T-1000
Senior Member
- Feb 21, 2011
- 144
- 42
Mkuu Kwa mtu ambaye hajazisoma hukumu hizo anaweza hisi walionewa lakini ukizisoma hukumu hizo kama una roho nyepesi unatokwa machozi jinsi watoto walivyofanyiwaMmoja wa majaji waliohusika na hukumu hiyo (Thomas Mihayo) na ambaye alishawahi kuwa Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika, akiwa amestaafu aliulizwa na Mwandishi na akajibu kuwa Watu wanaona wameonewa lakini ni kwa sababu hawakupata fursa ya kuona ushahidi.
Alisema ushahidi ulikuwa mzito sana. Nasikia kuna Jaji mmoja Mwanamke mwanzo wa kesi baada ya kuona ushahidi wa picha toka kwa Daktari aliyewafanyia uchunguzi Watoto wale aliamua kujitoa. Nafikiri kama Mwanamke aliumia sana na akaona pengine anaweza akatoa hukumu yake kwa kusukumwa na emotions