Hebu ona haya ya ndugu JK huko aliko sasa

Na kama tunae basi ni kwa matakwa ya wachache. Kwa jinsi hali ilivyo sijui kama tutatoboa 2015. Angalia mfimuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi
 
Kama unajikubali upo poor in mind.. kwa nini umlaumu raisi?
Tusipende kulaumu kila achofanya raisi, tukumbuke anafanya kwa ajili yetu.

Rejao, maandamano alimaanisha hawezi kutoka kwenye lindi la umasikini wa kimawazo wa JK, maana na yeye ni M-TZ!! Aibu au fahari anayovuna JK akiwa nje, huwa wanatoa kwa wote kama wa-TZ na si JK pekee!! Well this is the time na yeye kupokea part of blames zinazosababishwa na failure ya uongozi katika government. Kubali au kataa, tuna matatizo mengi na suprisingly ni kwa sababu tu ya ukosefu wa busara!!

Binafsi huwa nachukia jinsi JK anavyotembeza bakuli...
 
Hivi ile siasa ya Ujamaa na KUJITEGEMEA iliishia wapi?? Nilifikiri wameachana na Ujamaa lakini bado tunataka Tujitegemee. Kwa mtizamo wa sasa inaelekea TZ inataka kuwa nchi TEGEMEZI!!
 
Tatizo sio kutafuta wawekezaji tatizo chi imejipanga vipi kupokea Hal wawekezaji. Nchi nyingi zilizoendelea hapa duniani zina uwekazaji mwingi tok a kwa makampuni makubwa. Wao wanfanya na kujipanga wakati wa ku negotiate deal, wako smart na very organised . Wanapanga regulatory structure nzuri.

niko hap Perth na niliweza kuudhulia mkutano huo. Wa Naigeria wameleta delegate ya wafanyabiashara 180 na maafisa pamoja na watu wa usalama 20, wako very organized Kilauea state imekuja na wafanyabiashara wakiwa wameweka vita vyao kwenye maandishi na mahitaji Yao yak very open. Serikali Yao ina aim kuipiku South Africa in 2030 kiuchumi.
watanzania tumekuja wafanyabiashara wane na maafisa ya serikali zaikai ya ishirini. Hatuko organized . Hatujui nini tunataka wenzetu wameendaa investment attraction books na wamevidistribute kwa watt wote , watz wamekuja na copy chache na nyingi zimegawiwa kwa watz wenyewe.
Unapochaguwa wasaidizi wabovu na wewe mwenyewe unakuwa mbovu
 
Gaddaffi alipoingia madarakani aliwaambia wawekezaji wa kigeni walikuwa wanachota mafuta kule Libya kuwa lazima mafuta hayo yawanufaishe watu wa Libya kwa kiasi kikubwa. Wawekezaji walijifanya kumtishia kuwa kama ni hivyo basi wataacha hiyo biashara ya kuchota mafuta kabisa na watu wa Libya wakose kabisa walichokuwa wanapata kutoka wa wawekezaji hao. Gaddaffi aliwaambia kuwa watu Libya wamekaa hapa miaka zaidi ya 5000 bila hicho kipato kidogo walichokuwa wanapata kutokana na mafuta sasa kungekuwa na shida gani kama wawekezaji wangeacha kuchota haya mafuta. Wawekezaji baada ya kuona msimamo wa Gaddaffi ilibidi tu wakubaliane naye.

Kutokana na huo msimamo wa Gaddaffi Libya ilikuwa ni nchi ya kwanza katika nchi zilizokuwa zina mafuta kwa wakati huo kuanza kufaidi matunda ya rasilimali yake ya mafuta. Baada ya hapa nchi nyingine ziliiga mikataba ya Libya.

Kikwete anatakiwa kufanya hivyo. Hakuna kuwabembeleza wawekezaji. Wao wamekuja na mitambo lakini nchi masikini ndizo zenye rasilimali.

Sasa hapa inakuwa kama vile mtu anamefamiwa na vibaka ambao wanataka kuchukua pesa zote mfukoni. Huyu mtu anageuka tena kuwaomba vibaka wamwachie angalua hata hela ya nauli ya daladala.
 
Tatizo sio kutafuta wawekezaji tatizo chi imejipanga vipi kupokea Hal wawekezaji. Nchi nyingi zilizoendelea hapa duniani zina uwekazaji mwingi tok a kwa makampuni makubwa. Wao wanfanya na kujipanga wakati wa ku negotiate deal, wako smart na very organised . Wanapanga regulatory structure nzuri..........Hatuko organized . Hatujui nini tunataka ...........
Unapochaguwa wasaidizi wabovu na wewe mwenyewe unakuwa mbovu

Very well Said!!
 
From ICHIKAELI MARO, Perth, Australia, 26th October 2011 Daily News

President Jakaya Kikwete ( left) confers with the Director of Commonwealth Business Forum Dr Mohan Kaul in Perth, Australia on Tuesday, ahead of the club’s Heads of Government Meeting which starts on Friday.( Photo by Fred Maro)
PRESIDENT Jakaya Kikwete said here on Wednesday that foreign investors in Africa should plough back part of their gains to benefit the local communities.
He told the Secretary General of the Commonwealth Business Council, Dr Mohan Kaul, that proceeds from foreign investment should help efforts to improve food security and creation of decent employment in Africa.
Dr Kaul was briefing Mr Kikwete on the Commonwealth Business Forum, a side event, which the president is expected to address on Friday ahead of the Club summit opening on Friday.
President Kikwete said it was important for the Commonwealth to support the poorest member nations in reducing poverty in the same way it was propping up democracy, good governance and rule of law.
“The major obligation of Commonweath is to assist the poorest nations within the Club, especially those in Africa, to deal with the challenges of climate change (and poverty alleviation.)”
The president said such intervention would stimulate creation of wealth, reduce unemployment and promote equitable distribution of wealth in poor nations, which form majority of Commonwealth members.
Meanwhile, President Kikwete held discussions with the Executive Vice-President of Shell Oil Company, Mr Guy Outen.
They discussed prospect of Shell investing in offshore oil and natural gas prospecting in Tanzania.

Mie huwa nashangazwa sana na uwezo wa JF members humu ndani, hii forum ndugu zanguni inazidi kudharaulika kila kukicha inasubiria kufa tu. Hapo rais alichosema kibaya kipi ? tatizo lenu ni wachambuzi juu juu badala ya wachambuzi kina !
 
Kikwete bana, hajifunzi; habadiliki! Eti wazungu wabembelezwe kusaidia nchi maskini, kutokana na utajiri wanaovuna ktk investment zao. Tunashindwa kuweka mikataba mizuri tunabaki kuwapigia magoti ili watujengee vyoo! Aibu!
huyu naye akili kama za mbuni kuchomeka kichwa mchangani akihisi amejificha. Wakati wa campain alisema cha kwanza atakachofanya ni ku review mikataba. Alivyoingia madarakani akawa wa kwanza kumtuma karamagi kusaini mkataba wa buzwagi. Lazima masaburi yanatumika kutoa mawazo
 
Yaani pamoja na kuitengeneza vizuri hiyo habari imetoka hivyo. Sijui ingeachiliwa kavu kavu bila ya kupambwa na kuhaririwa ingekuwaje?
 
Hivi ile siasa ya Ujamaa na KUJITEGEMEA iliishia wapi?? Nilifikiri wameachana na Ujamaa lakini bado tunataka Tujitegemee. Kwa mtizamo wa sasa inaelekea TZ inataka kuwa nchi TEGEMEZI!!

No, ni kwamba TZ tunatataka tutoke kuwa Tegemezi na kuwa nchi ambayo inaweza ikajiamulia mustakhabali wake wenyewe badala ya kusubiri huruma za wafadhili.

Tangu tupate Uhuru na mpaka leo, nchi yetu imekuwa tegemezi, ikitegemea fadhila za mataifa mengine ili kufanya lolote la maana. Kitu pekee ambacho budget ya serikali yetu imekuwa ikiwezesha ni ulipaji wa mafao ya watumishi wa umma, ununuzi wa stationery na uendeshaji wa magari aina ya STK Toyota VX na GX.

Ni juzi tu ndiyo tulianza kujaribu kujenga barabara na pesa zetu wenyewe. Miradi yooooote ya umeme ni ya misaada. Airport zoooote ni misaaaada. Yaani haijalishi, wewe katika mizunguko yako ukiona kitu chochote cha maana ujue kuwa ni msaada kutoka kwa mataifa fadili.

Namna pekee ya kuondokana na hii hali ni kwa uchumi wa TZ kukua kwa kasi kubwa, ili hata kodi inayopatikana kutokana na shughuli za uchumi, basi iweze kupanda. Lakini unatakiwa vile vile kuelewa kuwa ukusanyaji wa kodi kubwa siyo dawa ya kila kitu. Actually, unaweza ukakusanya kodi kubwa sana lakini zikaishia kwenye ununuzi wa ma STK makubwa zaidi na mengi zaidi, ili kufikia lenga la STK moja kwa kila mtumishi wa serikali.

Hapana, ukuwaji wa uchumi utasaidia mwananchi mmoja mmoja kwa kufungua fursa za ajira na za biashara. Ukimuajiri mtu, unampa uhuru na uwezo wa kujipangia mustakhabali wa maisha yake na watu wake. Huyu mtu hawezi akajali kuwa huu mradi ni wa Serikali, SU, Muhindi au Mzungu. Watu wanaotaka kila kitu kiwe cha SU au Serikali nadhani ni watu ambao hawajui wenzao wasio na ajira wanapitia ugumu gani.

Ni kwa sababu hiyo ambapo ninaona jitihada za Rais wetu za kuleta wawekezaji ni lazima ziungwe mkono. Mimi hata ningependa itungwe sheria kuwa mtu yeyote atayehujumu mwekezaji, achukuliwe kama muhujumu wa uchumi.
 
bado sijaona Jk kakosea wapi labda tu kwa sababu wakosoaji wake hawawezi kukaa kimya lakini pia hawawezi kumsifia hata kwa zuri atakalokuwa amefanya
Akiwa hapa nyumbani anasema tumejaribu tumeweza........anasema chakula kipo, maghala ya serikali yamejaa chakula cha kutosha...
Akienda mje anasema ...helpe us to improve food security.........my bad!!
 
Mie huwa nashangazwa sana na uwezo wa JF members humu ndani, hii forum ndugu zanguni inazidi kudharaulika kila kukicha inasubiria kufa tu. Hapo rais alichosema kibaya kipi ? tatizo lenu ni wachambuzi juu juu badala ya wachambuzi kina !
drunk-people-3-400x282.jpg
 
Tumeshindwa kuona faida ya Dhahabu halafu tunawaita maharamia ya oil and gas ? hawa hawana mchezo ukitaka kuwabana wanakukodishia Nato,kizazi hichi dhahabu itatutosha oil/gas tuwaachie kizazi cha wanetu.

Kazi kulia lia tu. Yeye alichosema ni kwamba lazima kuwe na reciprocity katika kuvuna rasilimali na kwa taarifa yenu rasilimali hizo haziwezi kuleta maendeleo kwa kuendelea kuwa ardhini. Kinachotakiwa hapa ni kuweka mipangi sawa na kurekebisha mipango mibovu ya huko nyuma ili kuwe na usawa katika kufaidika na rasilimali hizo ambazo zinahitaji mtaji katika kuzifanya ziwe za manufaa kwa umma.
 
Mbopo let me agree kwamba you are right on this na tuangalie uhalisia sasa .Tumesha chimba sana hadi sasa eneo kubwa ya madini yamechimbwa kweli .Je tunepata ngapi na wangapi wamenufaika na machimbo haya iliwa ni mali ya wananchi wote ? Usisahau kutaja wahanga wa maeneo ya madini pia mkuu .Haya nangojea useme .
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Ukiona hivyo ujue yeye ni mfaidika anashindwa kuelewa tu kuwa njaa yake inamfanya auze haki yake ya uzaliwa wa kwanza kwa mchuzi wa dengu ili tu atulize minyoo tumboni. Hajui kuwa siku moja yeye pamoja na kizazi chake watajitolea hata uhai wao kuweza kuwaondoa hawa watu ambao leo tunawakaribisha kwa magoti.

Uwekezaji bila maandalizi ya watu wa ndani ni ukoloni waaina yake nchini kwetu. Sijawahi ona hata mfano mmoja wakupigiwa mfano kuanzia viwanda vya wahindi hadi makampuni ya wageni kwamba wameleta welfare. Kama kwa uchache tu hali ni hii vipi tukiwafanya kuwa giants wa uchumi wetu si ndiyo hii tunayosikia kwamba mafisadi wakiguswa nchi itayumba itakuwa order of the day?

Kwanini lakini Rais wetu anakosa huruma na sisi watu wake? Okay hasikii sauti zetu wachache lakini je ushuhuda wa maisha ya wabongo wengi walio katika ajira za hawa 'wawekezaji uchwara' si kelele tosha kumfanya aache kwanza atafakari niwapi tumepotoka?
 
Akiwa hapa nyumbani anasema tumejaribu tumeweza........anasema chakula kipo, maghala ya serikali yamejaa chakula cha kutosha...
Akienda mje anasema ...helpe us to improve food security.........my bad!!

mi ndio maana huwa nashangaa watu wanaosema hatuwezi kuongozwa na wanawake wakati behaviour za viongozi wetu hazina tofauti na kinamama! we need real men who can stand for us! sio kwenda kutetemekea wazungu
 
Kazi kulia lia tu. Yeye alichosema ni kwamba lazima kuwe na reciprocity katika kuvuna rasilimali na kwa taarifa yenu rasilimali hizo haziwezi kuleta maendeleo kwa kuendelea kuwa ardhini. Kinachotakiwa hapa ni kuweka mipangi sawa na kurekebisha mipango mibovu ya huko nyuma ili kuwe na usawa katika kufaidika na rasilimali hizo ambazo zinahitaji mtaji katika kuzifanya ziwe za manufaa kwa umma.

Reciprocity gani unayoiongelea, yeye analia tu akiwa huko nje kuwa inahitajika kuwa na reciprocity, wakati mikataba aliyo iatamia magogoni imejaa madudu!!! Alijifanya atabadili mikataba ya madini wapi..... tunashuhudia the so called 'wawekezaji' wanavyooombwa na kubembelezwa kulipa kodi!!! Nimeshangaa sana kuwa Ashanti ndo kwaaaaaanza wanaanza kulipa corporate tax this year 2011 baada ya miaka kumi...

Halafu leo unasema, hajakosea..... my foot with JK issies!!! Zimejaa unafiki... I like the way Nigerians and Rwandees... they are attending the forum strategically!!! Sisi tumepeleka wauza sura na wapenda sifa...
 
Ukiona hivyo ujue yeye ni mfaidika anashindwa kuelewa tu kuwa njaa yake inamfanya auze haki yake ya uzaliwa wa kwanza kwa mchuzi wa dengu ili tu atulize minyoo tumboni. Hajui kuwa siku moja yeye pamoja na kizazi chake watajitolea hata uhai wao kuweza kuwaondoa hawa watu ambao leo tunawakaribisha kwa magoti.

Uwekezaji bila maandalizi ya watu wa ndani ni ukoloni waaina yake nchini kwetu. Sijawahi ona hata mfano mmoja wakupigiwa mfano kuanzia viwanda vya wahindi hadi makampuni ya wageni kwamba wameleta welfare. Kama kwa uchache tu hali ni hii vipi tukiwafanya kuwa giants wa uchumi wetu si ndiyo hii tunayosikia kwamba mafisadi wakiguswa nchi itayumba itakuwa order of the day?

Kwanini lakini Rais wetu anakosa huruma na sisi watu wake? Okay hasikii sauti zetu wachache lakini je ushuhuda wa maisha ya wabongo wengi walio katika ajira za hawa 'wawekezaji uchwara' si kelele tosha kumfanya aache kwanza atafakari niwapi tumepotoka?
nakubaliana nawe kwenye nyekundu lakini nashangaa kuwa unakubaliana naye kwenye swala la kuleta wawekezaji huku ukijua wazi hakuna maandalizi ya kutosha ya kuweza kuwafanya wananchi wafaidike na hao wawekezaji. binafsi naamini kuwa ni watanzania pekee ndio wanaweza kujiletea maendeleo yao wao wenyewe na siyo wawekezaji kutoka nje kwani kazi yao ni kuiba kupora na kuhujumu nchi hawajali kama watu wanafaidika au vipi angalia mfano wa nchi zilizokabidhi rasimali zao kwa wawekezaji zilizoendelea hakuna hata moja.
 
Back
Top Bottom