Synod
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 4,092
- 4,033
Ukweli kwamba mahakama iliwakuta na hatia ya kubaka hauwezi kupingika wala kubadilishwa. Na ukweli kuwa rais aliwaachia kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na katiba pia hauwezi kubadilishwa. Lakini tukio hili linaunganishwa na ile amri yake ya kufukuza wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shule. Hapo ndo watetezi wa masuala ya watoto na haki za binadamu wanapima mzani, kumwachia mtu aliyehukumiwa kuwa kabaka halafu unamfukuza shule aliyepata ujauzito; pengine kwa kubakwa pia. Hapa panahitaji busara kweli kweli. Ndiyo maana vyombo vya habari ambavyo huwa sio vya kishilawadu hadi vya ulaya viliandika kuhusu utata huo wa matukio hayo mawili. Kuna chombo kimoja cha kuaminika kutoka huko ulaya niliona wakiandika kuwa MAGUFULI AWAACHIA HURU WABAKAJI WA WATOTO HUKU AKIAMURU WASICHANA WANAOPEWA UJAUZITO WAKIWA SHULE WAFUKUZWE.Kama kuna ushahidi kwamba kweli walibaka watoto wa umri wa miaka sita na nane hilo halisahemeki, labda siku ya hukumu ya Mungu lakini sio ya hapa duniani. Yaani hao ni wa kuozea kwenye jela mpaka wafe. Japo nimesema kama kuna ushahidi, isije kuwa kulikua na kizungumkuti cha kuwaonea hao jamaa. Labda jamaa hawakufanya hicho kitu, iwe kuna mtu aliwacheza na kuwambambikizia, maana nategemea hadi rais afikie kuwapa msamaha lazima usalama wa taifa walichunguza kwa kina.
Kuna makosa ya kusamehe, hata wauaji husamehewa, lakini walawiti wa watoto wadogo, bora ufie jela.
Ukiiangalia kauli hii huwezi kulaumu chombo hicho cha habari wala kukiita cha kishilawadu, maana ni kweli aliamuru wasichana wajawazito wafukuzwe shule, babu seya aliachiwa kwa mujibu wa sheria na mahakama ilimuona na hiyo hatia.
Lakini kama ulivyouliza kuhusu ukweli wa kutokea tukio hilo la ubakaji. Naweza kusema babu seya mwenyewe, wanawe na wale watoto wanaodaiwa kubakwa ndio wanaojua ukweli halisi wa hili tukio. Sisi wengine tunaweza kuwa tunasukimwa na emotions tu!
Shida kubwa ni kuwa suala hili linagusa maslahi ya wengi kijamii, kisiasa n.k. Wengi wanadai babu seya alionewa na alisingiziwa kwa sababu binafsi. Ilifikia hatua wakati wa kampeni za uchaguzi 2015 baadhi ya wagombea wakinadi sera zao kupitia suala hili kuwa wakichaguliwa watawaachia huru akina babu seya.
Kutokana na hayo maneno ndo maana mitazamo iko tofauti, na rais naamini kupitia washauri wake na watu wa usalama wamelifanyia kazi suala hilo. Ndo maana hata baada ya hawa jamaa kuachiwa watu wengi walipongeza hatua hiyo, maana wengi ni kama walikuwa wakiisubiri kwa hamu.