Hatua ya BOT kuhakikisha riba inayotozwa na mabenki inashuka, inahusu na riba ya mkopo ya wafanyakazi itayotolewa na Mabenki ya Biashara?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,035
144,386
Nimesoma taarifa ya BOT inayoongelea kushusha riba kwa wakopaji katika mabenki ya kibiashara lakini nimeshindwa kuelewa kama punguzo hilo litagusa mikopo inayotolewa na mabenki kwa wafanyakazi

Nauliza hivi kwasababu taarifa ya BOT inaongelea punguzo kwa sekta binafs pamoja na sekta ya kilimo.Sasa najiuliza mikopo ya wafanyakazi ni sehemu ya hiyo mikopo ya sekta binafsi iliyotajwa katika taarifa hiyo?

Waandishi wa habari kama waajiriwa, walishindwa kuuliza hata jambo linalowagusa wao wenyewe kama wafanyakazi?

Kama punguzo hilo halihusu wafanyakazi, je BOT watakuwa wametenda haki kwa wafanyakazi wa nchi hii?

Tukumbuke mikopo ya wafanyakazi riba zake katika mabenki ya biashara hufikia asilimia 16 mpaka asilimia 17.

Au ndio mpaka watumishi walalamike kisha Mama aunde kamati ya kumshauri juu ya hili?

Taarifa ya BOT kuhusu punguzo hilo la riba kwa sekta binafsi inapatikana pia kupitia uzi huu hapa chini:

Ndio inahusu pia riba ya mikopo ya wafanyakazi ambayo inajumuishwa kwenye kile kipengele cha mfuko wa shilingi trilioni moja.
 
Nilikwenda benki moja nikaambiwa mpaka sasa hawajapokea taarifa rasimi juu ya hilo na Meneja wa Benki akaonyesha wasiwasi kuhusu hatua hii ya BOT kama kweli itatekelezwa.
 
Yaani kama inahusu na watumishi, wacha nisiwe na papala nisubili mwezi wa tisa nifanye top up aisee maana hali si hali dah
 
Tatizo mabenki yanaweza kupunguza muda wa kukopa iwapo watashusha riba kufikia kiwango kisichozidi asilimia 10 kwa mwaka.

Wakipunguza muda wa kulipa mkopo, maana yake makato yataongezeka na kufanya lengo la kumsaidia mkopaji lisitimie kama lilivyokusudiwa hivyo nashauri BOT wahakikishe mabenki hayapunguzi muda wa watumishi kukopa.
 
Punguzo la riba linahusu bank zitakazo pata sehemu ya shs 1tr ambazo watakopeshwa kwa riba ya 3% na wao kuzikopesha kwa riba isiyo zidi 10% kwa PRIVATE sector. Siyo wafanyakazi ila wafanyabiashara. Kumbuka utaratibu huu una lenga kusisimua biashara...siyo kukopesha individual.

Kwa wafanyakazi wategemee punguzo ambalo litatolewa na ma bank husika baada ya kupunguza amana za bank zinazowekwa BoT kama guarantee. Hakuna unafuu wa moja kwa moja kwenye personal loans.
 
Hilo nalo neno, ngoja nitamuuliza meneja wa tawi la NMB hapa Mishap kesho..

Maana njaa zimezidi
 
Punguzo la riba linahusu bank zitakazo pata sehemu ya shs 1tr ambazo watakopeshwa kwa riba ya 3% na wao kuzikopesha kwa riba isiyo zidi 10% kwa PRIVATE sector. Siyo wafanyakazi ila wafanyabiashara. Kumbuka utaratibu huu una lenga kusisimua biashara...siyo kukopesha individual.

Kwa wafanyakazi wategemee punguzo ambalo litatolewa na ma bank husika baada ya kupunguza amana za bank zinazowekwa BoT kama guarantee. Hakuna unafuu wa moja kwa moja kwenye personal loans.
Bila shaka uko sahihi kabisa.
 
TAASISI KAMA BAYPORT,PLATINUM ETC HALI ITAKUAJE????NA KUHUSU MIKOPO AMBAYO NI TAYARI ILISHAKOPWA JE WATASHUSHA RIBA KWA MIKOPO INAYOREJESHWA????
 
Mikopo itakayoshuka riba ni mikopo inayohusu kilimo, kwa lugha rahisi hii inawahusu wafanyabiashara wa sekta ya kilimo. Kasome tena lile tangazo vizuri.
 
Sio kweli,.wewe ndio kasome vizuri hasa katika kile kipengele cha BOT kutenga trilioni moja(kipengele iv) kwa ajili ya kukopesha mabenki kwa asilimia 3 ili na benki zitoe mkopp isiyozidi riba ya asilimia 10.
 
Mzee wamesema kabisa kwa ajili ya mikopo ya kilimo, kama unataka kujipa matumaini ya uongo endelea kukaza shingo tu.
 
Punguzo la riba linahusu bank zitakazo pata sehemu ya shs 1tr ambazo watakopeshwa kwa riba ya 3% na wao kuzikopesha kwa riba isiyo zidi 10% kwa PRIVATE sector. Siyo wafanyakazi ila wafanyabiashara. Kumbuka utaratibu huu una lenga kusisimua biashara...siyo kukopesha individual.

Kwa wafanyakazi wategemee punguzo ambalo litatolewa na ma bank husika baada ya kupunguza amana za bank zinazowekwa BoT kama guarantee. Hakuna unafuu wa moja kwa moja kwenye personal loans.
Private sector ni pamoja na individual. Yeyote anaweza kunufaika na utaratibu huu. Ingawa hofu yangu ni kama benki za biashara zitakubaliana na huu utaratibu. Benki zinaweza kuamua kugoma na zishiriki kwenye utaratibu huu, na kupelekea lengo la BOT kutofikiwa. Inaelekea utaratibu huu ulifikiwa na BOT bila kushirikisha benki za biashara, ndio maana unaona mpake leo hii Benki za biashara hazina taarifa rasmi ya uwepo wa utaratibu huuu.
 
Back
Top Bottom