Hawa wanaweza kuoana?

Kama wazazi wanakaa kama mke na mume ( kwa maana hawajaoana bali wanakaa kama mtu na kimada wake) kwa muda mrefu BASI na hao watoto wahame tu hapo kwao na kuwekana kinyumba kama walivyofanya Wazazi wao.

Kama walikuwa bado hawajaanza kale kamchezo basi wana haki kamili kuoana.
 
Ngoja nikwambie Eiyer, kwa sisi waafrika anayelala na baba yako ni mama yako na anayelala na mama yako ni baba yako,period! Utake usitake hizo ndizo taratibu zetu za kiafrika. Jambo hili wala halina mjadala wambie hao marafiki zako wanawakosea adabu wazazi wao ,wambie waache kabisa upuuzi huo.
 
Umenena mkuu
 
Mh...Mungu awasamehe wazazi na watoto...wajipange tu kivingine watafute wengine..
 
Mimi nafikiri wanaweza kuoana hata kwa kupata baraka za wazazi wao. Uhusiano wao sio kikwazo kwa ndoa yao. Wazazi wanaweza kuwaunga mkono au la, itategemea ni kwa kiwango gani wako 'open minded' na kutambua hali halisi. Kuwazuia kuoana wawili wanaopendana inahitaji sababu zinayoingia akilini because there can be more harm than good. Mimi naona wawaeleze wazazi azma yao ya kuoana wasikilizie respose kutoka kwao. Lakini mimi ninavyofahamu wawili wakishapendana wakaamua kuoana ni vigumu kuwazuia. Naamini wazazi watatumia busara katika jambo hili.
 
Ngoja nikwambie Eiyer, kwa sisi waafrika anayelala na baba yako ni mama yako na anayelala na mama yako ni baba yako,period! Utake usitake hizo ndizo taratibu zetu za kiafrika. Jambo hili wala halina mjadala wambie hao marafiki zako wanawakosea adabu wazazi wao ,wambie waache kabisa upuuzi huo.
Nimekusikia mkuu!!!!
 
mkuu kwa mila na desturi za kiafrika hili halikubaliki kabisa....tayari hawa ni kaka na dada kwani mama na baba tayari wameshakuwa kitu kimoja..itawezekana kwa kuchakachua lakini sio mila wala desturi ya kiafrika achilia mbali hapa bongo. waache hizo tamaa zao za ngono. kwanza wazazi wao wakipata hizo habari wanaweza kupatwa na shinikizo la damu kwa mshtuko. kijana ajitahidi sana kumueleza binti kuwa yeye ni sawa na kaka yake na binti atambue hilo. tufumbue macho kitendo cha kuwa wameshafanya mapenzi...ila tukemee kitendo cha kuoana. binti anapepo la yale mambo yetu ya kikubwa afanyiwe maombi na councelling. ni hayo tuu
 
Mh! Maishani iko mitiani jamani... Vijana mpaka hapo wamekosea mila na desturi na pia wazazi wao. Hata km mnahemkaje m2 mamake akishalala na babako anakuwa nduguyo! Ila kwa msukumo wa hisia zenu mwaweza kuoana ila angalieni athari za pembeni(jamii)itawaonaje? Mtaish kwa raha bila kujali watu wanasemaje juu yenu? Mnaweza kumezea vidole mtaani vitakapokuwa vinanyoshwa kwenu? Mtakuwa na mshipa wa kuwaangalia wazazi usoni? Majibu ya haya yatakupa mwanga.
 
nadhani waende kuongea na wazazi wao kwani naona ni sawa wakioana.
wangekuwa wamelelewa tangu utoto kama dada na kaka hapo sawa.
 
Sangara thanx!!But ugumu upo hapo ndo maana hawa watu hawajui wafanye nini!
 
Hii ni another movie ya LAMORIR.....

movie(hadithi)ni zao la fasihi,fasihi ni kazi ya sanaa,na SANAA NI KIOO CHA JAMII(SIO MSANII!..LOL) kwa maana kwamba inaakisi kile kinachotokea kwenye jamii husika.mara nyingine huenda mbali zaidi hata kutabiri kitakachotokea baadae!sasa kama mkasa,tatizo,hadithi,kisa,utunzi,viwe vya kweli au vya kubuni,vimewekwa hapa na mdau maana yake vime/vili/vina/au labda vitatokea kwenye jamii yetu au kwa wenzetu.tusichukulie kwa mzaha tu kila kitu jamani heshima yetu itashuka.we changia kutokana na muono wako kwa swala husika,huna mchango kaa kimya soma ya wenzio au hama uzi kabisa!
 
Back
Top Bottom