala mijini. kote pakitangazwa maandamano watu wanaandamana.
 
Hilo ni dokezo au taarifa?
Taarifa inayohitaji kufanyiwa kazi inakuwaje fupi na at such a close range?
Jaribuni kuwa more strategic and specific maana hata well wishers and supporters mtaanza kuwaboa kwa kutoeleweka kwenu.
 
John Heche inabidi aje atueleze vizuri maana haya mambo ya kuwekana juu juu tunaweza kuacha kwenda kazini watu wakala mishahara yetu!! Toeni taarifa vizuri wakuu ili tujipange, tuandae mabango kabisa.
 
Tatizo hawa CDM hawapo strategically.. hawajui wanachokitaka!
kila siku wanatuacha dilema, Lengo la lema la kujipeleka mahakaman hatujui lilikuwa nini, wameshaenda tena kumuombea dhamana wenyewe, sasa hivi tena wanataka kuandamana dar, huku tunaona Zitto anagombana na NCCR mageuzi, mara gazeti ya mwanahalisi! tunaambiwa tena Slaa anatembea na bastola mikutanoni, mara tena mbowe kapotea, alikojificha hapajulikani!
Haya ni matukio machache tu ndani ya muda mfupi yanayokihusu hiki chama ambacho bado ni kichanga sana. wangejipanga vizuri.

mkuu sababu ya LEMA kugoma thamana ni kuwa kila alipokuwa anatoka kwenye kes mahakaman wananch waliokua wamejitokeza kusikiliza kes yake wanamfuata na kuongozana nae mpaka ofisin kwake matokeo yake polic wanamkamata tena na kumfungulia kesi nyingine kuwa amefanya maandamano.Huku maafisa polis na wanausalama wakimfuata na kumuhoji mara kwa mara na kushindwa kuwa huru kufanya shughuli zake na kuwatumikia wananch wake.
Ndiyo mana akaamua akakae gerezan kuliko kukaa uraian ambako hawi huru kwa kufuatwa fuatwa na maofisa polis na usalama.

Jingine anadai kuwa maafisa hao wamekuwa wanamtishia mda mrefu juu ya kumfunga.Ili kumkata makali yake ya upinzan ndiyo mana akaamua agomee thamana ilikuwaonyesha kuwa jera kwake cyo ki2 cha kumtishia .Mkubwa hatishiwi nyau.

Hata kama LEMA alikataa thamana cku hyo lkn bado zamana yake ilikuwa waz. je? kwan kukataa zamana ni kosa kisheria na kama alikataa kwa usalama wake je?

Sawa LEMA alikuwa na kosa kukataa zamana je hakimu naye alikuwa na haki kukataa kusain hati ya kutolewa kwa LEMA??Au naye alitoa uamuz wa mawazo mgando??

Hili swala kwa upande wangu naliona kama limekaa kisiasa na kama lingeendeshwa kisheria lisingefikia hapa lilipo na kama mambo ya kisheria yatatolewa hukum na kutatuliwa kisiasa hakika hakuna upande utakao kubali na kila suruhu itolewayo na mahakama au vyombo vya usalama.
 
Hii ni Kimara mpaka Magogoni. Kisha mtu mzima anakimbilia Sirte (Bagamoyo)

Bila Lema? bila Slaa na silaha yake? bila Mbowe (maana nasikia kaingia mitini), bila Zitto (maana nasikia ana soo na Mbowe), bila Lissu maana nasikia hataki mambo yasiokuwa ya kisheria.
 
Bila Lema? bila Slaa na silaha yake? bila Mbowe (maana nasikia kaingia mitini), bila Zitto (maana nasikia ana soo na Mbowe), bila Lissu maana nasikia hataki mambo yasiokuwa ya kisheria.
Mzee kaamua awe anatembea na gun.. naona atawakuwa anawaogopa sana vijana wa Arusha!
 
Anapoteza tu muda! akaandamane tu huko vijijini, siyo hapa dar. Huku watu wana ufahamu na wanajitambua. aje kwa staili nyingine!
endelea kujidanganya kwamba maandamano ni vijijini tu, Eleza kwa nini pamoja na wizi wenu wa kura CCM haikufanya vizuri Dar hasa ubungo, Kawe na Segerea? Hamna jipya magamba's

mnaishi kwa kutisha wananchi badala ya kuwatatulia matatizo yao - huko ndiko kuishiwa kisiasa. mbinu hii ni ya kizamani sana huwa haina muda ina expire.
 
Tanzania nzima watu wanaandaa maandamano wamechoka kunyanyaswa. Mwisho wa siku haitakuwa chadema bali peoples power!
 
Kibali Chapo Polisi Tayariiiii...??? maana hapo wataanza sababu ya Al shaabab...Tanzania siasa kweli na kazi za polisi ndiyo hapo zinaponimalizaga
 
Huyo jamaa na wenzake hao wana FUNZA huko juu kichwani na huko chini, hua wanawawasha ndio maana hawawezi kosekana kwenye ku-crash thread zinazozungumzia CDM, wala hakuna haja ya kujaribu kuwaelewesha lolote maana ni kazi bure, nia zao ni ku-divert concentration ya mambo ya maana yanayozungumziwa always.
Wahurumieni hawa wako kazini, Nape anawalipa kutokana na idadi ya comments wanazochangia kwa siku. Wasipotoa upupu hapa jamvini kwa siku watoto watakufa njaa.
 
Wana JF

Muda mfupi uliopita makao makuu CDM , Mwenyekiti wa vijana Taifa John Heche Suguta amengaza maandamano makubwa Dar es Salaam kesho asubuhi kuanzia eneo la kimara.

Yeye pamoja na makamanda wengine walikuwa na mkutuna na wanacha wa CDM makao makuu.
Kweli ni kimue mue nchi mzima, mpaka maghamba waelewe kinacho endelea!!!!!!!!!
 
ccm hata wajigeuze vip mtaji wao wa kura za ubwete walizo kuwa wanazitegemea unazid poromoka.
Mtaji mkubwa wa kura ccm ni wazee na maskin wanao wadanganya kwa t-shirt,kofia na kanga bila kusahau pombe za kienyeji lkn makund hayo nayo yamestuka kwa sasa na kikubwa kilicho wastua ni hali ngum ya maisha na ufujaji wa raslimal na ufisad unao fanywa na magamba.
Mim naamin kwa maisha ya sasa na hali jinsi ilivyo ikatokea kuna sehem kunamgombea wa ccm peke yake halafu upand wa 2 liwekwe jiwe haitakuwa ajabu jiwe likiibuka na kura nying.

cdm nao na his kama wanashindwa kucheza na timing.kama maandaman wanayoyafanya mara kwa mara yanaweza kuwapunguzia wafuas na kupoteza iman kwa raia na kuonekana wapenda fujo na nikund la vurugu.
ni kwel idad kubwa sana ya wananch wanataka kuona mabadiliko yanafanyika lkn viongoz wa cdm wanashindwa kusoma nyakati.
kama swala la LEMA haiwezi ikawa ndiyo hoja kuu ya kuitisha maandaman na kuwashawish raia na wafuas wake wa mikoa mbali mbal kuandamana juu yake wakat kuna raia wangine hata huyo lema hawamjui kbs.
maandaman kwaajil ya lema yatawapotezea timing kwa kuwa mwenyew alikataa zamana.
wangetafuta hoja yenye mashiko kwa taifa ndiyo wahamasishe maandaman nch nzima.
 
tatizo hawa cdm hawapo strategically.. Hawajui wanachokitaka!
Kila siku wanatuacha dilema, lengo la lema la kujipeleka mahakaman hatujui lilikuwa nini, wameshaenda tena kumuombea dhamana wenyewe, sasa hivi tena wanataka kuandamana dar, huku tunaona zitto anagombana na nccr mageuzi, mara gazeti ya mwanahalisi! Tunaambiwa tena slaa anatembea na bastola mikutanoni, mara tena mbowe kapotea, alikojificha hapajulikani!
Haya ni matukio machache tu ndani ya muda mfupi yanayokihusu hiki chama ambacho bado ni kichanga sana. Wangejipanga vizuri.
kwa hiyo haya yanakusumbua mno kiasi kwamba huna raha moyoni pole ndg
 
Back
Top Bottom