DOKEZO Haya mashimo barabarani tunataka yachimbuke futi ngapi ili kuyaziba

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mvua zimeleta majanga na kuacha majanga. Lakini Mvua zisingekuwa na maafa makubwa kama tungekuwa na mifumo mizuri ya maji taka. Kwa kuwa na mifumo mibovu maji yamejitengenezea njia zake na kuharibu miundombinu mingine. Barabara nyingi sana haziko katika hali nzuri na zinaweza kuharibu magari mengi sana nchini.

Kwa kuzurura sehemu chache tu, nimeona yafuatayo. Kona ya Shekilango (Dar), karibu na soko kuna bonge la shimo na lina maji mengi. Sijui kwa nini linaachwa hadi muda huu ikiwa serikali za mtaa zipo.


Barabara ya Temeke na Stand ya Temeke imejaa madimbwi na maji meusi ambayo ni tishio kwa magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu ambacho kwa sasa ni tishio kwa afya za waliowengi.


Madimbwi hayo na maji haya ni hatari kwa vyombo vya moto na kwa watoto. Je tunasubiri mtu afe?
Kwanini tusijenge mitaro mikubwa ya ardhini....yaani mtandao wa mitaro mtaa hadi mtaa mixer maji taka ya majumbani
 
Njoo mkoani mtwara ambapo shetani amechimba mashimo mpk ameamua kuyafukia mwenyewe tu!
Mwisho wa mwaka nilkuwa nampeleka jamaa yangu mkoa wa Tanga kutoka huko kusini (masasi) to Tanga asee unakwepa mashimo na draft za kutosha hadi unabaki kucheka
 
Kalete mkuu
Na huku ni ushuaji
20240116_120306.jpg
 
Back
Top Bottom