Elections 2010 hatusemi kama JK hakushinda ila tunataka,,,,!

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Kusema kweli watu hawapingi ushindi wa CCM au tuseme ushindi wa Jakaya Kikwete au Sheni ,wananchi kwa ujumla wanataka kitangazwe kile kilichopatikana kwa uhakika bila ya kumpendelea mwananchi yeyote yule aliegombea nafasi awe mbunge ,Raisi ai Mwakilishi na hata diwani.

Hakuna sehemu yeyote ile hapa Tz katika uchaguzi uliopita juzi jana ambako hakukutokea matatizo ,uchaguzi huu ulianza kutayarishwa miaka mingi iliopita naweza kusema miaka mitano iliyopita ,iweje leo majina ya watu hayaonekani,ya huku yamepelekwa kule ,huu kama si ujinga ni kitu gani ,au utakuwa wizi kama wengi tunavyofikiria.

Machafuko yote na upumbavu wote uliotokea umesababishwa na tume hizi za uchaguzi (tume ya Muungano na ile tume ya Zanzibar). Kuna majimbo kura hazikutosha ,kuna kura zimeonekana mitaani hata kabla ya uchaguzi ,kuna sehemu uchaguzi haukufanyika ,ni matayarisho gani hayo ambayo yalitayarishwa miaka mitano iliyopita na watu hawa wa NEC na ZEC wakiulizwa katika sehemu mbalimbali wanasema kila kitu kimekamilika.

Naona huu ni wakati wa kuhusisha mawakili wote wa vyama vya upinzani na kukusanya matokeo na kasoro zote zilizojitokeza na kuathiri uchaguzi ili hizi tume zifikishwe mahakamani kisheria kabisa ,bila ya kuoneana haya wala yale watu hawa wakiachiwa ndipo inapokuwa rahisi kuharibu uchaguzi makusudi ni lazima wawe na masuala ya kujibu kwenye mahakama zetu hizi na kama hela ya kuwashitaki haitoshi uanzishwe mchango wa shilingi tano au kumi na kwa mujibu wa mtu anavyoweza kuchagia ili watu hawa wapelekwe katika vyombo vya sheria.

Hii ni tabia ambayo vyombo hivi imevizoea tokea ulipoanzishwa uchaguzi wa vyama vingi na ikiwa hawatafikishwa kwenye vyombo vya sheria japo siku moja watazoea na itakuwa vyama vya upinzani vinadumaa na mwisho hata wananchi watachoka na watakuwa hawashiriki katika chaguzi zijazo kwani weshajua matokea hata kabla ya kupigwa kura kuwa CCM watachukua kila kitu na kugawa vile watakavyo wao.

Kila uchaguzi Chama kinachokuja juu huwa kinafanyiwa unyama huu wa kubadilishiwa matokeo na kupigwa na chini ,nafikiri ni bora hawa watu wa tume washitakiwe tu na nina hakika hawataikwepa sheria ,ikiwa ushahidi wa kuharibu uchaguzi huu ni wa uhakika na uwazi kabisa ,basi ni lazima wataishia jela ,hivi ni wananchi wangapi walijiandikisha na walipokwenda kuhakiki wanakuta majina yao hayapo ,ni wangapi majina yalikuwepo walipokwenda waliambiwa waende kwenye sehemu nyingine na huwa wanahangaishwa na kuwakatisha tamaa ni matokeo mangapi yamebadilishwa na kutangazwa sivyo ? Naamini kabisa Tume zikijua wanachokitangaza sio tokeo la uhakika ,kwa maana hiyo walikuwa wanatenda makosa ,ni lazima waadhibiwe.

Ila watu hawa watakuwa na tofauti gani na mafisadi ? Kwa maana watapeta tu ,lakini ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.
 
Nimekupa asante yangu kwa sababu leo umegusa source ya problem na siyo symptoms kama Malaria Sugu afanyavyo!
 
Back
Top Bottom