Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislamu wenyewe kwa Tanzania...

Status
Not open for further replies.
Chama soma hoja badala ya kuleta uzushi. Naona umeanza kuthibitisha aliyosema Mtoi. Maana badala ya kuangalia nini kimeongelewa unaanza shutuma na jazba.

Taasisi ya Masheikh na wanazuaoni wa Kiislamu Tanzania imesikitishwa na mhemuko hasi na ghadhabu za baadhi ya waislamu zilizopitiliza na kupelekea kutoa mwanya wa kutendeka uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu.

Source:
https://www.facebook.com/pages/ITV-Tanzania/195736147204034
 
Bwana Mohamed Mtoi sifahamu kiwango chako cha elimu ila hiki ulichoandika kimekaa kichadema zaidi kuliko ukweli wenyewe; unataka kuniambia katika mamilioni ya waislamu waliopo Tanzania ambao hawakujaaliwa kusoma walikataa wenyewe au tu ni matatizo ya mfumo mzima uliokuwepo? Kigezo cha kusema raisi na makamu ni waislamu hakina mshiko; tatizo lipo na ni kubwa sana lisipofanyiwa marakebisho litakuwa ni balaa kubwa kwa taifa letu; yapo matatizo yamechangiwa na waislamu wenyewe na yapo ambayo serikali imechangia kwa kiasi kikubwa; hii hoja yako ya kusema tatizo hulioni ni mtazamo wako ambao umeliangalia kwa kiwango cha muuza kahawa.

Chama
Gongo la mboto DSM

Sitegemei kutoka jambo jema huko....!!
 
Nimeusoma kwa makini sana huu ujumbe; nimejifunza vitu vingi sana vizuri ndani ya Uislam. Sikuwahi kuwaza hata siku moja kuwa ndani ya Uislam kuna watu wenye HEKIMA na UWEZO mkubwa wa kuchanganua mambo Kama yalivyo kwenye mada hii. Well said.

Kama hii ni mada unayofikiria ni ya kiwango cha juu sana iliyotolewa na muislam, basi nakupa pole. Lakini sishangai ndio uwezo wa vijana wa vijiweni kufikiri. Hata hivyo umejitahidi sana mpaka ukausoma ujumbe wote, huwa si kawaida kwa vijana wa vijiweni. Ama kweli huu ujumbe umekupendeza.

Nasisitiza kuwa sikushangai maana mawazo yako yote yapo kwenye maneno yako kama nilivyoya nukuu:.... "Freedom is Comming Tomorrow" Na usipokuwa huru hata uwezo wako wa kufikiri ni mdogo. Endelea kujifariji.
 
Bwana Mohamed Mtoi sifahamu kiwango chako cha elimu ila hiki ulichoandika kimekaa kichadema zaidi kuliko ukweli wenyewe; unataka kuniambia katika mamilioni ya waislamu waliopo Tanzania ambao hawakujaaliwa kusoma walikataa wenyewe au tu ni matatizo ya mfumo mzima uliokuwepo? Kigezo cha kusema raisi na makamu ni waislamu hakina mshiko; tatizo lipo na ni kubwa sana lisipofanyiwa marakebisho litakuwa ni balaa kubwa kwa taifa letu; yapo matatizo yamechangiwa na waislamu wenyewe na yapo ambayo serikali imechangia kwa kiasi kikubwa; hii hoja yako ya kusema tatizo hulioni ni mtazamo wako ambao umeliangalia kwa kiwango cha muuza kahawa.

Chama
Gongo la mboto DSM
Hivi unafahamu watu wenye akili mgando kama hizi za kwako hata huyo Ibilisi atakukana siku ya mwisho? Serikali ni ya CCM na ndiyo unasema inadhulumu haki za Waislamu, halafu wewe huyo huyo ndiyo mshabiki mkuu wa CCM, sasa ni kwa nini tusiseme chama ni adui wa Uislamu?
 
Last edited by a moderator:
Bwana Mohamed Mtoi sifahamu kiwango chako cha elimu ila hiki ulichoandika kimekaa kichadema zaidi kuliko ukweli wenyewe; unataka kuniambia katika mamilioni ya waislamu waliopo Tanzania ambao hawakujaaliwa kusoma walikataa wenyewe au tu ni matatizo ya mfumo mzima uliokuwepo? Kigezo cha kusema raisi na makamu ni waislamu hakina mshiko; tatizo lipo na ni kubwa sana lisipofanyiwa marakebisho litakuwa ni balaa kubwa kwa taifa letu; yapo matatizo yamechangiwa na waislamu wenyewe na yapo ambayo serikali imechangia kwa kiasi kikubwa; hii hoja yako ya kusema tatizo hulioni ni mtazamo wako ambao umeliangalia kwa kiwango cha muuza kahawa.

Chama
Gongo la mboto DSM

mkuu mi sikubaliani na wewe mi naona tatizo sio mfumo, mfumo haupendelei wakristo na kugandamiza waislamu wala haupendelei waislam na kugandamiza wakristo ila waislam walio wengi wanahitaji mapinduzi ya kifikra kutoka katika fikra za kulaum ukristo na badala yake wawe na fikra za kujiendeleza ktk nyanja mbalimbali kuanzia nyanja ya kiuchumi, kielim, kisiasa na kijamii. mi naona kuna haja hata ya kubadili mitaala ya mafuzo ya vyuo vya madrasa kwa kufundisha watoto kuwa na upendo na umoja na watu wote na kuondoa mafunzo yanayowatenga waislam na watu wa dini nyinginezo. Mtoyi nakupongeza kwa makala yenye mafunzo mema
 
Mkuu chama,
Waende Makete, Njombe, Makambako, Ngara, Karagwe, Ivinza, Namtumbo, Kibosho, Karatu, Arumeru, Igunga, Tarime, Rorya, Mwitongo, waone watu walivyochoka hakuna cha Mkiristo wa Muislam waya mtindo mmoja.

Ndio wote wamechoka, lakini kidogo kilichopo tugawane wote. Nafikiri umenielewa kabla sijaendelea.
 
mkuu mi sikubaliani na wewe mi naona tatizo sio mfumo, mfumo haupendelei wakristo na kugandamiza waislamu wala haupendelei waislam na kugandamiza wakristo ila waislam walio wengi wanahitaji mapinduzi ya kifikra kutoka katika fikra za kulaum ukristo na badala yake wawe na fikra za kujiendeleza ktk nyanja mbalimbali kuanzia nyanja ya kiuchumi, kielim, kisiasa na kijamii. mi naona kuna haja hata ya kubadili mitaala ya mafuzo ya vyuo vya madrasa kwa kufundisha watoto kuwa na upendo na umoja na watu wote na kuondoa mafunzo yanayowatenga waislam na watu wa dini nyinginezo. Mtoyi nakupongeza kwa makala yenye mafunzo mema

Acha kubwabwaja bila kufahamu. Hivi unajua katika ujenzi wa Mahospitali na mashule hususan vyuo vikuu vya S. t Joseph pesa inatoka wapi. Nijibu hilo kabla sijaendelea. Kifupi katika ule mkataba wa MoU, pesa inatoka wapi.

Huwezi ukamruhusu mmoja apewe pesa kibao na wafadhili na mwingine ukamfungia. Ukilielewa hilo ndio utaelewa nini maana ya Mfumo kuwa kigezo cha udidimizaji.
 
Mkuu chama,
Nimemsoma Mwana Mtoka Pabaya, kaandika vitu vingi sana lakini 97% ya bandiko lake ni hadithi za bulicheka na mke wake Elizabeti...kuna sehemu anasema Waislam wanazaa sana wake 3 watoto 11 huwezi kuwasomesha kama ni hivyo kwa nini kwenye sensa Wakiristo wanasema wao wapo wengi.

Kuna sehemu tena anajichangaya anasema Waislam wataishia kuwa mafundi koroboi, narudia maneno yangu mtaani mbona wote wamechoka tu wanataka kujiaminisha Wakiristo hawana shida..

Halafu anashauri tusomeshe watoto wetu bibilia.

Ikiwa mimi ni Bulicheka wewe utakuwa marehemu, tena wa miaka mingi ambaye mifupa yake haibebeki tena kwani inamomonyoka. Shida ya itikadi zenu ni kupenda kuandaa ubishi kabla hujaelewa mtu anazungumza nini. Unatumia energy kubwa kuandaa ubishi badala ya kujaribu kupata point.

Kubisha na FACTS ni ujinga uliotukuka. Nenda katika jamii za Kiislamu fanya utafiti na sio kubishana kienyeji. Mimi nilizungumzia Birth Rate peke yake, lakini wewe umerukia kwenye Population.

Mkuu Ritz, mimi sio wa level yako linapokuja suala la kufikiri. Na usikurupuke siku nyingine ukajaribu kudhania kuwa na mimi nakurupuka. Birth Rate sio ndio determinant factor pekee ya population. Kumbumka mimi nilisema wanazaa sana, lkn sikusema mpo wengi. Yanzingatie haya kabla hujaja na blah blah zako:

1. watu 10 wakizaa watoto 11@ hawawazidi wingi watu 30 wenye watoto 4@
2. Nilizungumzia Birth Rate inavyoathiri makuzi na malezi lakini sikugusia Death Rate. Hilo nalo lina nafasi unapozungumzia population.
3. Hakuna sehemu nimesema Wakristo hawana shida. Shida ipo hususan vijijini lkn sisi tunazitizama shida zetu kama changamoto na hatukumsingizii mtu. Palipo na tatizo, tunaweka shule mambo yanabadilika.
4.
Halafu anashauri tusomeshe watoto wetu bibilia.
Haya ndio mavuno ya upumbavu wa kupenda kuandaa hoja za kubisha kabla hujaelewa mtu anazungumza nini. Hakuna sehemu nimesema muwafundishe watoto wenu Biblia. Nilichokuwa nazungumzia pale ni namna ya ufundishaji. Kutoelewa kwako ni dalili kuwa ulisoma madrassa na ukawa ukibondwa kichwani kila unaposhindwa kukariri jambo.

Na mwisho nikushukuru kwa kunifumbua macho. Siku zote unafiki huleta maafa zaidi ya faida. Kumbe kigezo cha kusema mpo wengi ni fact kwamba mnazaa sana! Mkuu Ritz, punguza unafiki.

Kama leo tuna watu wapo mahabusu kwa makosa ya uvunjifu wa amani, uharibifu wa mali na wizi uliofanywa ndani ya makanisa, kwa kauli ya kutafuta kuonekana wema tukasema kuwa "wale sio waislamu bali ni wahuni tu, muislamu hawezi kufanya vile kwa kuwa uislamu haufundishi wizi na fujo", je wahalifu hao na wengine wenye tabia kama zao tunapohesabu sensa wahesabiwe kama waislamu au lah?
(Mkuu chama, hili swali linakuhusu pia)
 
Last edited by a moderator:
Michango hii ya hawa Watanzania wenzetu Waislam, imenigusa sana. Na kama akina Ponda wangekuwa wanakuja na hoja kama hizi, hakika sisi watanzania wote kama Taifa tungeungana na kuona ni namna gani Watanzania wote tunaweza kuungana na kuona namna iliyo bora ya kuwasaidia wenzetu hawa waislam, kama kundi mojawapo katika jamii yetu. Maana mafanikio ya Mtanzania yeyote ni mafanikio yetu kama Taifa.

Nina imani hata viongozi wa makanisa wangekuwa tayari kushirikiana na viongozi wa kiislam kuwapa uzoefu wao katika uendeshaji wa taasisi mbalimbali za huduma na za kiuchumi. Lakini mambo haya hayawezi kutokea kwa kuchochea chuki.

Ni ukweli ulio wazi kuwa makanisa, na hasa kanisa katoliki wana uzoefu mkubwa sana wa kuendesha huduma na miradi mingi ya kiuchumi kuizidi hata serikali. Na hii inathibitishwa na ukweli kuwa KANISA KATOLIKI NDIYO TAASISI TAJIRI KABISA KULIKO TAASISI ZOTE DUNIANI. Kwa hiyo waislam wasilitazame kanisa Katoliki Tanzania kuwa limekuwa na miradi mingi eti kwa sababu linawanyonya waislam au waumini wa dini nyingine. Mizizi yake ya kulifikisha hapo lilipo imetoka mbali sana na lina uzoefu mkubwa uliopatikana kwa miaka mingi.

Nakubali kuwa kuna waislam wengi sasa hivi ambao ni wasomi wazuri lakini au hawashirikishwi kuwasaidia waislam wenzao au hawataki kushirikiana na waislam wenzao, wamewaacha watu wenye upeo mdogo wawaongoze waislam, na matokeo yake, kazi kubwa wanayofanya ni kueneza chuki na kutokufanya chochote kuwasaidia waislam katika maisha yao ya kila siku.

Waislam wanahitaji kujifunza kutoka kwa mataifa kama Uturuki ambayo yana waislam zaidi ya 90% lakini hawana mambo ya kipuuzi, na wameamua kuondoa hata baadhi ya mambo ambayo wanayaona ni ya kipuuzi au si ya lazima japo yamekuwepo katika mafundisho ya uislam kwa miaka mingi. Kwa mfano, sheria ya Uturuki hairuhusu mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja, na ni more strict kuliko hata ilivyo kwa mataifa ambayo yana wakristo wengi.

Nashauri kuwa, ili kuepuka madhara mabaya zaidi kwa Taifa letu, kwa uislam na waislam wenyewe, huu ni wakati ambao ni muhimu kuhakiksha taasisi za dini ya kiislam zinaongozwa na watu wenye kiwango kizuri cha elimu, upeo mpana, mwono wa kimaendeleo na ubunifu, wenye nia ya kujitolea, n.k. Kunahitajika mapinduzi makubwa ya ndani katika taasisi za kiislam. Wanatakiwa kuanzia wapi, sina uhakika. Kwangu mimi sioni kama ni lazima sana kiongozi mkuu wa Bakwata awe na PhD au Masters degree, lakini asiwe na elimu chini ya degree lakini awe na upeo mpana na karama ya uongozi.

Tatizo kubwa jingine ya Waislam, sioni kama wana mfumo wa uongozi unaoeleweka. Kuna vikundi vingi ambavyo haijulikani vinaripoti kwa nani, na nani ana uwezo wa kuviwajibisha. Hata katika makanisa, lazima kuna wakorofi lakini tofauti na waislam, wakristo wana mifumo ya kiuongozi ya kuwajibisha au hata kuwafukuza wanaotenda kinyume ya miongozo iliyowekwa. Kukosekana kwa mifumo hiyo, imesababisha kufanya mambo ya aibu hata misikitini kiasi cha kufikia hata baadhi ya viongozi wa waislam kucharazwa bakora na waumini wao. Yanapotokea mambo kama hayo, uislam kwa ujumla unadhalilika.



Tatizo letu waislam ni kua hatutaki kubadilika. Sitegemei Mufti wa darasa la Saba aweze kuja na vision + mission ya kuipeleka Bakwata mbali kama afanyavyo Doctor Alex Malasusa.

Mi nimesoma A-Level Islamic Seminary, yaani ni bora ukwepe darasa unaweza kupona kuliko kukwepa sala. Watu wanajengwa kiimani zaidi kuliko kidunia, no balances.

Pia kuna tofauti kubwa ya uendeshaji wa taasisi zetu tofauti na wenzetu. Tukijiuliza Mufti wetu anawajibika kwa nani nje ya nchi, jibu hakuna. So akiboronga hakuna wa kumsimamia maana ye ndio Top. But wenzetu mfano Waroma, wao wanawajibika Vatican, hivyo no ujinga ujinga wa kiuongozi.

Sambamba na hilo, hao wakubwa zao wa nje wanawapa musaada mbalimbali, ndio maana kila siku vigango, parokia, usharika n.k. vinafungulia na kuanzishwa. Sisi wakubwa zetu wa kutupa misaada wako wapi? Ni kina nani?

Pia utakuta hata sera ni tofauti. Wenzetu wanatafuta pori a.k.a msitu, wanafyeka na kuweka mission hapo. Hapo zitapatikana shule, hospitality, other economical activities e.t.c, sisi hatuna akili hiyo.

Mimi ukiacha A-level, shule zingine zote nimesoma na hawa ndugu zangu, yaani Waislamu wenzangu nafanya kuwahesabu, wako wapi wengine?? Hawakuchaguliwa? Au hawakuomba? Wali-qualify? Why?

Hivi kuna sababu zozote za kisayansi zinazofanya mtoto awe/asiwe na akili just because of dini yake?? Nikichora graph ya waislamu nlioanza nao primary walioacha shule mpaka nimemaliza shahada ya pili, pyramid ni Kali sana? Where are others??

Fanya research fupi tu;
Pitia kituo cha daladala anza kuuliza jina wale mateja wa pale, utaambiwa Dullah, Muddy, Ally, Ramso and the like. Toka hapo upitie mahakama za chini ambazo kesi mbalimbali kama za wizi wa kuku, kutukanana, kupigana, n.k. zinahukumiwa, majina ni hayohayo.

Tumeshakosea, tufanyeje sasa??
Real inahitajika debate then utekelezaji on this issue.
 
Kwa kweli hayo yote yaliyosema hapo juu ni haki na kikubwa kwa Waislamu ni kuwa ........ONLY EDUCATION will take you whre you want to be.............ila tuu kwa kuzingatia mafunzo ya mtume wetu, tutafiak mabl;i zaidi kwani JAZBA na kejeli kwa wengine itainya imani yetu ionekane kama ya kukosekana kwa USTAARABU wa Uvumilivu na stahaha ya IMANI kwa awaye yote.
Hebu fikiria wenzetu wakristo wao ni Kanisa.......pembeni CHEKECHEA.....dipensary na hata shule za ufundi wowote kwa WAUMINI WAO........sisi kimetushinda nini wakati UISLAMU ndo wakwanza kutua huku kabla ya UKRISTO.......!!!!!
hebu angalia sehemu zote za kwanza kwa Uislamu ni Vyuo vingapi vipo ........sekondari ngapi na hata hospital ngapi...
Angalia wenzetu...........tukianza na huko Kilimanjaro.....Marangu...Ashira kuna kanisa la kwanza toka enzi hizo na pana shule ya Msingi na Sekondari na mita chache tuu ni Chuo cha kwanza cha Ualimu......wafanya wao walioleta huo Ukristo na ndoo maana watu wa huko ni WASOMI na ..........Machame.......kuna kanisa na pembezoni ni Hopsital kubwa na chuo cha Udakitri kipo hapo na sekondari kwa ajili ya Watoto wa Kike ambo ndugu zetu waislamu wa machame watoto wao walisoma huko.
Angalia huko Peramiho...........uatajua mengi kuhusu hawa watu WAKRISTO na juhudi zao za ELIMU.
Usiende mabi hapa DAR.......huko pugu ni wamisionari walianzisha eneo lile la PUGU seondari na maendelo yake.
Bagamoyo jeeee............Kondoa JEEEEE...........Kigoma jeee.........Kilwa jeee.....
ELimu ndugu zangu ndo muhimu .
 
By Ritz Mkuu chama,
Waende Makete, Njombe, Makambako, Ngara, Karagwe, Ivinza, Namtumbo, Kibosho, Karatu, Arumeru, Igunga, Tarime, Rorya, Mwitongo, waone watu walivyochoka hakuna cha Mkiristo wa Muislam waya mtindo mmoja.

Hapo kwenye bold utakuwa una wazimu wewe sio bure.

Hapo kwenye red yaweza kuwa sahihi kwa kiasi fulani, na hii ni kutokana na tabia ya Wajaluo kuoa wake wengi, kurithiana n.k. Kwa hiyo unaweza kuona jinsi ndoa za kurundikana zilivyo kikwazo. Hayo maeneo mengine sina hakika, lkn nakuhakikishia kuwa hayawezi kuwa yamechoka kama Mafia
 
Asante sana ndugu Ritz, na haya ndio nilitaka ndugu yetu Mohameh Mtoi ayaelewe. Na hata kama hakuyasoma katika maisha yake, itakuwa ni kwa sababu ya ule uadui wa uislam namba 1 alioutaja 'Elimu ndogo'. Kwa hiyo kwa hili naye ni muathirika, ni vyema tukiwa pamoja kupambana na adui yetu.

Lakini Mohamed Mtoi huwezi kupambana na adui yako mpaka umjue ni nani. Nikiwa na maana yule aliyekupa pingamizi katika njia zako. Kazi kubwa kwako Mohamed Mtoi ni kumtafuta huyo adui. Muhtasari huu wa ndugu Ritz utakusaidia kumjua adui yako.

Narudia, Asante sana ndugu Ritz, Mwenyeezi Mungu Akujalia na akuongezea nguvu ya kuwaelimisha Waislam wasiojua chanzo cha matatizo yao.

Mimi naamini adui wa kwanza wa Uislam, NI WALE WAISLAM WANAOMFAHAMU ADUI YAO NA WAKAAMUA KUNYAMAZA AU KUJIPENDEKEZA NA KUPINDISHA UKWELI.

Ni jambo la ajabu sana kuwa hii Taasisi moja ambayo amekuwa akiimba Mohamed Said kwenye vitabu vyake ndo ilikuwa mwarobaini wa matatizo ya waislam wa Tanzania, ni ajabu sana. Hakuna ushahidi wa kitaalam unaoonesha kuwa taasisi hii pekee ndo ingekuwa suluhisho la matatizo yote tunayoyaona leo. Hata bakwata ingevunjwa miaka hiyo, leo hii watu kama hawa Mohamed Said na wafuasi wake wangekuwa wakilalamikia kuvunjwa kwa Bakwata kama tatizo kuu lilitoleta balaa kwa waislam.

Binafsi nimezaliwa na kukulia katika mazingira yenye waislam wengi na hadi leo ninao ndugu wengi waislam. Siwezi kusema kuwa wale ambao wameshindwa ni kwa sababu kulikuwa na mpango maalum wa kuwafanya washindwe; inaonekana kuwa kushindwa kwa mtu hakuhusiani sana na dini yake, bali mtu mwenyewe. Swali ambalo limekuwa likiulizwa bila majibu ni kuwa kwa nini waislam wengi hawaonekani katika vyuo vikuuu na taasisi za elimu? Wengi kama kina Zawadi Ngoda na Kina Mohamed Said majibu yao ni kuwa waislam wanahujumiwa na wakristo. Hili ni jibu rahisi kwa maswali magumu.

Hakuna ushahidi wowote wa kitaalam unaoonesha kuwa wakristo wanafanya vizuri kielimu kwa sababu ya kupendelewa au mkono uliojificha unaowahujumu waislam. Naamini kuna watanzania wengi (Nikiwamo mimi) ambao wangeshavujisha siri ya mpango huo kwa waislam. Hili suala la watu kusoma unaona ni suala la mahali zaidi mtu anapotoka kuliko dini yake na lina misingi yake katika historia yetu kuliko kitu kingine chochote. Yaani unaweza kutoa mfano tu kuwa wale wanaotoka mikoa ya kaskazini hasa Kilimanjaro; awe mwisalmu au mkristo nafasi zao za kusoma zilikuwa sawa na utawakuta sehemu nyingi sana. Bahati mbaya mikoa hii wakaazi wake wengi ni wakristo, lakini ukichukua takwimu za waliosoma katika mikoa hiyo; uwiano wa dini zao kwa kisomo unalingana na uwiano wa uwingi wa watu kwa dini zao. Najua hapa swali kubwa litakuwa, takwimu hizo umezipata wapi? Jibu langu ni utafiti binafsi. Wale wanaotoka mikoa ambayo tokea huko nyuma haikuwa na shule za kutosha (kama Kigoma, Tabora, Singida) n.k. hawakusoma wote wakristo kwa waislam. Mbona hatulalamikii wakristo wa Kigoma, Tabora, Singida, Rukwa, n.k. ambao hawakusoma, ila tunalalamikia kutosoma kwa waislam na hasa macho yetu yakiwa yanatazama zaidi mikoa ya pwani kwenye waislam wengi? Hao wakristo wanaosemwa wengi ni wa Kilimanjaro, Kagera na Mbeya zaidi sana.

Kwa hiyo ukitaka kulaumu mfumo unaowapendelea watu na kuwahujumu watu wengine, ni wazi kuwa mfumo huo ulikaa zaidi kimikoa kuliko kidini. Kwa hiyo mimi sitaridhika kina Mohamed Said na wafuasi wao kina Ponda wanapolalamikia wakristo; kuwa ndo wanaowahujumu waislam; naomba kama kweli wana chembe ya uzalendo wawatetee si waislam tu, bali hata wakristo wanaotoka katika mikoa ile ambayo inaitwa mikoa ya pembezoni. Naamini kabisa kuwa uzalendo si nia yao na kupigania haki za waislam si nia yao; bali lengo ni kupata vyeo kwa kutumia mwavuli na kisingizio cha uwiano wa Kidini.

Sasa nije hili la vurugu za Zanzibar, Kariakoo na uvunjaji wa Makanisa huko Mbagala. Inawezekana mpo watu ambao mnaamini kukwa Sheikh Ponda na Kina Mohammed Said (kina Zawadi Ngoda na wengineo mnaamini hivyo) wanapigania haki za waislam. Lakini kwa mtu yeyote mwenye macho ya kuona na akili ya kufikiri atajua kwa uhakika kabisa kuwa kilichotokea katika maeneo hayo kina malengo ya kisiasa zaidi kuliko kupigania haki za waislam. Uamsho Zanzibar ni siasa zaidi kuliko dini na ni bahati mbaya sana kuwa ukitumia dini (uislam) ni rahisi kuvuta wafuasi lukuki. Aina ya uislam ambao mimi nimekulia katikati yao ni uislam wenye kutumia busara. Haiwezekani asilani kwa tukio la watoto hao lianzishe vurugu za kiwango kile. Mihadhara ya Sheikh Farid huko Zanzibar ni Muungano zaidi ambalo ni suala la kisiasa.

Nimalizie kwa kusema kuwa nchi yetu ina matatizo mengi. Uwiano alijaribu sana kuutetea mwalimu Nyerere; kupitia sera yake ya Ujamaa na Kujitegemea. Bahati mbaya sana mafanikio yake ndo wale wasioona mnayoyatumia kama fimbo ya kumpigia - Yeye mwenyewe alisema kuwa katika yale waliyofanya, tunachukua yale ya kijinga na kuhoji yale ya msingi tuliyopaswa kujifunza. Mfumo mpya tuliomo, ni mfumo wa Ubepari. Ubepari haujali historia imekutupa wapi, ubepari unajali sana uwezo wako wa kushindana katika soko la wazi, soko la kidunia. Ieleweke kuwa wakati tunapambana wenyewe kwa wenyewe kwa kuangalia kichwani umevaa nini, tulipo sasa ni mahali ambapo hata serikali yetu ina "limited Power" ya kubadirisha mambo. Uchumi wetu tayari unashikiriwa na makampuni makubwa ya kimataifa ambayo hata kama hatutaki yataendelea kufanya kazi katika nchi yetu. Tutaendelea kupigana huku wenzetu wakibeba kila kinachowezekana, tutakapomaliza kupigana, tutajikuta kumbe tulikuwa tunapigania kisichokuwepo.

Tofauti zilizopo kielimu haziwezi kusahihishwa kwa kupambana na watu ambao hawakuzileta hizo tofauti. Tunaweza kufanya juhudi za makusudi za kuweza kurekebisha hali hiyo. Juhudi za Makusudi hizo ni pamoja na serikali kutekeleza wajibu wake. Mapambano yetu inatakiwa tuyaelekeze serikalini kuhakikisha kuwa Rushwa, Ufisadi, Utumiaji Mbaya wa Madaraka, n.k. vinaondoka na mahari pake panachukuliwa na Utawala Bora wenye kuwajibika kwa watanzania wote bila kujali dini zao.
 
Kwa kweli hayo yote yaliyosema hapo juu ni haki na kikubwa kwa Waislamu ni kuwa ........ONLY EDUCATION will take you whre you want to be.............ila tuu kwa kuzingatia mafunzo ya mtume wetu, tutafiak mabl;i zaidi kwani JAZBA na kejeli kwa wengine itainya imani yetu ionekane kama ya kukosekana kwa USTAARABU wa Uvumilivu na stahaha ya IMANI kwa awaye yote.
Hebu fikiria wenzetu wakristo wao ni Kanisa.......pembeni CHEKECHEA.....dipensary na hata shule za ufundi wowote kwa WAUMINI WAO........sisi kimetushinda nini wakati UISLAMU ndo wakwanza kutua huku kabla ya UKRISTO.......!!!!!
hebu angalia sehemu zote za kwanza kwa Uislamu ni Vyuo vingapi vipo ........sekondari ngapi na hata hospital ngapi...
Angalia wenzetu...........tukianza na huko Kilimanjaro.....Marangu...Ashira kuna kanisa la kwanza toka enzi hizo na pana shule ya Msingi na Sekondari na mita chache tuu ni Chuo cha kwanza cha Ualimu......wafanya wao walioleta huo Ukristo na ndoo maana watu wa huko ni WASOMI na ..........Machame.......kuna kanisa na pembezoni ni Hopsital kubwa na chuo cha Udakitri kipo hapo na sekondari kwa ajili ya Watoto wa Kike ambo ndugu zetu waislamu wa machame watoto wao walisoma huko.
Angalia huko Peramiho...........uatajua mengi kuhusu hawa watu WAKRISTO na juhudi zao za ELIMU.
Usiende mabi hapa DAR.......huko pugu ni wamisionari walianzisha eneo lile la PUGU seondari na maendelo yake.
Bagamoyo jeeee............Kondoa JEEEEE...........Kigoma jeee.........Kilwa jeee.....
ELimu ndugu zangu ndo muhimu .

Kwa maoni haya, Uislamu wako utatiliwa shaka.
 
Soma kwenye article ya mtoi kipengele #3 & 4 lengo lake hasa ni kutaka kuipaka matope CCM tatizo la mfumo uliopo ni la kurithi tangu serikali ya kikoloni na yamekuwa yakiendelezwa siku hadi siku; hakuna wa kunitumia sina shida ya maisha kidogo nilichonacho namshukuru Mungu; nimeongea kwa mtazamo huru; kama kuna kitu hukubaliani nacho njoo mjadala tutaelemishana kadri ya uwezo wetu; lengo ni kuhahkisha Tanzania hatuingii kwenye mtego wa wavaa mabomu tunataka amani ya kudumu. Usiogope kuulizana viwango ni kawaida kwa wajadili mada.

Chama
Gongo la mboto DSM

Huyu Mohamed Mtoi achana naye, kaleta Thread halafu mwenyewe kaingia MTINI. Kuna maswali mengi anahitajiwa kujibu hapa barazani yeye kakimbia, na wanaojibu ni watoto wa vijiweni. Kwa hiyo mjadala si mtamu kama vile nilivyoufikiria, vyema nikaangalie TENIS kuliko kumsubiri huyu mtoa mada.

Huy alitaka umaarufu tu hapa JF KAUPATA, usishangae kusikia kesho ANATANGAZA DHAMIRA YAKE YA KUGOMBEA URAIS. Kwa vile Kabwe kanuka, huwenda wakampa nafasi hiyo. Subiri nimpigie simu Mh Slaa!
 
Umeainisha vizuri sana ndg.Waislamu wote wangepata nakala hii,nadhani wangebadili fikra na kuachama na maandamano yasiyo na manufaa na badala yake kufanya kazi kwa bidii zaidi
 
Maswali magumu yanapojibiwa kwa majibu mepesi yasiyo na chembe ya utafiti wa kihistoria ni kujipumbaza. Ndio maana wanazuoni wanabarizi upya historia halisi ya mapambano ya kupigania uhuru ambao baadhi ya waliopumbazwa wanaaminishwa kuwa mapambano ya kudai uhuru eti yaliasisiwa na Julius Nyerere; kwao harakati za majimaji, Mirambo, Mkwawa nk si kitu chochote.

Hata historia ya mapinduzi ya Zanzibar iliyoaminishwa miaka nenda rudi si sahahi..kama wabisha bofya zanzibar revulution 1964 katika google uone video halisi ya kilichojili siku hiyo ambao mamluki kutoka mashamba ya mkonge ya Tanga walivyovamia zanzibar na kuanza kutekeleza kile ambacho hivi sasa kinaiitwa mauaji ya kimbari.

Pia dhana ya uwepo wa mfumo kristo ni kimeo ambacho kutokana na ukweli wake si rahisi kufutika kwa kauli rahisi za kujiridhisha binafsi...ulikuwepo na upo, hivi sasa unajadiliwa zaidi kwa vile watu wameamka kutokana na utandawazi na uhuru wa mpana wa kutoa maoni na kupata habari, na tatizo hilo haliwapati waislamu tu kwani hata wakristo wasio wakatoliki wamekuwa wakiathiriwa kwa namna moja ama nyingine.

Kwa upande mwingine hata kwenye pumba lazima kuwe na punje chache za mchele:... Waislamu wanaobweteka na kudhani kuwa hatma ya maendeleo yao imo mikononi mwa wengine, ndio wengi hapa nchini na ukanda wa afrika mashariki. Sababu ni za kihistoria: Waarabu walioleta Uislamu upande huu walitoka maeneo ya nchi za emarati km oman nk ambao wamekubuhu kwa umwinyi. Kwa bahati mbaya usilamu uliopokelewa ulipokelewa na umwinyi ambao si sehemu ya mafundisho ya uislam.

Ndio maaana utakuta dhana ya kujiendeleza na kujitegemea katika kujiletea maendeleo haina mashiko...kwao tegemeo ni wafadhili; tofauti na nchi za kiislamu km Pakistan, Iran, Uturuki ambao ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kiuchumi na kiteknolojia hadi nyingine kuwa miongoni mwa the super power kwa kufanikiwa kuunda mabomu ya Nyuklia. Nini Cha Kufanya: Kwanaza waislam wajivue gwanda na kujitambua kuwa hatma yao imo mikononi mwao.

Waache umwinyi, wajibidishe katika kusoma elimu zote mbili za dunia na akhera na washiriki kwa uwezo wao kuchangia hatakati za maendeleo yao...wakati wa kutoa sadaka ya thumni misikitini si wakati wake bali watambuane na wahimizane kutoa michango kulingana na nguvu zao za kiuchumi.

Tujifunze kutoka Waislamu wa Machame Moshi. Sanjari la hilo michango yote iratibiwe kwa uwazi na kutolewa taarifa za matumizi yake zitolewe kwa waumini mara kwa mara. Wadumishe amani na upendo miongoni mwao na wenzao wa dini nyingine. Na wasikubali kutumiwa kama dodoki la kuwapeleka waroho wa madaraka katika kupata uongozi, hata km wanaahidiwa pepo ya hapa duniani kwani uzoefu unatoa picha tofauti. Na kila Muislamu ajihoji ameifanyia nini dini yake katika mathalani kipindi cha mwaka mzima, mwezi hata wiki moja!
 
ni jambo la ajabu sana kuwa hii taasisi moja ambayo amekuwa akiimba mohamed said kwenye vitabu vyake ndo ilikuwa mwarobaini wa matatizo ya waislam wa tanzania, ni ajabu sana. Hakuna ushahidi wa kitaalam unaoonesha kuwa taasisi hii pekee ndo ingekuwa suluhisho la matatizo yote tunayoyaona leo. Hata bakwata ingevunjwa miaka hiyo, leo hii watu kama hawa mohamed said na wafuasi wake wangekuwa wakilalamikia kuvunjwa kwa bakwata kama tatizo kuu lilitoleta balaa kwa waislam. ......


kwakweli nimependa maoni yako tanzania mbele daima! Maslahi mengine yatafuata
 
Katikati ya mjadala, mmoja wetu anaingiza u-chadema. Hili ndo tatizo letu.
Tuijadili hoja ya mwenzetu: kwa nini waislam wapo nyuma sana, kwamba tangu tupate uhuru mwaka 1961, ni hivi karibuni ndo wanampata Jaji Mkuu wa kiislamu, eti serikali ndo iliyowakandamiza.
Swala au jibu hapa ni rahisi. Ni nini mfumo wao wa elimu? Je Rais anakuwa na wigo mpana wa kumchagua amtakaye? kama wigo ni mdogo kwa nini?
Kwa maoni yangu, tangu tupate Uhuru wenzetu waislam (maana mimi ni Mkristo) mfumo wao wa elimu uliegemea zaidi elimu akhera kuliko dunia. Lakini mambo yanayokuja kutawala uendeshaji wa dunia hii (Siasa,nk) ni elimu dunia ndo hushika nafasi.
Sidhani kama rais wa nchi anapotaka kumteua msaidizi wake ataangalia vigezo vya mtu mwenye upeo mkubwa wa elimu Akhera.
Wakati mfumo wa elimu wa kikristo humwandaa mtoto na elimu sayansi tangu akiwa nursery school, waislam, aghlabu humpeleka mtoto katika madrasa, na hapa si nia yangu kubeza elimu ya madrasa, nk, bali lazima kuwe ni uwiano mzuri kati ya elimu mbingu na elimu sayansi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom