Haya ni mapenzi au kujidhalilisha!!

hajiamini, au hana kazi ya kufanya. haya siyo mapenzi, kuna hatari kawekwa kiganjani
 
Huko Uholanzi Wanaume na wenyewe wanapewa Likizo ya Uzazi km Mkeo kajifungua
Huko Kilimanjaro Mwanamme anashinda kilabuni kwenye mbege na hela za mauzo ya kahawa na maharagwe hajui nyumbani mama kaenda shamba na kurudi na kuni wakati chakula hakuna cha kulisha familia.
Kwa hiyo ya Ngoswe mwachie Ngoswe maana km Housegirl hakuna Baba ndio anatakiwa ambane huyo wa kike wa darasa la 7 apike na kusaidia kupika
Mm nimeona kwa waarabu Mwanamke akijifungua hashiki kitu chochote ni kazi ya Mama mkwe na house girl au House Boy sasa km huna uwezo huo au huamini katika UTWANA NA UBWANA msimlazimishe aige mila za UMWINYI acheni afanye kazi
Leo ukiombwa mtoto wako akawe Housegirl wa mwarabu au mswahili TAFADHALI kataa
 
inanikera na leo imenikera zaidi hadi nasikia kukereketwa kooni! Jamani hapa ninapoishi kuna jirani ambaye ni baba mwenye familia ya mke na watoto wanne. Kati ya watoto hao mmoja wa kufikia ni wa kike ambaye amehitimu elimu ya msingi, na wa kiume yupo darasa la sita wakati hawa wengine wawili ni wadogo.
huyu bwana akiwa nyumbani anafanya kazi zote kama mke/mdada wa kazi ikiwa ni pamoja na kupiga deki, kuosha vyombo, kupika, na kufua nguo zote hadi nguo za ndani za mke wake na matambala anayotumia akiwa katika siku zake (hii ni kweli kabisa) na mbaya zaidi kazi hizi huzifanyia nje kweupe kabisa na akina mama majirani wakiwa wanamwangalia ikiwa ni pamoja na hao watoto wake wote !! Sasa kitu ambacho kimeniudhi leo ni kuona anafua suruali na nguo zingine za huyo binti yake wakati yeye anacheza lede barabarani, binafsi najiuliza haya ndio mapenzi tunayostahili kuwaonesha/kuwafanyia watoto na wake zetu? Na je, nitumie njia gani kumfikishia ujumbe kuwa anayofanya ni kujidhalilisha? Kwani imefika sasa watoto wanamuona kama mhudumu tu hapo nyumbani. Naombeni ushauri wemu kwani mwanakwetu anatutia aibu.



eeh eeeeeh,,kwani vipi??
Niache nimsaidie mheshimiwa mke wangu,,sitaki niache nimsaidie,,hata kama ni limbwata si nimepewa mimi kwani we ina kuuma nini??
Mibinjuo ninayompa usiku we huioni,,au unaiona??au unakuja kumsaidia??mbona shughuli ninayompa usiku yeye anavumilia tuh??kuhusu mtoto huyo wa kufikia we niache tuh nimfulie,,si nimempenda mama ake??napenda na ua lake sasa,kwani kuna ubaya??
Ukinifatilia na kunionea huruma wala hutonimaliza dada,,sijaanza leo shughuli hii
tumependana wenyewe maneno maneno ya nin??
Me machungu yangu nalipizia usiku na napewa bila masemango
niache,nimesema niacheee...
 
Acheni wivu nyie!! Watu wakipendana watia midomo, wakipigana wawasaidia kuripoti TAMWA!! Acha wale bata na hakuna hata mmoja kati yao ameshaleta kesi mtaani eti anaonewa!!! Pilipili usioila yakuwashia nini?
 
Afu dunia hii ya sasa ya matambara kweli, mjini hapa??
Wakati kuna freestyle hadi za mia mbili??
Wizi mtupu!
Mwanamme mzima kiushikwa ushahidi ndio huku

Umeona eeh! Amekurupuka ameshindwa hata kujipanga!
 
Aaaaaaah! Embu muache bi shosti AJILIE MATUNDA YAKE YA SUKARI YA DUBAI!!!!!!!!!! Chezeyaaaa KUWEKWA KWENYE CHUPA NA KUPILIZIWA KUTWA MARA 3!!!!!!!!!!!!!

Hata akimwambia NIBEBE nipeleke Dukani anambeba!!!!!!!!!!!!! Ndo dawa yenu hiyoooo bila hivo BEIJIN tutabaki twaisikia!!!!!!!!!

Na kama ningekuwa mke wa huyo mbaba ningesikia unaleta ushambenga NA WEWE NAKUWEKEAAA VITUZZZZZ!!!!!!! WATULI WAMSAIDIA MWENZIO KUSUUZA VITAMBAAAA!!! lol!

kama ndio hivyo hata mimi ntakuwa nimewekwa kwenye chupa maana kila siku lazima nifue.hebu ngoja nikamuwashie mke wangu moto kwamba kwa nini ananiweka kwenye chupa hivihivi.
 
conclusion..., wanawake wamesapoti mambo anayofanyiwa mwanakwetu. wanaume hawajakubaliana na hii hali huku wengine wakishangaa kinachomtokea mwanakwetu. kimsingi hali hii haikubaliki na ni bora wanaume tujue mipaka yetu katika mapenzi na kuishi kama vichwa vya familia.
 
Tatizo langu sio kwenye yeye kufua 'matambara' ya mkewe (hizi vitu bado zinatumika?). Muache amfulie mkewe banaa, kama anakula chumvi seuze kufua? Tatizo langu ni huyo binti anaecheza ready wakati babake anamfulia. Hajafunzwa kuwa responsible, akiwa na kwake na kama mganga wa mamake keshakufa mbona ndoa itamshinda?
 
Tueleze kwanza mke wake ni mtu wa wapi (mkoa gani)? tukijua anakotoka tutajaribu kumsaidia ushauri.
 
wewe unapungukiwa na nini?hayakuhusu jali ya kwako

Kuna wakati watu wa nje huwa inatuhusu. Maisha sio mtu na mkewe tu, kuna jamii. Sasa unakuta kila mnachopanga kufanya na mshikaji mkewe anamkataza hata cha faida ya familia yake. Mwenzenu kafiwa hata na mamaake jamaa linakatazwa na mkewe kwenda kumpa pole mshikaji! Nakumbuka kuna mshikaji mkewe alikuwa anamchomoa kwa matusi na kumsukunasukuma hata mbele ya kadamnasi eti arudi nyumbani akafue. Kwa mfano mnacheza draft hivi, analibinua hivi kumwaga kete!!! Acha bana, usifanye mzaa ni haya mambo.
 
Inanikera na leo imenikera zaidi hadi nasikia kukereketwa kooni! Jamani hapa ninapoishi kuna jirani ambaye ni baba mwenye familia ya mke na watoto wanne. Kati ya watoto hao mmoja wa kufikia ni wa kike ambaye amehitimu elimu ya msingi, na wa kiume yupo darasa la sita wakati hawa wengine wawili ni wadogo.
Huyu bwana akiwa nyumbani anafanya kazi zote kama mke/mdada wa kazi ikiwa ni pamoja na kupiga deki, kuosha vyombo, kupika, na kufua nguo zote hadi nguo za ndani za mke wake na matambala anayotumia akiwa katika siku zake (hii ni kweli kabisa) na mbaya zaidi kazi hizi huzifanyia nje kweupe kabisa na akina mama majirani wakiwa wanamwangalia ikiwa ni pamoja na hao watoto wake wote !! Sasa kitu ambacho kimeniudhi leo ni kuona anafua suruali na nguo zingine za huyo binti yake wakati yeye anacheza lede barabarani, binafsi najiuliza haya ndio mapenzi tunayostahili kuwaonesha/kuwafanyia watoto na wake zetu? Na Je, nitumie njia gani kumfikishia ujumbe kuwa anayofanya ni kujidhalilisha? Kwani imefika sasa watoto wanamuona kama mhudumu tu hapo nyumbani. Naombeni ushauri wemu kwani mwanakwetu anatutia aibu.

Hayakuusu, subiri aje akuombe ushauri ndio umpe. Hujaombwa unatoa ukiombwa je?
 
He he he he, hii taarabu naipenda
Kwa mfuga Mbwa inapigwa mwamnzo mwisho

Kanikumbusha kuna jirani baba mzima aliwahi shushuliwa sina hamu

aliambiwa na binti karibia kwa kumzaa "mtu mzima ushahidi" Aliondoka kainamisha kichwa
Baba yangu akamwambia, wewe utaingiliaje mambo ya familia za watu

Huwa sitaki ushahidi kwenye familia za watu

Mashauzi Classic "Sina muda huo sina... Wa kukaa vibarazani na kumdiskasi mtu...!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom