DOKEZO Haya mashimo barabarani tunataka yachimbuke futi ngapi ili kuyaziba

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
420
670
Mvua zimeleta majanga na kuacha majanga. Lakini Mvua zisingekuwa na maafa makubwa kama tungekuwa na mifumo mizuri ya maji taka. Kwa kuwa na mifumo mibovu maji yamejitengenezea njia zake na kuharibu miundombinu mingine. Barabara nyingi sana haziko katika hali nzuri na zinaweza kuharibu magari mengi sana nchini.

Kwa kuzurura sehemu chache tu, nimeona yafuatayo. Kona ya Shekilango (Dar), karibu na soko kuna bonge la shimo na lina maji mengi. Sijui kwa nini linaachwa hadi muda huu ikiwa serikali za mtaa zipo.

1705385701534.png
1705385715593.png

Barabara ya Temeke na Stand ya Temeke imejaa madimbwi na maji meusi ambayo ni tishio kwa magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu ambacho kwa sasa ni tishio kwa afya za waliowengi.

1705385821022.png
1705385832307.png

Madimbwi hayo na maji haya ni hatari kwa vyombo vya moto na kwa watoto. Je tunasubiri mtu afe?
 
Wanajenga miundombinu mibovu ili wajitengenezee hela kwenye marekebisho ya mara kwa mara.

AKILI AKILI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Kona ya shekilango ilianza kama katone tu maji yalituma kwa kiasi kidogo baadae paka bonyea ile lami ikatoka kalikuwa kadogo sana , sina hakika kama mamlaka hawajaliona huwa tunasubiri likue liwe tatizo ndio waje kitu mbacho itaongeza gharama kutibu
 
Mkuu mtoa hoja hapo solutions ni moja, JMP alithibitisha kuwa unaweza kupata jawabu la tatizo on the spot, kusanya wakazi wote wa mtaa huo na funga hiyo barabara, within 30mins mkuu wa mkoa,RPC, wajenzi wa barabara watafika hapo na kuwasikiliza na kuona tatizo hilo, humu ni kulalama tu, hakusaidii chochote
 
Hili ni janga la nchi nzima, ukitembea huko mikoani utajionea mashimo kila barabara
Mambo yanaenda kasi sana, uwajibikaji hakuna kabisa. Sasa hivi kupita njia usioijua ni mtego. Nitawaletea picha ya kashimo kalikoanza kama kashimo ka panya.
 
We inashangaa mashimo, hauulizi majitaka yalivyojaa karibia kila kona Kariakoo chemba zinafurika na hapo ndiyo tunaambiwa wilaya inayoongoza kimapato!
 
Sasa si bora nyie hilo likwepeni tu, huku mikoa mingine kuna shimo IST ikiingia haionekani
 
Kwa sisi wa "Kijitomchuzi" weka na Kijenge road karibu na makutano ya Mabatini Road na ile ya Mama Salma Road...barabara kila mvua zikinyesha lazima ziondoke na lami...

Kuna shimoz nyingine zipo Maktaba Street/Azikiwe Rd hapo karibu na Holiday Inn, nyingine pia sugu zipo Azam Round pale Jamhuri, India na Mkwepu zinapokutana...halafu sasa funga kazi ipo Zanaki St karibu kabisa na DTV roundabout...
 
Pesa nyingi za kigeni zitatumika kuagiza vipuri kutokana na magari mengi kuharibika, hawa watu wanawaza kujipimia kwa urefu wa kamba hawajali hali ya maisha ya wananchi na uchumi wa nchi kiujumla.

Juzi nimepita barabara ya kitunda-kivule, ni mbovu hatari huku ikitumiwa na magari kibao, daladala na yale ya watu binafsi, nchi imeshindikana hii....​
 
Kwa sisi wa "Kijitomchuzi" weka na Kijenge road karibu na makutano ya Mabatini Road na ile ya Mama Salma Road...barabara kila mvua zikinyesha lazima ziondoke na lami...

Kuna shimoz nyingine zipo Maktaba Street/Azikiwe Rd hapo karibu na Holiday Inn, nyingine pia sugu zipo Azam Round pale Jamhuri, India na Mkwepu zinapokutana...halafu sasa funga kazi ipo Zanaki St karibu kabisa na DTV roundabout...
Hayo ya DTV juzi usiku niliyavaa,yalifunikwa na maji!
 
Kama unatoka Temeke ile kona ya kwenda Tazara kuna bonge la shimo,huku mitaani ndo shida tupu na hakuna anayejali, mpaka unajiuliza hawa viongozi wa serikali za mtaa kazi yao hasa ni ipi?

Na kingine huku mitaani kinachoharibu sana barabara ni kukosa mifereji na karavati,mvua ikinyesha barabara ndo ndo mfereji unategemea nini? Hata kama hakuna lami,ili la maji ya mvua kukatisha barabarani tutaendelea kulalamika kila siku.Kuna muda mpaka unajiuliza sisi watu weusi tuna akili za namna gani?
 
Back
Top Bottom