Haya magazeti yanamuonea Magufuli au ndivyo ilivyo

Mmoja wa majaji waliohusika na hukumu hiyo (Thomas Mihayo) na ambaye alishawahi kuwa Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika, akiwa amestaafu aliulizwa na Mwandishi na akajibu kuwa Watu wanaona wameonewa lakini ni kwa sababu hawakupata fursa ya kuona ushahidi.

Alisema ushahidi ulikuwa mzito sana. Nasikia kuna Jaji mmoja Mwanamke mwanzo wa kesi baada ya kuona ushahidi wa picha toka kwa Daktari aliyewafanyia uchunguzi Watoto wale aliamua kujitoa. Nafikiri kama Mwanamke aliumia sana na akaona pengine anaweza akatoa hukumu yake kwa kusukumwa na emotions
Mkuu Kwa mtu ambaye hajazisoma hukumu hizo anaweza hisi walionewa lakini ukizisoma hukumu hizo kama una roho nyepesi unatokwa machozi jinsi watoto walivyofanyiwa
 
Kama kuna ushahidi kwamba kweli walibaka watoto wa umri wa miaka sita na nane hilo halisahemeki, labda siku ya hukumu ya Mungu lakini sio ya hapa duniani. Yaani hao ni wa kuozea kwenye jela mpaka wafe. Japo nimesema kama kuna ushahidi, isije kuwa kulikua na kizungumkuti cha kuwaonea hao jamaa. Labda jamaa hawakufanya hicho kitu, iwe kuna mtu aliwacheza na kuwambambikizia, maana nategemea hadi rais afikie kuwapa msamaha lazima usalama wa taifa walichunguza kwa kina.

Kuna makosa ya kusamehe, hata wauaji husamehewa, lakini walawiti wa watoto wadogo, bora ufie jela.
Mahakama zote ziliwaona wana hati, huu msamaha au waondolei kosa. Ushahidi pasina shaka ndiyo unaoweza kumtia hatiani mtu. Gazeti halina kosa wale ni wabakaji asilimia mia, na kwani wamwambie watakuwa watu wema?
 
Ulivyoiweka inakaa PR lakini pia umeiacha kiaina, kwanza neno mnalotumia la 'kubaka' hilo ni PR, maana kosa lilikua la kulawiti watoto. Ambalo ni mbovu sana hata zaidi ya kuua mtu, maana hao watoto kuanzia hapo waliishi maisha ya kizombi ni kama waliouawa tu.

Kuna jinsi mnaizungusha ili ionekane kama ni kosa la kubaka (rape) ya watu waliobalehe ambalo halina uzito kama kulawiti watoto wa miaka sita na nane.
Anayway kuna kitu kimoja nakubaliana na wewe, kwa rais kufikia uamuzi wa kuwaachia huru hawa, lazima kuna uchunguzi wa maafisa wa usalama walihusika pakubwa na kupata ukweli kindani ndani. Maana sioni jinsi rais anaweza kujitoa ufahamu na kuwaachia huru walawiti wa watoto waliohukumuwa na mahakama baada ya ushahidi kudhihirisha matendo yao.
Akhsante kwa masahihisho, kweli ni kulawiti sio kubaka kama nilivyoandika hapo awali.

Lakini kuhusu eti tunalizungusha ili ionekane ni kubaka badala ya kulawiti, sijui unamaanisha akina nani tunaolizungusha. Maana kama nilivyokwambia hili suala lilifikia kuwa la kisiasa hadi wagombea kulipigia kampeni za uchaguzi kwa kujua kuwa wapiga kura wengi walikuwa wanaamini kuwa hao jamaa walisingiziwa (maneno ya chini chini)

Lakini naweza kukuelewa, nadhani unamaanisha tunaomuunga mkono JPM ndo tunalizungusha suala hili. Binafsi sioni haja ya kufanya hivyo, maana haitabadilisha chochote!
 
Mtoa mada mbona hueleweki? Huamini kama walibaka? Au huziamini mahakama zetu? Au ulitaka gazeti liandikeje?

Kwanza kabisa huwa sina imani na mahakama za Kiafrika, maana zinategemea uchunguzi wa mapolis wa Kiafrika wasiokua na vitendea kazi ipasavyo na huishia kukurupuka.
Hivyo naomba iwe kwamba uchunguzi ulifanywa kindani na kugundua jamaa hawakua na makosa, lakini hayo ya kudai eti wasamehewe maana hakuna mtu asiyekua na makosa dunia hii, aisei kulawiti watoto haisameheki.
 
Mkuu Rais ni taasisi wala si mtu mmoja!! Ukisikia wanasema Rais elewa ni taasisi wala si mtu mmoja!!
Mkuu rais ni mtu mmoja tu, ndiye anayepigiwa kura na ndiye anayeapishwa, na akipatikana na kosa ndiye anayepigiwa kura na kutokuwa na imani naye, hata katika katiba ukiisoma utaona inamataja rais kama mtu mmoja, kiingereza wanatumia he/she.
 
Naomba tupate maana ya maneno haya matatu
1)Kubaka
2)Kulawiti
3)Kunajisi
Nadhani tunayachanganya, mimi kwa jinsi ninavyofahamu, kubaka ni kufanya ngono na mwanamke bila ridhaa yake, na inachukuliwa mtoto chini ya miaka 18 hawezi kutoa ridhaa, hivyo ukifanya mapenzi na mtoto wa kike inachukuliwa ni kubaka.

Mapenzi kinyume na maumbile ni kulawiti, lakini ukimfanyie mtoto mdogo kinyume na maumbile ni kumnajisi..

Kama kuna anayejua tofauti na hili ninaomba msaada.
 
Kwa uamuzi wa Rais Magufuli kuwasamehe hiyo ilikuwa haki yake kikatiba lakini kwa kuwakaribisha hawa jamaa ikulu ni big mistake kwani Mwalimu Nyerere alisema Ikulu ni pahala takatifu kwa kwa wahalifu wa aina hii pamoja na kusamehewa hawakutakiwa kukaribia ikulu hiyo.
 
MK254,
Umeuliza swali muhimu sana ambalo lingetakiwa maelezo ya kina sababu ya mhimili wa serikali/dola/ executive kuamua kuwafungulia hawa jamaa wa familia ya Nguza.

Ikiwa kama Mh. Rais na bodi ya parole n.k walipitia kesi na kuona kuna mapungufu au jambo jipya wakaona hakuna haja ya kulipeleka mahakamani kupoteza muda haki ipatikane kwa wafungwa basi wangetolea maelezo maelezo ya sababu ya kuamua kutumia ''uwezo'' wa kikatiba ambao ni sheria mama rejea.

Kwa taasisi ya Urais kuamua kuwapa 'msamaha', kunazua maswali mengi mengine ''chanya'' kuwa ''wafungwa'' hawa wa familia ya Nguza walionewa na kuna maswali mengine ''hasi'' kuwa inakuwaje ''wabakaji'' wameachiwa.

Mhimili wa Mahakama au Bunge au Serikali ina la kujifunza kuhusu uamuzi wa msamaha huu ikiwa tu sababu zitawekwa wazi na kusaidia huko mbeleni kama kuna maamuzi ya ''shindikizo/pressure'' basi mihimili hiyo itajitahii kuiepuka na kutenda haki kwa wote na muda wote.
 
Always two sides to the story...then there is the truth...Hii kesi ilinichanganya sijui niamini nini...
 
Watz bana, wabakaji ikulu? Hiyo ikulu baadaye mtakuja ifanyia maombi, hadi na mafuta ya upako humo ndani mtayamaga sana.
 
Back
Top Bottom