Haya ndio mambo makubwa yanayoigharimu ccm

Join Date : 3rd May 2012
Posts : 10
Rep Power : 303
Likes Received6
Likes Given0




Umetumwa kuja kuwaamsha ccm? Kama kweli unapenda mabadiliko, huu siyo muda wa kuwaambia ccm wafanye nini...so what??? Ili waendeleze ufisadi wao na kuangamiza raslimali za taifa kwa makaburu wa ndani na nje ya nchi???? Watu tunataka mbadala wa ccm na si vinginevyo...Anyway...karibu jamvini..
 
Undiluted truth. Spot on and to the point. But I'm curious to knnow the reasons why you took the troubles to laid it bare
 
jg.jpg


tnajari tu wakuu muwe wapole tukifaniwa tutawaambia ila kwa sasa mtuvumilie tuuuuuuuuu
 
Hapo cdm mbona dr Slaa ni mungu mtu pamoja na mbowe
Hapo ndipo unapokosea
Kosa la Chadema halihalalishi kosa la CCM
Mtoa mada ameamua kuwasaidia CCM, ameijadili CCM wewe unaitetea CCM kwa kujilinganisha na Chadema
Mmepewa dokezo ili CCM isipotee kwenye historia na inapaswa izingatie ili ije kuwa chama imara cha upinzani
 
Wanaccm msiposhughulikia mambo haya, hakika chama chenu kitashindwa vibaya 2015 na hata chaguzi zingine.
(1)Raisi kuwa mwenyekiti wa chama Taifa.
Hili ni tatizo kubwa sana, kwani inakuwa vigumu kwa chama kuisimamia serikali hata pale inapoboronga kwa mfano hali ilivyo sasa.
(2)Utaratibu kuwa raisi aliyepo lazima atumikie vipindi 2 vya miaka mitano mitano.
Hakika huu ni utaratibu mbovu sana kwani hata kama ataonekana kupwaya au kuvurunda ktk kipindi cha kwanza shariti apewe kipindi cha pili na ukimpinga chama kinakujia juu.Kigezo kiwe ni uwezo ni si kubebana na athari yake hata nyie sasa mnaiona.
(3)Individuals kuwa muhimu kuliko hata chama.
Inasikitisha sana ccm ya leo iko radhi kubeba watu wachache kwa gharama ya chama kizima.Mtu amefanya madhambi ya wazi ila atalindwa kwa nguvu zote bila kujali athari kwa chama.Kulindana ni cancer ianayotafuna taswira ya chama chenu mbele ya macho ya umma.
(4)CCM ya leo kutokujali na kupuuza shida za maskini walio wengi na kujali matajiri kuanzia kwenye chama chenyewe na nchi nzima kwa ujumla.
(5)Wanaccm wenyewe kushindwa kukemeana,kukosoana na kuelzena ukweli pale mnapokosea na badala yake mmewaachia wapinzani hakika watazidi kupanda chati.
(5)Ahadi za miaka nenda rudi zisizotekelezwa.
(6)Wanaccm kumuona raisi kama mungu mtu asiyestahili kukosolewa na badala yake kujipendekeza kwake mkitarajia kupewa vyeo.Mkosoeni siyo kujipendekeza anakiathiri chama.
(7)Viongozi na wanaccm kutokusoma alama za nyakati.
Athari yake mnashindwa kujua nini umma wa watanzania unataka kwa sasa na mmebaki kuhubiri siasa za kizamani za amani na utulivu.Watanzania wa leo wanajua hata wapinzani wanaamini na kuthamini uwepo wa amani na utulivu.
(8)Rushwa wakati wa uchaguzi.
Hii ni wakati wa uteuzi wa wagombea ndani ya chama na kwa wapiga kura kwa ujumla.Kumbukeni sasa hivi vyombo vya habari vinaendesha elimu ya uraia isiyo rasimi na watanzania wanaelimika na kujua athari ya rushwa hasa kwenye uchaguzi.
(9)Siasa za makundi na ufalume wa kupeana madaraka unaojipenyeza kwa kasi ndani ya chama chenu.
Hapa sihitaji kutoa ufafanuzi wenyewe mnayajua haya.
Huu ni ushauri wa bure kwenu.

Kwa ufupi, kinachoiua CCM ni utawala mbovu usioangalia sheria.
 
Tunashukuru ndugu yetu Salary slip kwa kusema ukweli. Laiti viongozi wetu wangekuwa wakisikiliza na kuzingatia maoni kama haya chama chetu hicho kikongwe kingeweza kuepuka kifo. Lakini macho yao yamefungwa kwa kuwa mwisho wao umefika.
 
Mkuu umenena... Pia kuna ishu ya raisi na familia yake kufanya biashara wakiwa ikulu...
 
tunashukuru ndugu yetu salary slip kwa kusema ukweli. Laiti viongozi wetu wangekuwa wakisikiliza na kuzingatia maoni kama haya chama chetu hicho kikongwe kingeweza kuepuka kifo. Lakini macho yao yamefungwa kwa kuwa mwisho wao umefika.
kwa sasa chama kiko makini mno baada ya hili baraza jipya imani ya watu imeanza kurudi kwa kasi sasa kidumu chama chetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom