Heche atangaza maandamano Dar kesho, Polisi yapiga marufuku!

Bila Lema? bila Slaa na silaha yake? bila Mbowe (maana nasikia kaingia mitini), bila Zitto (maana nasikia ana soo na Mbowe), bila Lissu maana nasikia hataki mambo yasiokuwa ya kisheria.
Mtasema saana mwaka huu sijui kama mtachomoa, mtanange wa CDM ni noma saana!!!!!!!! Mpaka mkae darasani kujifunza mbinu mpya sio kukurupuka mnazidi kupoteza dira!!!!!Mnaingia vizuri kwenye mitego ya wakombozi!!!!!
 
Mtujuze dhima nzima ya maandamano hayo ndo itakuwa rahisi kupata watu wengi naona mtoa taarifa alikuwa na haraka ya kupost mada ili aonekane kaanzisha mada kitu ambacho mods wanakazi kubwa nadhani thread kama hazina details za kutosha ziwe zinawekwa kando ili watoa mada wajifunze kutoa mada kwa umakini na kwa manufaa ya wanajamvi wote.

Maandamano ni haki ya kikatiba sema hapa kwetu siasa zimeingilia uhuru wa kisheria na hivyo nchi inaongozwa bila kufuata misingi na kanuni za sheria zinasema nin. Wajibu wa polisi ni kutoa ulinzi na sio kutoa kibali cha maandamano. Hili wanalijua na ushahid upo wazi makusanyiko ya watu aidha mikutano ama maandamano yanayofanywa na chadema yamekuwa na amani bila uwepo na polisi ila yanakosa aman pale polisi wanapopokea amri za kisiasa na kuzitekeleza bila kujua sheria ni msumeno na ipo siku itawahukumu hata wao kwa uovu wanaotutendea sasa hivi. Warejee Tunisia, Misri na Libya ni mifano mizuri ama majirani zetu wa Rwanda jinsi sheria inavyowarud viongozi waliokuwa wanaikwepesha kwa misingi ya kuwaonea wananchi na kuwadhulumu.
 
ninavyojua mimi cdm haina nguvu dar; kwa hiyo si dhani kama kutakuwa na uumgwaji mkono wowote ule kutoka kwa wananchi! Hata hivyo cdm ndio imeshasambaratika hivyo, kwa sababu slaa, mbowe, lissu, lema, wataishia jela; zitto atahamia ccm au nccr hivi punde, waliobaki ni dhaifu hawana uwezo wa kukifanya chama ''kisimame imara''

poleni chadema
 
Kwa taarifa yenu ni kuwa maandamano hayo sio ya Dar pekee bali yameombewa vibali kila wilaya ya nchi hii tangu jana , na kama kuna watu wanandoto kuwa CDM Dar haina nguvu wanapaswa kuiona CDM kesho dar .

kuna taarifa za tamko la Kamishina Chagonja ambalo atalitoa punde kuhusiana na mikutano na maandamano ya CDM kesho so ntawajuza likishamalizika kuchapwa ........
 
,.,.. Lengo la lema la kujipeleka mahakaman hatujui lilikuwa nini...


Haya ni matukio machache tu ndani ya muda mfupi yanayokihusu hiki chama ambacho bado ni kichanga sana. wangejipanga vizuri.



Unaonekana hujui yanayoendelea ndani ya nchi.

Lema hakujipeleka mahakamani. Alikamatwa na kushtakiwa. Halafu hufahamu taratibu za mahakamani. Kwani ukienda mahakamani unapelekwa magereza!? Amka mkuu!

Halafu cdm ina miaka karibu ishirini sasa ikifanya siasa humu nchini. Ndio chama cha upinzani chenye wabunge wengi nchini. Tena kutoka katika kanda zote za nchi. Ndio kinaongoza kambi ya upinzani bungeni. Wewe unaona ni kichanga!? Lazima ubongo wako unashida.
 
Wahurumieni hawa wako kazini, Nape anawalipa kutokana na idadi ya comments wanazochangia kwa siku. Wasipotoa upupu hapa jamvini kwa siku watoto watakufa njaa.
Mbona we mpagazi wa Lema au ndo Nyani haoni kundule?
 
Kibali Chapo Polisi Tayariiiii...??? maana hapo wataanza sababu ya Al shaabab...Tanzania siasa kweli na kazi za polisi ndiyo hapo zinaponimalizaga

Wamesema hawataki kibali cha polisi washawapa taarifa inatosha mwendo mdundo nasikia harufu ya ukombozi
 
Muishie Ubungo. Zaidi mkunje Sam Nujoma, mpite mwenge hadi sinza kwa walevi hadi Shekilango kisha mrudi Kimara au Mkitoka mwenge muelekee Kawe. Mkiingia mjini wafuasi wenu watakuwa kwenye keyboards na kuwachungulieni madirishani. Mtabaki kituko tu.
 
Anapoteza tu muda! akaandamane tu huko vijijini, siyo hapa dar. Huku watu wana ufahamu na wanajitambua. aje kwa staili nyingine!

Naunga mkono, twendeni vijijini tukafanye kolabo la kulima na kununua mazao.
 
HEbu wekeni chini upumbavu wote na sasa kapigeni kazi bungeni jamani bado tunakiamini chama
hawa CCM ni kuwatupia mambomu ndani ya bunge huku nje wanamiliki kila kitu sasa ni mda wa kujipanga hapa mjini
 
Hii ni Kimara mpaka Magogoni. Kisha mtu mzima anakimbilia Sirte (Bagamoyo)


Ha ha ha ha nilitaka niku gongee "LIKE " lakini sizioni sijui kwangu tu..akigoma kutoka magogoni tukimkamata tunamtia jiti panchonyo kama mzee wa Bengazi
 
CDM uwa hatuna maandamano ya kuvunja amani..wanao vunja amani ni CCM na vyombo vya dola...

Haya, nawatakia maandalizi mema. Lakini waambie viongozi wenu waache kufanya upinzani wa wenyewe kwa wenyewe.
 
Anapoteza tu muda! akaandamane tu huko vijijini, siyo hapa dar. Huku watu wana ufahamu na wanajitambua. aje kwa staili nyingine!

Unafikiri wote wanawaza kwa masburi kama wewe. Wanajitambua, we subiri uone maana maisha yanawatandika kweli Watanzania hasa wale wa Uswahili wanaopenda kuchagua CCM kwa kishindo.

Na watakoma, Natamani Sukari ifike shilingi 5,000, chai inyweke Ikulu tu na kwa maafisa wa Serikali na CCM na vibaraka kama wewe REJAO
 
Asante John Heche naunga mkono maandamano yafanyike Dar walau uku Arusha tupumzike tumechoka kila siku Arusha kwani Dar,Mwanza,Mbeya,Dodoma,Kigoma si Tanzania.



Upumzike kitu gani? Kwani ulishawahi kuandamana wewe!? Huko nduruma unapokaa hata mabomu huyasikii halafu unasema umechoka! Unachekesha sana ngongo.
 
Unafikiri wote wanawaza kwa masburi kama wewe. Wanajitambua, we subiri uone maana maisha yanawatandika kweli Watanzania hasa wale wa Uswahili wanaopenda kuchagua CCM kwa kishindo.
Na watakoma, Natamani Sukari ifike shilingi 5,000, chai inyweke Ikulu tu na kwa maafisa wa Serikali na CCM na vibaraka kama wewe REJAO
kila mahali CCM inashinda kwa kishindo...Chadema wataendelea tu kuwa looserz! karibu CCM tuijenge nchi yetu..ondoka huko kwenye vurugu

Mawazo yako ndiyo yapo huko...yaelekea unatumika sana

Naunga mkono, twendeni vijijini tukafanye kolabo la kulima na kununua mazao.
Angalau hapa umeongea la maana! wenzako wanawaza tu kuandamana

Unaonekana hujui yanayoendelea ndani ya nchi.
Lema hakujipeleka mahakamani. Alikamatwa na kushtakiwa. Halafu hufahamu taratibu za mahakamani. Kwani ukienda mahakamani unapelekwa magereza!? Amka mkuu!

Halafu cdm ina miaka karibu ishirini sasa ikifanya siasa humu nchini. Ndio chama cha upinzani chenye wabunge wengi nchini. Tena kutoka katika kanda zote za nchi. Ndio kinaongoza kambi ya upinzani bungeni. Wewe unaona ni kichanga!? Lazima ubongo wako unashida.
Yeah, ujinga unaondelea nauona sana, naona ujinga CDM wanaoufanya wa kujipeleka wenyewe magerezani

Unabisha Rejao kuwa wewe hulipwi na maghambas, sema unalipwa nanani basi???????
Nalipwa na wewe...nikiona haitoshi nitaomba incriment

kujitambua wewe!? Bado sana!
Mbowe na Zitto wakijitambua wao ni akina nani na mimi ndio nitajitambua
 
Back
Top Bottom