Haya mambo ya nimesikia, nimeambiwa, nimeona kwenye TV ndo yanayotugharimu

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,917
Heshima kwenu Wajasiriakilimo.

Swala la Ujasirimali ni gumu sana, Ujsirimali sio swala la kitoto, unahitajika kujitoa mhanga ki sawa sawa.Wengi wamekuwa wanafanya hivyo na wengine imekuwa ni kazi ngumu.

Wengi wetu tunapenda sana mafanikio, ila ya muda mfupi na ndo yanayo pelekea haya yote yanayo tokea,
Wengi wetu hatuna spirt ya ujasirimali zaidi ya kutaka tajiri wa short cut wa kulala na kuamka tajiri, mtu anataka alime na auze anunue hata V8 ndo hayo tunawaza wengi wetu.

Sasa tumebakia kujaribu hiki na kile, yaani mtu hana ndoto tena ubongo umefikia mwisho kwenye kuwaza, yaani kama ni gari imekita haiendi mbele wala hairudi nyuma

Kufuata mkumbo kulivyo.
Utakuta mjasirimali mwenzangu alikuwa analima nyanya, kaacha ghafla halimi tena, karukia vitunguu kwa sababu alisimuliwa kuna jamaa kajenga nyumba kwa vitunguu, kalima masimu mmoja kaona hailipi kaacha, kaaza kufuga kuku wa mayai kafuga kaona hailipi kaacha, kauona kwenye TV kilimo cha ufuta kina lipa, katuafuta shamba kalima msimu mmoja kaacha, kashawishiwa afuge Broilers kafuga kama mara mbiuli kaacha, kaona kwenye TV kutengeneza sababu karukia, katengeneza kaacha, karukia kufuga Sungura kwa sababu kaambiwa inalipa.

Wakuu kwa staili za aina hii sahai mazima mafaniko, make hapa mtu anakuwa haeleweki yuko kama popo si mnyama si ndege,

Mambo haya ya:
- Nimehamasishwa,
-Nimevutiwa,
- Niliona kwenye TV
-Nilisikia mahali
-Tumeshauriwa
-Tumefundishwa

Haya ndo yanayo cost watu yaani mtu haamini dream yake sasa amebakia kurukia hiki na kuacha kesho kakamata hiki.

Kinacho takiwa stiki pale unapo penda, stiki kwenye Idea yako na iamini idea yako, acha kufuata wanacho sema watu au kufanya watu, zile ni drem zao.

Watu wanakuja na Idea zao sasa wapateje pesa ndo hayo ya kuambiwa lima kile na fuga kile, na mtu bila kuwaza anaingia huko,

YOU GUYS, TRUST IDEA YAKO NA AMINI IDEA YAKO NI BORA ZAIDI
 
Mkuu asante kwa mawazo mzuri yakutujenga wajasiriamali wadogo ama wanaotarajiwa kuanzisha ujasiriamali
 
True say. I think wengi tunaiga interest za watu wengine ndomaana tunafeli
Mada za akili kubwa na tija kubwa zinasomwa na kuchangiwa na wachache.Ahsante kwa kutukumbusha makosa yetu na kutuonyesha njia za kurekebisha makosa yetu.Kama ilivyo kwenye mafanikio halisi itasomwa na wachache itatekelezwa na wachache Zaidi.
 
Mkuu kuna wajasiliamali wamevamia kambi za wengne na hii ndo husababisha mtu kuto kuwa na msimamo katika utekelezaji wa mradi husika . nimebahatika kutembelea wajasiliamali wengi ila ninacho kutana nacho huwa kinanifanya nijue walio vamia ujasiliamali ni wengi kuliko wajasiliamali wenyewe
 
Heshima kwenu Wajasiriakilimo.

Swala la Ujasirimali ni gumu sana, Ujsirimali sio swala la kitoto, unahitajika kujitoa mhanga ki sawa sawa.Wengi wamekuwa wanafanya hivyo na wengine imekuwa ni kazi ngumu.

Wengi wetu tunapenda sana mafanikio, ila ya muda mfupi na ndo yanayo pelekea haya yote yanayo tokea,
Wengi wetu hatuna spirt ya ujasirimali zaidi ya kutaka tajiri wa short cut wa kulala na kuamka tajiri, mtu anataka alime na auze anunue hata V8 ndo hayo tunawaza wengi wetu.

Sasa tumebakia kujaribu hiki na kile, yaani mtu hana ndoto tena ubongo umefikia mwisho kwenye kuwaza, yaani kama ni gari imekita haiendi mbele wala hairudi nyuma

Kufuata mkumbo kulivyo.
Utakuta mjasirimali mwenzangu alikuwa analima nyanya, kaacha ghafla halimi tena, karukia vitunguu kwa sababu alisimuliwa kuna jamaa kajenga nyumba kwa vitunguu, kalima masimu mmoja kaona hailipi kaacha, kaaza kufuga kuku wa mayai kafuga kaona hailipi kaacha, kauona kwenye TV kilimo cha ufuta kina lipa, katuafuta shamba kalima msimu mmoja kaacha, kashawishiwa afuge Broilers kafuga kama mara mbiuli kaacha, kaona kwenye TV kutengeneza sababu karukia, katengeneza kaacha, karukia kufuga Sungura kwa sababu kaambiwa inalipa.

Wakuu kwa staili za aina hii sahai mazima mafaniko, make hapa mtu anakuwa haeleweki yuko kama popo si mnyama si ndege,

Mambo haya ya:
- Nimehamasishwa,
-Nimevutiwa,
- Niliona kwenye TV
-Nilisikia mahali
-Tumeshauriwa
-Tumefundishwa

Haya ndo yanayo cost watu yaani mtu haamini dream yake sasa amebakia kurukia hiki na kuacha kesho kakamata hiki.

Kinacho takiwa stiki pale unapo penda, stiki kwenye Idea yako na iamini idea yako, acha kufuata wanacho sema watu au kufanya watu, zile ni drem zao.

Watu wanakuja na Idea zao sasa wapateje pesa ndo hayo ya kuambiwa lima kile na fuga kile, na mtu bila kuwaza anaingia huko,

YOU GUYS, TRUST IDEA YAKO NA AMINI IDEA YAKO NI BORA ZAIDI
We miss you a lot brother in A Tango what's up.
 
ni kweli na hili ndo tatizo letu Tz wepesi kukata tamaa tunataka mafanikio chap chap
 
Ujasiriamali ni dhana ambayo misingi yake mikuu ni kujifunza kila leo,kupenda unachofanya,uvumilivu wa kusubiri matokeo na ubunifu.Katika nyakati za sasa watu wamekuwa wakiingiza kwenye shughuli za uzalishaji mali kwa dhana ya ujasiriamali wakati wakitaraji mafanikio makubwa kwa muda mfupi.Kiuhalisia matokea ya ujasiriamali mara nyingi uwa yanakuja polepole na baada ya mtu kuwa amejifunza vya kutosha na kukijua anachokifanya kwa ufasaha.
Sasahivi kuna kundi kubwa la wahamasishaji wa mambo ya ujasiriamali wanafanya jambo jema lakini kinachokosekana tu ni muunganiko wa ndoto za wale wanaowafundisha na nadharia wanazofundishwa.Ikumbukwe pia hawa wamahasishaji nao wanatafuta pesa,kuhamasisha inaweza wao wanatimiza ndoto zao laki hadhira wao wanaishia kufanikisha ndoto za wahamasishaji.
Kimsingi ukianza ujasiriamali wa ndoto yako usilenge kupata faida,lengo kwanza kufanya kitu kitokee ili uweze kuleta mabadiliko au kutatua tatizo kwenye jamii inayokuzunguka.
Mwisho jitafiti mwenyewe unahobby gani,taaluma gani,kipawa gani etc tathimini katika hivyo unaweza kutumia kipi kuzalisha mali katika mazingira yanayokuzungua na hatimaye kuvuka mkoa,nchi na hata Bara.
 
Back
Top Bottom