Hatimaye nimemjua na kuanza kumuona Mwenyekiti na Diwani wa Mtaani kwetu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Salaam ndugu zangu,

Nimekaa mtaani kwetu hapa takribani Miaka mitatu lakini sikuwahi kumjua Wala kumuona Mwenyekiti Wala Diwani wa Mtaani kwetu.

Tumekuwa tukipata shida za Maji, changamoto za kijamii lakini daima sikuwahi kumuona. Lakini Mwaka huu tangu uingie nimemuona zaidi ya mara tano.

Diwani amekuja na Diwani Cup, Mwenyekiti anaitisha vikao vya mtaa kusikiliza changamoto zetu.

Hapa najiuliza alikuwa wapi Mzee huyu. Kwanini amechangamka sana wakati huu kutaka kutusaidia.

Vipi huko mtaani kwenu viongozi wa Mtaa wameanza kujitokeza mwaka huu au wapo siku zote?
 
Back
Top Bottom