Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

Huwa hatatui chochote. Anachokifanya ni kukaa kimya tu na kuangalia upepo, na mwishowe watu, magazeti nk yatanyamaza. hana IQ ya kutatua migogoro on the face. Atawezaje wakati hao wanaovurugana ni mafisadi waliyomuweka? Ataanzia wapi?
 
Umri umemuondoa mtu mzigoni...
Umri tu???????????
Uwezo wetu wa kufikiri umevia
Majamaa mengine yana makashfa hata yaoge na tindikali hayatakati lakini bado yapo yanadunda
Dah Kama hupendwi CCM hata ukivunja glass bar unafukuzwa
 
Nahisi kuna chembe ya uadilifu kwa masauni. Rekodi zinaonyesha kuwa wapo wengi wana kasoro kama hizo lakini hawataki kujiuzulu nyadhifa zao. Woto kwao kuachia ngazi kwani tumeshawajua. Hawakuughushi majina tu, hata vyeti vyao na shule walizosoma zina utata mkubwa. Hongera masauni ila kaa chonjo na akina Moyo sio watu wema hao
 
DSC09235.JPG

Mimi nauliza huyu wa kwanza hapa ni shibe tu ndio awe hivyo? Halafu mtegemee kuwa asipigane kufa na kupona ccm ishinde? labda force/area na mi-sugar au mengine yammalize kabla ya ushindi. Ila kama tuko imara kwa mbio hatuwezi wala kwa umakini kwani wakati anahitaji milo kumi kwa siku, wengine tunahitaji mlo mmoja tu mida iliyobaki ni mapambano.
 
Duh Its increeedible by the way,

Sasa hili ni mmoja mbili lazima watalipizana kisasi kwenye kuwapigia kura za maoni wabunge katika majimbo yao hao UVCCM wanakotoka amini nawambieni mtashangaaa sasa na hii ndio mwanzo hao hao UVCCM wanapigana vijembe na ndio hao hao kwenye harakati za kupitisha majina ya wabunge katika maeneo yao ndio watakao tumika na watakuja na mtindo wao wasiku zote wa vi message na matusi na kashfa nyingi tuu yani UVCCM wanatunika vibaya sana na sio kuwa hawajui bali ni njaaa zao na kutokuwa na uimara na ummoja wao na kuendekeza majungu na chuki na fitna ndani ya UVCCM kiha ni wote kutaka madaraka ya kupewa kama mwana JF hapo juu alivyosema wanawania kupewa Ukuu wa wilaya na nafasi zinginezo kama ubunge wa kuteuliwa jamani mmmh ivi mapinduzi ya kisiasa yakuja lini ndani ya UVCCM mtaburuzwa mpaka lini na kauli au sera za watu wachache kwa manufaa yao na yenu nyie kundi dogo la UVCCM mnao jitenga na kuwakimbia wenzenu kisa kwa maslahi??
 
Masauni anasema wanampinga kwa sababu ya msimamo wake wa kusimamia rasilimali za umoja. Kwa kauli hiyo utagundua ugomvi huu ni kwa sababu ya hela. Ufisadi unaanzia awali kabisa!
Sababu ya kujiuzuru si umri kama wanavyodai umri umetafutwa juzi tu kama kisingizio tatizo hasa ni maslahi kama kawaida yao na bado yanakuja makubwa mtayasikia.
 
kuangusha sio tatizo, tatizo jee Uvccm au CCM itasambaratika kama nccr mageuzi baada ya kungatuka mrema?

Unashangaza sana MS: Anayeangushwa ni chaguo lako halafu unasema hakuna tatizo! Utawala gani huo? Na unajuaje iwapo CCM itatawala milele? Unayajua alivyopanga Mungu Mwenyezi katiuka siku zijazo? Au sasa utasema JK na CCM ni chaguo la Mungu? Kwa taarifa yako CCM inaweza kusamabaratika kupita hata NCCR na dalili trunaziona kila kukicha!

Kampigie kampeni JK kule kwa wale mamilioni waliojifunika mablanketi na wanaosubiri mashati ya kijani. wana njaa. Siyo humu ndaniu kwenye JF -- humu ni maji marefu kwako kihoja kitu kinachothibitishwa na hoja zako za kivivu!
 
Nakubaliana nawe kabisa. Lakini kwa upande mwingine, huyu mjamaa tumuachie na topic zake, kwani anasaidia sana kumpaka matope huyo mtu wake JK. Kuna mengi tuliokuwa hatujui sasa tunayajua kuhusu JK. GO ON MS.
 
kn sio kule tu, hata mujini Bongo, jiji lenye wajanja, lenye wasomi, wenye vyuo vikuu Jk anapeta. ndio maan hata Upinzani hapo kufa maji. sasa watz gani wasiomkubali Jk?

Huna uhakika kabisa na hili unalolisema. Tena kabisa! kama unategemea matokeo ya uchaguzi ujao, na bila shaka ndivyo unategemea, basi hapo ndipo umepotoka, kwani uchaguzi gani huo unaosimamiwa na NEC iliyachaguliwa na Mwenyekiti wa CCM? Wizi mtupu. Mwaka 2005 majina zaidi ya laki moja hayakuonekana katika daftari kule jimbo la Temeke peke yake, na NEC walikiri baadaye. Wengi wa wale hawakuona majina walikuwa wafuasi wa CUF, kutokana na walivyokuwa wanalalamika katika ofisi zao. WIZI mtupu.

Kwa kuwa umegusia NCCR mwaka 1995 NCCR ilihujumiwa hapa Dar na hiyo hiyo NEC kwa kutopeleka vifaa in time kimakusudi tu. (hili liliigwa ktk uchaguzi Visiwani mwaka 2000). WIZI MTUPU! Baadaye NEC ilikiri kufanyika hujuma, lakini ilikataa siyo wao. Mkoa wa Dar ulikuwa ngome ya NCCR mwaka huo. WIZI MTUPU!

Mwaka 200 mikutano ya CUF ilikuwa inapigwa mabomu ya machozi bila sababu yoyote, kionekane ni chama cha vurugu1 Woga wa CCM. WIZI MTUPU!!¬!

Tendwa kaamrishwa na JK kutoiandikisha CCJ kwa hofu ya kubwagwa! WIZI MTUPU na HUJUMA.
 
Inasemekana CCM zanzibar wanasema kuwa wanakusudia kumsusia Kikwete zanzibar na kwa kweli mwaka huu kama uchaguzi utafanyika kikwete anaweza kupatwa na bumbuwazi wa jinsi kura atakazozipata zanzibar. Mkuu kaya kuna fununu zinasema anataka kuhakikisha anashinda zanzibar kwa vyovyote lakini hana support ya CCM zanzibar kwani hawamtaki.
Mpasuko wa CCM bara na CCM zanzibar unazidi kuongezeka na usione ajabu Kikwete akapigiwa kura za chuki kwa ninavyowajua wazanzibari.
 
We have not yet passed from anger about what's going on in our political system to cynicism and alienation.
Thats what I gonna say!!!
 
Huna uhakika kabisa na hili unalolisema. Tena kabisa! kama unategemea matokeo ya uchaguzi ujao, na bila shaka ndivyo unategemea, basi hapo ndipo umepotoka, kwani uchaguzi gani huo unaosimamiwa na NEC iliyachaguliwa na Mwenyekiti wa CCM? Wizi mtupu. Mwaka 2005 majina zaidi ya laki moja hayakuonekana katika daftari kule jimbo la Temeke peke yake, na NEC walikiri baadaye. Wengi wa wale hawakuona majina walikuwa wafuasi wa CUF, kutokana na walivyokuwa wanalalamika katika ofisi zao. WIZI mtupu.

Kwa kuwa umegusia NCCR mwaka 1995 NCCR ilihujumiwa hapa Dar na hiyo hiyo NEC kwa kutopeleka vifaa in time kimakusudi tu. (hili liliigwa ktk uchaguzi Visiwani mwaka 2000). WIZI MTUPU! Baadaye NEC ilikiri kufanyika hujuma, lakini ilikataa siyo wao. Mkoa wa Dar ulikuwa ngome ya NCCR mwaka huo. WIZI MTUPU!

Mwaka 200 mikutano ya CUF ilikuwa inapigwa mabomu ya machozi bila sababu yoyote, kionekane ni chama cha vurugu1 Woga wa CCM. WIZI MTUPU!!¬!

Tendwa kaamrishwa na JK kutoiandikisha CCJ kwa hofu ya kubwagwa! WIZI MTUPU na HUJUMA.

You are damned right. Kiongozi yeyote anayeingia madarakani kwa wizi wa kura na ghilba nyingine dhidi ya wapinzani wake siyo kwamba anapendwa. Nashangaa MS anashikilia JK anapendwa huku ilibidi maswahiba waibe BoT ili kumpitisha, pamoja na kumfanyia hujuma mgombea mwenzake katika kinyang'anyiro cha 2005!
 
Nimjuavyo Jk Tangu achukue uenyekiti ndani ya CCM na Urais wa Tz, Mgogoro wa Uvccm uliopo sawa na gunia la usufi na sio chuma, yaani ni mwepesi kwake kuutatua, ataumaliza na utaisha salama salmin.
1) mgogoro wa SS na Lowasa and Rostam, Ameutatua
2) Zanzibar sio nchi. sasa kama hadithi, kautatua
3)tUCTA, nayo huo umeyayuka bila hata mabomu ya machozi
4)waraka wa wakatoliki na waislam. ameutatua na sasa kila kiongozi wa dini wamemkubali

anaebisha asubiri wiki chache zijazo

Goosh!

1 . tUCTA nini?

2. Mgogoro wa Zanzibar si nchi ulikuwepo lini?

3. Hivi hizi nyaraka zilikuwa ni migogoro pia?

Malaria Sugi au Sugu?
 
Jk katengeneza bifu na wafanyakazi!leo useme tucta nini?utashangaa safari hii ktk uchaguzi mkuu itakuwaje.
 
walaka umemfanya kuomba kukutana na viongozi wa dini last week,nakumbuka Marin Hassan alimuweka kati Marmo kama si kujitetea na kuweka mambo sasa kwa kuhofia elimu ya uraia itakayotolewa na taasisi pevu kama Roman walivyo fanya.
 
We ms huyu jk we umemjulia wapi? Mbona unashabikia utafiri we ni nyumba ndogo yake? Au ndiyo malaria imeshakuwehusha? Vibaya hivyo kumshobokea mwanaume mwenzio hivyo
 
Nimjuavyo Jk Tangu achukue uenyekiti ndani ya CCM na Urais wa Tz, Mgogoro wa Uvccm uliopo sawa na gunia la usufi na sio chuma, yaani ni mwepesi kwake kuutatua, ataumaliza na utaisha salama salmin.
1) mgogoro wa SS na Lowasa and Rostam, Ameutatua
2) Zanzibar sio nchi. sasa kama hadithi, kautatua
3)tUCTA, nayo huo umeyayuka bila hata mabomu ya machozi
4)waraka wa wakatoliki na waislam. ameutatua na sasa kila kiongozi wa dini wamemkubali

anaebisha asubiri wiki chache zijazo
malaria haiondoki kwa kugawa net.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom