Haya matukio mawili; Kuna kitu asili inajaribu kutufundisha

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,657
698,408
Ni kitu cha kiroho sana na chenye mamlaka makubwa kwenye kanuni za asili za kidunia.. Ni kitu ambacho kama kingetokea miaka kumi hivi iliyopita PANGECHIMBIKA na pengine damu ingemwagika na hata kusababisha uharibifu mkubwa wa mali

Sio matukio ya kisiasa la hasha bali ni matukio ya kidini na wanadini.. Hata kama yanaweza kuwa ni ya kupanga ama kupangwa.. Wahusika hawakufanya kwa utashi wao bali kuna nguvu kubwa ya kiasili iliwasukuma kuyatekeleza

Tulimaliza mwaka 2022 na tukio lenye tafsiri nzito kiimani na kiroho.. Lakini kimwili wanadamu walipumbazwa na kukosa taharuki na misigano.

Ni tukio la wanadini kwa vyeo vya mashehe kutoka Dar walipojikusanya na kutoa tangazo la kumsifia sana kiongozi wa imani nyingine tofauti na yao, tangazo husika likafuatiwa na ahadi ya kwenda kumtembelea huyo kiongozi mwenye cheo cha nabii.. Na kweli walifanya hivyo na video zikarushwa.. Walimsifia sana sana

Wakamaliza ziara yao salama wakarejea majumbani mwao salama na hakuna dhahama iliyowapata! Kiongozi wao mkuu akawaita kwa upole na kuwauliza KULIKONII wakafanya yale..

Kwa mshangao mkubwa sana hata wao wakawa wanajishangaa wakiwa hawajui walipatwa na nini mpaka wakafanya yale yote!

Jambo lile liliisha kwa kuonywa, kuelekezwa kuomba radhi na maisha yakasonga kama hakuna kilichotokea kwenye jamii. Nikavuta taswira ya miaka kumi iliyopita hili lingetokea ingekuwaje.. Maana sidhani kama angepona mtu!

Asili inafanya kazi juu ya uwezo na maamuzi ya kibinadamu.. Asili ndio inatoa miongozo! Na hakuna awaye yote awezaye kupingana nayo!

Tukaingia mwaka mpya wa 2023 salama salimini.. Kiongozi mwingine maarufu wa kidini akawafagilia vijana wa dini nyingine kwa weledi na uaminifu

Jambo hilo likapokelewa kwa shangwe kubwa sana na wanadini wa dini ya wale vijana! Na ile video fupi yenye kuwasifu ikarembwa na kuwekwa nakshi za dini yao na ikasambaa ama kusambazwa kwa kasi sana
Hali ilikuwa tofauti kwa dini ya kiongozi husika, akaadhibiwa kwa mujibu wa kanuni zao.. Lakini mijadala ikawa mikubwa mitandaoni hasa wakimlaumu kwa kitendo kile na ya kwamba tukio moja tu tena lililomtokea yeye kalifanyia majumuishi kwamba vijana wa imani yake sio waaminifu na wa imani ya upande wa pili ndio waaminifu

Hebu turejee nyuma kule ambapo
Kuchinja tu wanyama kwa ajili ya kitoweo kulizua taharuki kubwa mpaka watu kususiana mabucha
Hebu turejee kule nyuma ambapo watu walijeruhiwa, kuuliwa na nyumba za ibada kuchomwa moto kwa vitu vidogo mno!

Hebu turejee kule nyuma ambapo hata mavazi ya wanafunzi shuleni mjadala wake nusura usababishe maafa nknk

Leo hii amani imetamalaki.. Tumeponywa majeraha mengi.. Nadhani tuna uelewa wa kutosha sasa ya kwamba kumbe nje ya hizi dini sisi ni ndugu, sisi ni marafiki sisi tuna asili moja. Tumefika mahali pa kuonesha ukomavu mkubwa wa kuvumiliana hata ndani ya dini zetu.

Imefika mahali tunayaheshimu maoni ya wengine hata kama yanatuudhi na kutukera

Asili imetuletea haya matukio mawili kama kumbusho la tulikotoka lakini kama tahadhari ya tuendako.. Ya kwamba kama tuliteleza lakini hatukuanguka tukasimama imara tumakinike hayo yasije kutokea tena!

Dini zetu si chochote si lolote mbele ya asili.. Asili ni timilifu, dini ni kengeufu
 
Najaribu kuwaza tu. Hivi kama tungekuwa busy kulijenga taifa letu kwa kufanya kazi kama tunavyoona mifumo ya nchi za wenzetu. Tungekuwa na wingi wa makanisa?
Muktadha wa wingi wa makanisa unaletwa na tatizo sugu la ajira, kukata tamaa na kutafuta short cut ya kutoka kimaisha kwa waumini hata kwa wamiliki
 
Mwaka 2012 wakati yule mtoto Mbagala kafanyaje sijui Qur'an,watu wakachoma makanisa rafiki yangu mmoja ktk kupiga piga stori ambaye tulitegemea awe think tank,ni master's degree holder akajiapiza "Wallah Yule mtoto hata Mimi ningemkamata nachinja".. Dini Dini Dini
Wale mashehe siku ile wasingefika kwao ama wasingekatiza hata wami na yule nabii angekiona cha mtema kuni
 
Ilifika mahali mpaka watu wanatambiana matajiri.. Kwamba dini yangu ina matajiri wengi kuliko yako
Dini yangu ina matajiri huo ni ushamba, kama wanao sifia heti wao ndio wengi bungeni halimashauli polisi mahakimu dini yao heti ndio yenye shule nyingi mahosipitali huo ni ushaba tu kwani hao walioko serikalini wa dini yako hiyo rushwa na hela wanazo iba unapewa au hayo mashule na mahosipital unaweza peleka mtoto wako akasoma bule au kutibiwa au hayo matajiri waliomo kwenye dini yako wewe unafidika nn na utajiri huo huo wote ni ushamba
 
Mwaka 2012 wakati yule mtoto Mbagala kafanyaje sijui Qur'an,watu wakachoma makanisa rafiki yangu mmoja ktk kupiga piga stori ambaye tulitegemea awe think tank,ni master's degree holder akajiapiza "Wallah Yule mtoto hata Mimi ningemkamata nachinja".. Dini Dini Dini
Huyo alikuwa ajui lolote mtoto mdogo wakale walimuita malaika
 
Back
Top Bottom