Haya ndio Maneno ya Mwisho ya Baba wa Taifa Hili Mwalimu Nyerere Kuhusu Muungano!!

W. J. Malecela kwa nini kama mnataka serikali mbili wawakilishi wa znz watoe tamko sasa kuwa watarekebisha katiba yao. hakuna haja ya kutumia nguvu. na muwaambie znz kuwa mambo ya muungano yanatakiwa kuwa yanaongezeka sio kupungua.

Ili kuonekana kijana unatakiwa kuongea kwa fact sio kukariri maneno ya nyuma bure bure. sikujua kama wewe ni mwepesi kiasi hiki.pamoja na msimamo wa chama chako ulipaswa kuandika hapa sababu za kupendekeza serikali mbili. vijana tukiwa hivi n aibu jamani.

wanafiki wakubwa nyie, acheni uzandiki wa kishenzi
 
Last edited by a moderator:
Nyerere alitufundisha pia kwamba tusiwe wajinga, alitufundisha kuwa watu wa kufikiri na kutafakari na kwamba yale mazuri tuyadumishe na yale mabaya turekebishe....pia alituambia ya kwamba mtu akikuambia kitu cha ujinga huku akitambua kuwa ni ujinga...halafu wewe ukakubaliana na ujinga.....hiyo ni hatari kubwa sana.......

....therefore hili ni suala la kutafakari kwa kina na last decision ibaki na wananchi wa pande zote......
 
Tuache kuchanganya mambo hapa
Kwani kila kitu alichosema Nyerere ni ukweli? Kuna watu aliwaita Wahuni je nalo hilo ni kweli? Tusichague yasiyotugusa na kuacha yanayotugusa.
 
Usilishe watu maneno.Hoja inayo jadiliwa mezani ni muundo wa serikali.AMA SSERIKALI MOJA,MBILI AU TATU.hakuna anayesema muungano uvunjwe.
 
- Mkuu punguza hasira maneno ya Mwalimu hapa mimi sijasema kitu, kama unataka pingana na maneno ya Mwalimu Baba wa Taifa kama alivyofanya Warioba, usinilaumu mimi hapa sijasema anything punguza hasira haya sio maneno yangu kaka ni ya Mwalimu!1

Le Mutuz

mkuu sio warioba aliepingana na mwalimu ni wananchi ndio walipiopingana na mwalimu..by the way naamini muungano sio msahafu kwamba usiguswe.
 
Nyerere alikuwa binadamu kama wengine maneno yake siyo msahafu kuwa yasipingwe, hakuna anayetaka kuvunja muungano tatizo la huu muungano una matatizo mengi.

Watu wanaitaji muungano wenye maslahi pande zote mbili, Jaji Warioba kaeleza kero za muungano huu wa kimaghumashi.

Siyo wote wanahoji huu muungano wanataka madaraka.[/

kwa mara ya kwanza leo nakuunga mkono..big up sana
 
Kumbe mnamkumbuka tu kuhusu muungano vipi kuhusu rushwa, ufisadi na uhujumu rasilimali za taifa?
-mikataba feki unaizungumziaje?
-utawala wa kifalme unaochipuka kwa kasi unauzungumziaje?
-vyombo vya dola kuua raia wasio na hatia unazumgumziaje?
-kuwafanya wananchi watumwa katika nchi yao vp?

**KAMA KWELI MNANUENZI NA KUMKUMBUKA MWALIMU BASI MKUMBUKENI KWA MATENDO.

My take: Tanzania kwanza wageni baadae

Nilitaka kuweka yangu ila kwa uliyoandika umemaliza, umenena hadi raha.
 
wanafiki wakubwa nyie, acheni uzandiki wa kishenzi

mnafiki ni wewe unayefuata mkumbo,wewe ukiambiwa kula mavi unakula tu,jamaa katoa hoja nzuri kwamba malicela kama ana support serikali 2 atoe uzuri wake basi au sababu za kufanya hivyo,we una ropoka tu,mburula wewe
 
"Kuifufua Tanganyika ni Kuiua Tanzania,Sikubaliani Kabisa na Swala hili,Kwa Sifa tu na Uroho wa Madaraka na huku Wakishabikiwa na Mazuzu kuna watu Watafanya Kila hila Zanzibar Ijitenge na Tanganyika,Nasema Dhambi hii ya Utengano na Iwatafune,Naomba Mungu anisamehe,Hakika Dhambi ya Utengano na Iwatafute hawatabaki Salama" - By.Mwl.Julius Nyerere.

"...Waasisi walituachia muungano wa nchi moja
yenye serikali mbili na siyo nchi mbili zenye
serikali mbili..." - Jaji Warioba
 
Mkuu naomba ujibu nukuu ya Mzee Warioba.....ni ya msingi sana, Nini chimbuko la nchi mbili zenye serikali mbili ambayo ndio hoja ya CCM

- "Serikali ya Tatu itategemea michango toka Serikali mbili, kuna uwezekano wa Serikali ya Tatu siku moja kukosa pesa za kujiiendesha kwa vile haitakuwa na Rasilimali, hata tume ya Rasimu imeshindwa kusema Serikali ya Tatu itatoa wapi pesa za kujiendesha" - BY JK

Le Mutuz
 
Maneno ya Nyerere sio msaafu. Na ukisoma maandiko ya biblia Mungu aliruhusu Ibrahim na Rutu watengane ili kuepusha machafuko ya ndugu hao.
 
Haka ka mungano mbona kanaliliwa hivi. Kwani Kana nini cha maana. Mbona Mimi sioni. Mpaka inafikia kuombeana laana kwa mwenyezi.

Marekani miaka ya 1800 kipindi cha rais abraham lincoln walipata sakata kama hili. Wakapigana civil wars so to defend the union. Lakini Hawa walikiwa sahihi kwa sababu walikiwa na nchi nyingi Zilizoungana, na sio mbili kama sisi. Hapa point ya defence ipo. Lakini kwa Tz na znz siioni.

To hell with this non profitable union.

Note. Sim yangu ina tatizo la letter 'u' so don't mind where it brings some confusions.

Ahsante kwa mfano, lakini naomba ujaribu kutuletea mifano inayofanana na mazingira yetu hapa Africa. Mazingira na hali ya Marekani ni tofauti saana ndugu!
 
Back
Top Bottom