SERGIO
JF-Expert Member
- Dec 13, 2012
- 348
- 145
Kama mnataka haki basi Dk.Slaa, Juliana Shonza na Zitto Kabwe waondoke madarakani kwa muda hadi uchunguzi ukamilike, vyenginevyo itakuwa ni kukiuka misingi ya haki na usawa katika sakata hili
Huwezi kamwe kutegemea Juliana Shonza awasilishe ushahidi wake dhidi ya Slaa katika kikao kinachoongozwa na Slaa, na haki itendeke.
Nashangaa kwa nini unashupalia Dr Slaa naye akae pembeni kupisha uchunguzi wakati unajua kwamba hajawahi kujihusisha na upuuzi wa kutoa au kujibu tuhuma hizi kupitia mitandao ya kijamii. Tunataka waliotoa tuhuma dhidi ya uongozi, kinyume na katiba na kanuni za chama, wapeleke vielelezo na kisha uchunguzi ufanyike. Zingatia kwamba kanuni na maadili ya CDM yanazuia kiongozi (kama Juliana) kutoa shutuma dhidi ya kiongozi mwingine nje ya vikao vya chama. Hilo ni kosa na ni lazima aadhibiwe kwa hilo kwanza, hata kama shutuma zake ni za kweli.