Heche atangaza maandamano Dar kesho, Polisi yapiga marufuku!

...go go go Makamanda wetu, haki haigawiwi bure na haielekei kugawiwa bure na mabaradhuli hawa wa CCM. Tunaiunga mkono kwa nguvu zote kauli ya Mh. Freeman Mbowe kwamba tutaonyesha waziwazi na kwa nguvu zetu zote kutokukubaliana na udhalimu, uonevu na manyanyaso makubwa yanayofanywa na Utawala wa kidhalimu(kupitia Polisi) kwa muda mrefu. Tuliokuwa nje ya ulingo tunaingia ulingoni rasmi kuongeza nguvu, tuliokuwa mbali tunarudi kuhakikisha mabadiliko yatatokea mapema itakavyowezekana. Tunajua na tunaelewa kwa kina kwamba kuna uwezekano mkubwa wa watu kuumia na pengine hata kupoteza maisha, hiyo ni sehemu ya kawaida kwa wapigania haki na uhuru popote duniani. Tunajua wazi kwamba mabaradhuli wakubwa wa nchi hii hawatokubali kirahisi hata kidogo kuachia nafasi maana wanayajua matokeo yake, tusife mioyo maana sisi ni wengi sana, tunasimamia ukweli na Mungu yu upande wetu daima..!
 
Hili la CCM nao kuomba kuandamana kisha kuzuiwa halafu wakashukuru ni mbinu ya ku-neutralize kilichotokea Arusha, CCM walizuiwa kufanya maandamano Arusha lakini walifanya na Polisi waliingiza mikia matakoni maana ni mabosi wao walikuwa wanashindana. Juzi CDM walipokesha pale NMC Polisi wakawavamia alfajiri, hii ni ishara ya woga kwa Polisi kisha wao wanaripoti ati Viongozi wa Chadema walijificha na wengine walikimbia. Polisi wana vifaa vingi vya kazi, kwanini wasiwakimbize tujue waliwakimbiza wakawakosa? kwanini tusione Polisi wakifukuza gari zao ili na sisi tujue cha kufanya?

Tumeshawaona Makamanda wa Polisi wana wasiwasi mkubwa, hata kauli zao ukiwaangalia na kuwasikiliza zinaonyesha woga mkubwa. Wanaujua ukweli uko wapi na wanaelewa wazi wanafanya unyanyasaji kwahiyo hali inapokuwa tete wanatatizika sana kuhusu lifuatalo.

Askari wadogo wako kwenye matatizo makubwa maana sasa hawalali wakati hata huko makwao chakula hakuna, nyumba zao zinavuja na kwenye joto nyumba zina joto kali kupita kiasi maana ni nyumba za makopo, hali zao kimaisha ni ngumu sana isipokuwa tu wale wala rushwa wakubwa, upande wa pili Makamanda wao wanaokaa maofisini na kuamrisha wenzao kwenda kupambana wanatangaza manyanyaso makubwa huku wakielewa wazi wanaowaamrisha kwenda kunyanyasa wananchi nao wamepanga mitaani kwetu na wake zao huomba msaada kwetu wanapotaka kwenda kujifungua.
 
Askari wa ngazi za chini nao wameichoka c.c.m na hata hawaipendi hata kidogo, wote ni chadema, nina ishi nao uku mtaani, nakaa nao vijiweni, nawajua. Hao wanapewa order na wakubwa zao kina Chagonj'a wanakuwa hawana jinsi zaidi ya kutekeleza ila wapate ugali. Wanasema sisi tulianzishe tu mwisho wa siku watakuwa upande wetu kwa sababu nao wanaathirika na huu mfumo m'bovu wa magamba, tuliona tunisia, misri, libya, polisi waliua watu mwisho wakasema basi.
Hakuna ukombozi bila damu kumwagika ndugu zangu.

Tusonge mbele Polisi wetu wana hali mbaya sana na hawawezi hata kidogo kufanya la ajabu maana tunakaa nao mitaani na wake zao na watoto wao tunacheza nao, ikiwa mbaya ni rahisi sana kuaza na familia zao kwahiyo nina hakika watatumia akili zao za kuzaliwa. Makamanda wao wanakaa kwenye nyumba nzuri wakiamka asubuhi wanaenda tu maofisini na kuamrisha huku wakiwa na Radio Call mikononi. Tunawashauri Polisi wadogo kutumia akili zao kuamua wanapokuwa kwenye uwanja wa mapambano, kwa sasa hakuna uwezekano wa kugeuka nyuma maana ukweli ni kwamba CCM hawana mpango wowote wa kugeuka nyuma. Nguvu ya umma iingie kazini, sina haja ya kusema sana maana mifano imeonekana sehemu nyingi duniani.
 
Acha kwanza mkione cha moto. wakati NCCR na baadaye CUF wakipata kipondo kwa CCM nyinyi mlichekelea. sasa zamu yeu hapo mtakapokuwa na akili ndo mtajua nini maana ya kushirikiana. sasa mmebaki peke yenu huko Arusha. siku ingine msijitenge kwenye harakati zenye masilahi kwa taifa. Yaani hapa ninafuraha mpaka basi. Siwapendi ccm na wala siwafagilii chadema kwa sababu wanajiona weo ndo wao.

Duu! Kwelı JF ımevamıwa hadı kıngwendu naye anamwaga uhalo wake humu??!
We kachekeshe watoto kwenye TV Jamvını sıo sıze yako.
Humu tunajadılı great thıngs usıng hıgh thınkıng capacıty.
Nyambaaf!
 
Back
Top Bottom